Tetesi: Kumbe Mo Dewji analipa TZS 4,000 watu kwenye kampuni yake

buku 4 usafiri kwenda na kurudi, asubh Chai, mchana chakula na usiku, bili maji, kodi, umeme nk hiyo inasoma negative. Kama ni kweli posho ndiyo basi kila mwaka hatuvuki robo.
 
Hao ni vibarua wa ingia toka sio waajiriwa rasmi.

Kuna jamaa anaendesha magari ya MO kusafirisha mizigo mikoani.

Ananiambia mshahara wake kwa mwezi haufiki 400K ila alikataa mchongo wa 700K kwenye kampuni la Cocacola.

Na jamaa kwa kazi hiyo hiyo ya udereva amejenga na ana Noah yake safi.

Japokuwa katika namna inaonekana kuwa MO analipa kidogo lakini ndio imebaki kuwa kimbilio la wengi kuliko hata huko wanakolipa vizuri.

Hiyo ni kwasababu kuna mianya mingi ya upigaji na ndio maana wengi wanakimbilia huko kwasababu wanauhakika wa kupata kikubwa zaidi kuliko huko kwingineko.
 
Be
Hii ni tofauti dada wa kazi ni kama member wa familia coz anakula, anavaa, anaishi hapo hapo nyumbani(halipi kodi) akiumwa unamtibia...hii ni tofauti na kulipwa 4000 halafu kila kitu unajitegemea.
 
Mo kwa level yake kutumia vibarua wa ingia toka wanaoliopwa 4,000 kwa siku bado ni scandal.
 
Ni vigumu mno kufanya upigaji katika kampuni ya mhindi, yeye kwa sababu ni dereva labda itakuwa anapata dili za pembeni kutumia gari la kampuni na kumfanya aingize pesa za ziada.
 
Yes hao wa mizigo wanakula hela angalau, na wanakuwaga na nyodo hatari
Wa mizigo wanapiga sana hela.

Hawa wanaopiga trip town kama sales huwa wanapewa bonus kwa kufikisha idadi fulani ya mauzo.

Hiyo bonus naskia ni 200 kwa kila chupa. Yani kama umepewa Mo energy ukaziuze madukani halafu zikaisha basi kwenye kila chupa ya MO energy uliyoiuza kutakuwa na 200 yako.

Sasa watu wanarudi na 100,000 kwa siku hapo hata mshahara mtu haufikirii.
 
Ni vigumu mno kufanya upigaji katika kampuni ya mhindi, yeye kwa sababu ni dereva labda itakuwa anapata dili za pembeni kutumia gari la kampuni na kumfanya aingize pesa za ziada.
Nani kakuambia??

Kaulize watu kabla ya kusema.

Kwa Bakhressa hakuna upigaji kwasababu most ya kazi inafanywa na mashine.

Kupanga soda, ku regulate kipimo cha soda na vitu vingine hiyo inafanywa na mashine lakini kwa MO ni watu.
 
Nani kakuambia??

Kaulize watu kabla ya kusema.

Kwa Bakhressa hakuna upigaji kwasababu most ya kazi inafanywa na mashine.

Kupanga soda, ku regulate kipimo cha soda na vitu vingine hiyo inafanywa na mashine lakini kwa MO ni watu.
Kibarua anaweza kutoka na katoni ya soda kwa Mo?
 
Hizi kazi za viwandani bongo kumbe karibia zote ni sweatshops tu, hazina tofauti na utumwa wa hiyari.
It's vicious circle of poverty.
Boss kulipa mishahara mikubwa ni gharama hii nchi, ukiongeza mishahara umejiongezea gharama za ziada za uzalishaji nje ya hilo ongezeko la mshahara.

Kuna approx 15% inayoenda kwenye mifuko ya jamii, sdl, wcf ya mshahara anayolipa.

Yaani kama unalipa mishahara 100,000,000 kwa mwezi, kwa wewe kuilipa hiyo M100 kuna Approx M15 zitaenda kwenye mifuko ya jamii na mamlaka nyingine za serikali.

Sasa ukifanya iwe M200 inamaana kuna M30 nje ya ongezeko la M100 umeiongeza kwenye gharama za uzalishaji.

Ni maamuzi yanayoleta gharama sana kuongeza mshahara so mara nyingine wanalipwa off records. Kwenye makaratasi unaonekana umelipwa 250,000 ila unakuta huo mwezi umeondoka hata na 500,000 ya marupurupu, posh n.k

Ndo maana unakuta mtu haachi kazi wakati ukipiga hesabu ya nauli ya kumfikisha hapo kazini tu mshahara wake umeisha.
 
Hiyo ni kwasababu kuna mianya mingi ya upigaji na ndio maana wengi wanakimbilia huko kwasababu wanauhakika wa kupata kikubwa zaidi kuliko huko kwingineko.
Kuna madau aliniambia alikuwa Kampuni ya Wachina wenyewe kazi yao ilikuwa wakiondoka na gari wakifika njiani ni kupiga mafuta nyoka yaani kuyaiba kutoka kwenye tenki na kuweka kwenye madumu na kuuza (mchina ndio hivyo anaishia tu kuita watu Alibaba) ila vithibitisho hakuna... its a dog eat dog world (Matsya Nyaya) na hapo nadhani hawa vibaka ndio wanampiga mchina na sio vice versa...

Kuna jamaa aliniambia ukitaka kufanya kazi kwa muhindi wewe shati ulilokuja nalo usibadilishe kununua jipya na kila siku lia njaa (ukianza kuonekana nadhifu anajua unampiga) ila ndio hivyo jamaa kuhamisha mizigo store ni kama kawa...

Alishasema Expatriate mmoja baada ya kuona kipato cha mtanzania na maisha wanayoishi conclusion yeka ikawa wabongo wote wezi....
 
Mo kwa level yake kutumia vibarua wa ingia toka wanaoliopwa 4,000 kwa siku bado ni scandal.
Hapo mi sioni tatizo kwasababu mbona kuna wengine wanalipwa nyingi.

Vibarua ni ngumu kuweza kuwa control ndio maana ukiangalia katika takwimu utaona MO ana wafanyakazi 20,000.

Kwenye hao 20,000 waliopo kwenye takwimu ndio wanaolipwa vizuri. Kwa hiyo hata hao wataopewa hizo scandal nadhani wataangalia malalamiko kama yanatoka kwa hao 20,000

Vinginevyo maana yake hao sio waajiriwa wake na wala yeye hawatambui.

Halafu mbona ipo easy sana. Mfano mimi nimepiga kazi ya kusaidia fundi.

Fundi ndiye aliyefanya mapatano ya bei na boss. Walivyoafikiana, fundi akaja kunitafuta mimi akanipa offer yake nikaona inafaa nikakubali.

So nafanya kazi nikijua kabisa kuwa nacholipwa ni kiasi ambacho hakiendani na kiwango anachochukua fundi japo kiuhalisia mimi ndiye nayefanya kazi kubwa.

Sasa kwa hapo kuanza kumlaumu boss kuwa hayupo fair analipa vibaya sio sawa.

MO yeye anamlipa UPAMI ambaye wameingia mkataba. Maswala ya vibarua kulipwa shingapi hilo yeye MO halimuhusu cha msingi kazi yake ifanyike basi.
 
Sad reality. Kuna β€œajira” chache sana mjini hapa zinazowalipa watu angalau TZS. 10,000/- per day

No wonders dada zetu wengi wameresort kwenye kuuza mbunye zao. Options are limited
 
Sasa hii ndio ambayo jamaa anaifanya.

Jamaa anabeba mafuta ya kupikia anapiga root za mkoani na sometimes anapasua hadi kongo.

Faidi ya kwanza anapiga mafuta sijajua anatumia mbinu gani ila anapiga.

Halafu wakati wakurudi gari linakuwa tupu kwa hiyo analiegesha stendi anawaita wapiga debe wanampigia debe anapata watu wakusafirisha mizigo anawapiga hela ya kutosha akifika home tayari ana jackpot.
 
...wizi wizi wizi wizi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…