Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Tatizo Tanzania hakuna standard.Hapo mi sioni tatizo kwasababu mbona kuna wengine wanalipwa nyingi.
Vibarua ni ngumu kuweza kuwa control ndio maana ukiangalia katika takwimu utaona MO ana wafanyakazi 20,000.
Kwenye hao 20,000 waliopo kwenye takwimu ndio wanaolipwa vizuri. Kwa hiyo hata hao wataopewa hizo scandal nadhani wataangalia malalamiko kama yanatoka kwa hao 20,000
Vinginevyo maana yake hao sio waajiriwa wake na wala yeye hawatambui.
Halafu mbona ipo easy sana. Mfano mimi nimepiga kazi ya kusaidia fundi.
Fundi ndiye aliyefanya mapatano ya bei na boss. Walivyoafikiana, fundi akaja kunitafuta mimi akanipa offer yake nikaona inafaa nikakubali.
So nafanya kazi nikijua kabisa kuwa nacholipwa ni kiasi ambacho hakiendani na kiwango anachochukua fundi japo kiuhalisia mimi ndiye nayefanya kazi kubwa.
Sasa kwa hapo kuanza kumlaumu boss kuwa hayupo fair analipa vibaya sio sawa.
MO yeye anamlipa UPAMI ambaye wameingia mkataba. Maswala ya vibarua kulipwa shingapi hilo yeye MO halimuhusu cha msingi kazi yake ifanyike basi.
Hata Ulaya na Marekani watu wanatumia model ya kutumia consultants ambao si waajiriwa, lakini kuna mikataba ya kuweka standards kwa hao agencies wa consultants inayoweka standards fulani.
Mo Dewji kashindwa kuweka hizo standards. Kashindwa kutumia agencies zenye standards.
Jambo ambalo linaweza kuwa sawa Tanzania kwa sababu hatufuati standards, lakini Mo kashavuka standards za Tanzania kafikia ubilionea sasa hivi anatakuwa kujiongeza kwenda na standards za dunia.
Kwa sababu huko duniani mabilionea wenzake wakisikia anatumia watu wanaoliowa dollar 1.5 kwa siku hiyo ni scandal.