Tetesi: Kumbe Mo Dewji analipa TZS 4,000 watu kwenye kampuni yake

Tetesi: Kumbe Mo Dewji analipa TZS 4,000 watu kwenye kampuni yake

Watumwa walikua wanalishwa vizuri na sehemu ya kulala na mahitaji yote sana ilo wawe na nguvu Sasa huyu GABACHORI yeye anawalipa elfu 4000 na Kila kitu wanajitegemea huu ni zaidi ya utumwa
We inabidi uendelee kubaki na mizinga, watumwa wa sehemu gani hao walikuw wanakula vizuri wanalala vizuri? Wa Brazil, Wamarekani au Uarabani? Na unaijua vizuri hiyo biashara ilivyokuwa au unahadithiwa tu! Watu walikuwa mpaka wanavalishwa helmet kichwani wasile kama adhabu? Fanya research yako upya.
 
Jibu hoja bana acha kutetea
Ebu twambie kibarua kwa sku anatakiwa kuripwa shingp, sheria inasemaje

Inawezekana familia yake haijaajari mtu ata mmoja ila haiondoi hoja yake

Na kua muajiri mkubwa Tz sio tiket ya kuripa vibarua ujira mdogo na usioendana na sheria za ajira
Hakuna sheria inayotamka kibarua alipwe kiasi gani kwa siku,malipo ya kazi yoyote ni makubaliano baina ya mtoa kazi na muhitaji kazi na wala hakuna kutwezana nguvu katika hilo.
 
Hawa watu wenye asili ya Asia ajira wanazotoa inataka moyo sana. Mshahara kiduchu + matusi na masimango, nimewahi kufanya nao kazi, sababu maneno ya dharau almanusura siku moja tuzichape ngumu. Halafu ni wachawi haswa wanafanya sana matambiko sehemu za kazi .
 
Shitholes countries ,mmoja wapo ni hii ,shithole Country ambayo haina strict labour laws za kuhakikisha mazingira bora ya kazi ,haki na ujira wa kumuwezesha mtu kuishi , Tanzania watu wanafanya kazi katika mazingira mabovu hatarishi ,dhulma katika ujira na manyanyaso .
Capitalism ya third world countries aka shithole countries inaumiza sana raia wa kawaida .
Ni zaidi ya utumwa
Nchi gani hawalalamiki low wages ?
USA? Russia ? China ?

Suala la.low wages sio Tz ni dunia nzima, labda North korea ndio sijasikia wakipiga kelele, kwa sababu waliopiga kelele waliuliwa wote
 
Mtoa hoja unaweza kukuta hata mfanyakazi wake wa ndani anamkopa huo huo mshahara wa 15,000 kwa mwezi.
 
Uzuri ni kwamba,hawajalazimishwa,wenyewe wataamua kuacha kama ni mateso
Huyu anatesa sana Watanzania imagine.

Leo nimepita sehemu mada ni kwamba jamaa kiwandani kwake hapa Dar es Salaam analipa 4000 yaani elfu nne

Hivi wadau hii ni kazi au mateso na unakuta mtu anaamka asubuhi anaenda kuifanya aisee Mimi siwezi fanya huu ujinga
 
Sawa.

Lakini naona hujaelewa hoja yangu.

Soma mission statement ya "The Giving Pledge".

"The Giving Pledge is a promise by the world's wealthiest individuals and families to dedicate the majority of their wealth to charitable causes."

Mo Dewji amesaini The Giving Pledge kuwa atatoa sehemu kubwa ya hela zake kwa hiyari yake, buree, ziende kwenye charitable causes, kwa sababu anaamini katika falsafa ya kugawa sehemu kubwa ya utajiri wake kabla hajafa.

Ninashangaa inakuwaje mtu aliyetia saini "The Giving Pledge" kutoa hela zake kwa charitable causes, kwa msaada tu, anashindwa hata kuwalipa vizuri wafanyakazi waje?

Hizo hela ambazo angewalipa wafanyakazi wake kiuchumi wala hazikutakiwa kuongeza bei ya chochote, kwa sababu angeweza kuwapa bonus au mshahara ambao haujali sana market prices.

Kimsingi swali ni hili.

Kama una roho nzuri sana mpaka umeahidi kutoa dola bilioni moja kwa charitable causes mbalimbali, kwa nini usitumie dola milioni chache kati ya hizo kuwaongeza kidogo nishahara wafanyakazi wako wanaokuzalishia mali za biashara zako?

Mo Dewji kweli yuko serious kwenye hiyo giving pledge? Au anatuzuga tu?
Kwanza kuna uhitaji wa ku cross check Claim za mtoa uzi maana tayar kuna watu wawili wameshapost humu kuwa kiwango hicho sio sahihi kuna mmoja kasema malipo ni 7500 unakatwa 1500 ya chakula mchana
 
Back
Top Bottom