MADAM T
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 6,240
- 3,972
Tatizo ni lilelile!Mo analipa 4000x30 = 120,000
Ila kuna kampumi za ulinzi zinalipa 90,000 kwa mwezi na "makato ya kinyanyasaji"
Tatizo ni lilelile!Mo analipa 4000x30 = 120,000
Ila kuna kampumi za ulinzi zinalipa 90,000 kwa mwezi na "makato ya kinyanyasaji"
Ataachaje kumkopa na yeye analipwa elfu nne kwa siku!Mtoa hoja unaweza kukuta hata mfanyakazi wake wa ndani anamkopa huo huo mshahara wa 15,000 kwa mwezi.
Hawapo wako kwenye kazi zao walizosomeaSasa waliosoma si wafanye hizo kazi!
Sasa kumbe wasiosoma wanahitajika sana!Hawapo wako kwenye kazi zao walizosomea
Kulipwa vizuri ndo shilingi ngapi?Sio kubeza, hapa tunataka kila mtu alipwe vizuri
Duh,hiyo 4000 unayoikandia binadamu wenzetu wanafanya maisha na kusomesha watoto zao.
Kwa hiyo hao wanaliopwa 4k sio watanzania!?
Duh,
4000 X 30 = 120,000/= kwa mwezi..
(kama unahudhuria siku zote 30).
Je, hiyo inatosha kufanya maisha na kusomesha juu?
Badala ya kusomesha , sijui kuchimba na blah blah nyingi . Awekeze hizo hela kwa hao wachache awalipe mishahara inayoeleweka wafanye miradi.Shida ni kujiona wewe ndio Mtanzania zaidi na unauchungu mno na Watanzania wakati hauna unachowasaidia...huyo huyo Gabachori anasomesha zaidi ya Watanzania zaidi elfu 10 kwa mwaka,anagharamia matibabu ya watoto wa Watanzania wenzake wenye ngozi nyeusi kitengo cha Saratani Ocean Road,Amechimba visima vinavyowapatia maji safi na salama Watanzania wenzake wenye ngozi nyeusi kariibu mikoa mingi yenye vijiji vyenye shida ya maji...Mtanzania wewe umesaidia kipi kwa watanzania wenzako wanaolipwa 4000 kama unavyodai??
Unamsifia mtu anaewalipa Watanzania wenzako 4000 hivi unamaanisha kweli?Wakati unamlaumu Mo kulipa 4000, unaweza kutuambia wewe na familia yako mmetoa ajira ngapi kwa Watanzania hata za kuwalipa 2000 kwa siku?
Kwa taarifa tu kwako ndio muajiri mkuu katika sekta binafsi Tanzania na hiyo 4000 unayoikandia binadamu wenzetu wanafanya maisha na kusomesha watoto zao.
Lastly naona damu ya kibaguzi imekujaa mwilini na kujiona wewe ndio Mtanzania zaidi kuliko Mo kisa rangi ya ngozi yako sio?
Mwaka 2009 mwalimu daraja iiiC alikuwa analipwa Tsh 170000 kwa mwezi na hapo chakula unajitegemea hiyo ni sawa na Tsh ngapi kwa siku? Hapo ni serikali ndiyo ilikuwa inalipa hivyo Sasa unataka mtu binafsi alipeje kama serikali unayoipelekea kesi yenyewe inalipa kiduchu?Matajiri karibu wote WA kiafrika Huwa ni wanyonyaji sana Kwa wafanyakazi wao!
Yaani Huwa wanafanya ile total exploitation of labor.
Na hii ni Kwa sababu ya ukosefu mkubwa wa ajira uliopo kwenye hizi nchi zetu ambapo watu wengi wako tayari kufanya kazi Kwa ujira wowote ule mradi wapate kula tu na sababu nyingine ni kutokuwepo Kwa mamlaka za usimamizi wa haki za wafanyakazi ambazo zingeweza kufanya kazi Kwa ufanisi.
Kiukweli kumlipa mtu 4,000/= Kwa siku haingiii akili hata kidogo hata kama kazi yake ni kukufutia vumbi tu ofisini.
Anzisha kiwanda Kisha lipa 15 per day na chakula kiwe juu yako tuone kama kitachukua hata miezi mitano hujafilisika.Heri usiajiri watu kwa kuwalipa ujira wa wizi huo ni utumwa kama utumwa mwingine na wote hao wanafanya kazi kwa sababu hawana namna yaani wanatumikishwa tu.
Tatizo mnadharau mno unadai nani kafanya maisha kwa hizo takataka unasahau Millard Ayo alikuwa analipwa Tsh 20000 pale ITV Leo ana millions of money,Nani kafanya maisha Kwa hizo takataka za kulipwa 4000 labda mwizi anazuga tu humo
We mjinga kweli Sasa millard ayo ni tajiriTatizo mnadharau mno unadai nani kafanya maisha kwa hizo takataka unasahau Millard Ayo alikuwa analipwa Tsh 20000 pale ITV Leo ana millions of money,
Kuajiriwa ili utajirikie humo ni kuwaza kijinga sana hata wewe huwezi kuajiri watu ili watajirike kupitia unachowalipa ,ishu ya kupata good life ni yako mwenyewe tu sio ya kutegemea ulipwe
Na huo ndiyo mpango mzima.Na ikibidi wasirudi tena wakatafute watakapolipwa zaidi inayoendana na matakwa yao.
Mbona sijaona viashiria vyovyote vya ubaguzi kwenye UZI wa jamaa? Labda tunatofautiana mitazamo; mimi nilivo muelewa, ni kwamba kaitazama status ya MO na bidhaa anazo zitengeneza, hafananani na havifanani na hiyo Tsh 4000/= Sijaona ubaguzi hapo hata kidogoLastly naona damu ya kibaguzi imekujaa mwilini na kujiona wewe ndio Mtanzania zaidi kuliko Mo kisa rangi ya ngozi yako sio?