Tetesi: Kumbe Mo Dewji analipa TZS 4,000 watu kwenye kampuni yake

Kwahiyo ni kosa la Mo kulipa hivyo? Unajua serikali yako inasema kima cha chini cha mshahara sekta binafsi ni sh ngapi?
 
Duh,
4000 X 30 = 120,000/= kwa mwezi..
(kama unahudhuria siku zote 30).

Je, hiyo inatosha kufanya maisha na kusomesha juu?

Mkinyimwa ajira ooh watu weupe wanatubagua, ila kwa mtu mwafrika kawaida, sijui mnataka nini aise.
 
Mwafrika akikulipa hiyo 4000 je utakuja kulalamika! Au vile mtu mweupe ndio mnamunzishia na mada! Duh sijui ni lini ubaguzi utatoweka!
 
Badala ya kusomesha , sijui kuchimba na blah blah nyingi . Awekeze hizo hela kwa hao wachache awalipe mishahara inayoeleweka wafanye miradi.

Na kwakuwa najua utaniuliza nimeajiri wangapi , nina kampuni mbili tofauti , na hamna mfanyikazi analamba chini ya laki tatu na nusu.
Labda cleaner ndo namlipa 300k na ni mmoja tu na hafanyi siku nzima , akimaliza shughuli zake huwa anasepa zake.
 
Unamsifia mtu anaewalipa Watanzania wenzako 4000 hivi unamaanisha kweli?
 
Mwaka 2009 mwalimu daraja iiiC alikuwa analipwa Tsh 170000 kwa mwezi na hapo chakula unajitegemea hiyo ni sawa na Tsh ngapi kwa siku? Hapo ni serikali ndiyo ilikuwa inalipa hivyo Sasa unataka mtu binafsi alipeje kama serikali unayoipelekea kesi yenyewe inalipa kiduchu?
yaani wewe unataka serikali ilazimishe mtu kulipa pesa Fulani wakati yenyewe tu ni choka mbaya?
 
Nani kafanya maisha Kwa hizo takataka za kulipwa 4000 labda mwizi anazuga tu humo
Tatizo mnadharau mno unadai nani kafanya maisha kwa hizo takataka unasahau Millard Ayo alikuwa analipwa Tsh 20000 pale ITV Leo ana millions of money,
Kuajiriwa ili utajirikie humo ni kuwaza kijinga sana hata wewe huwezi kuajiri watu ili watajirike kupitia unachowalipa ,ishu ya kupata good life ni yako mwenyewe tu sio ya kutegemea ulipwe
 
We mjinga kweli Sasa millard ayo ni tajiri
 
Lastly naona damu ya kibaguzi imekujaa mwilini na kujiona wewe ndio Mtanzania zaidi kuliko Mo kisa rangi ya ngozi yako sio?
Mbona sijaona viashiria vyovyote vya ubaguzi kwenye UZI wa jamaa? Labda tunatofautiana mitazamo; mimi nilivo muelewa, ni kwamba kaitazama status ya MO na bidhaa anazo zitengeneza, hafananani na havifanani na hiyo Tsh 4000/= Sijaona ubaguzi hapo hata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…