Uchaguzi 2020 Kumbe sera ya Bima ya afya kwa watanzania wote Tundu Lissu ka copy kutoka Ilani ya CCM!

Uchaguzi 2020 Kumbe sera ya Bima ya afya kwa watanzania wote Tundu Lissu ka copy kutoka Ilani ya CCM!

Kweli uelewa ni tatizo..., Bima ni nini ?, unadhani UK yenye National Health Service inamiliki hospitali zote ? Au unadhani OBAMA CARE ilikuwa ni serikali kujenga hospitali ?

Kuna kitu kinaitwa ruzuku, kwahio mapato au kodi zinaenda kutoa huduma, au unadhani tukijenga majengo ndio madaktari watakuwa wanafanya kazi bure au vidonge na dawa zitakuwa zinatoka kwenye hayo majengo kama chemichemi
Mkuu msamehe,huyo ni mwanaccm
 
Wasalaam

Leo Mama Samia akiwa Mwembe Yanga huku JPM akiwa Mara kule Kassim Majariwa akiwa Arusha....hakika CCM haina mpinzani!


Leo profesa Kitila Mkumbo ameweka wazi kuwa suala la bima ya afya kwa wote ni utafiti uliofanywa na CCM chini ya Wizara ya Afya na liko kwenye ilani na amekwenda mbele zaidi kutaja hadi kurasa!

Amesema wazi kuwa CHADEMA wamelidandia tu hawana uwezo wala wataalam wa kuweza kulielezea maana ukiwasikiliza kila mtu anaona halitekelezeki na akasema ukisoma Ilani ya CCM ya mwaka huu utaona limewekwa wazi kabisa suala la huduma ya afya au bima ya afya kwa wote na wameeleza kitaalam jinsi litakavyo tekelezwa!

Amesema wazi kabisa chadema ni wabobezi wa kutamka lakini kutekeleza hawana uwezo kwa kuwa ni ukweli ulio wazi hakuna jambo wanaweza kutekeleza hata ambalo wamewai kuliahidi kwa wanachama wao hakuna walio litekeleza maana wao wanachojua ni kutaja hila hawajui hata jinsi ya kupata hela hata kupanga ya kwao!

Mimi naungana na Kitila mkumbo kuwa CHADEMA hawana uwezo wa kutekeleza hilo wala hawana mkakati wala kutekeleza hiyo bima ya afya kwa wote kama ilivyo chambuliwa kwenye ilani ya CCM!

Wasalaam
Na waliokuwa wanampinga Lissu kwamba universal health care haiwezekani ni wanachama na mashabiki wa chama gani?
 
Back
Top Bottom