Kumbe Tanzania ilikopa fedha World Bank kuendeleza bandari, DP World anakuja kutumia fedha hizo kufanya kazi ambayo Tanzania imeikopea fedha WB-SOMA

Huyo mkurugenzi wa bandari kaongea maneno na fikra zake tu, lakini mengi aliyoongea hayako popote kwenye mkataba, hivyo muwekezaji hafungwi popote kuyatekeleza.

Jiulize haya yote aliyosema mkurugenzi wa bandari.
Je, yanahitaji kwa lazima muwekeza binafsi ili kuyatekeleza?
Je, serikali haiwezi kuyatekeleza?
Je, yanahitaji mkataba wa milele kutekelezwa?
Je, yanahitaji muwekezaji kupewa bandari zingine zote ili yatekelezwe?
 
Nimekwambia uelewa wako umekomea hapo... sasa DP world anakuja kuwekeza nini? Unajua maana ya kuwekeza?
Kwa hiyo ni wewe tu hapa Tanzania ndo unaejua physical meaning ya kuwekeza? mfano sema specific kwenye huo mkataba tatizo ni nini? na je kwenye mataifa yote DPW walikowekeza nao hawajui maana ya uwekezaji?
 
Mkuu Ina maana $21 Million ndio mtaji wa kuendesha bandari ya Dar es salaam?

Then alichopost Maria ni consultancy services za DP world kuandaa mfumo na sio kuendesha bandari. Ni mambo mawili tofauti kabisa
 
Wewe ni uchafu. Yaani wewe ni takataka
 
Source vipi ?
 
Kwa hiyo ni wewe tu hapa Tanzania ndo unaejua physical meaning ya kuwekeza? mfano sema specific kwenye huo mkataba tatizo ni nini? na je kwenye mataifa yote DPW walikowekeza nao hawajui maana ya uwekezaji?
Yaani mpaka leo hujui kwenye mkataba kuna tatizo gani!!? Wewe ulitakiwa uwe milembe
 
Basi serikali iseme inakodi kampuni ya kusimamia uendeshaji wa bandari kama vile Mkapa alivyowaleta Net group Solution waendeshe TANESCO na isiseme inaleta wawekezaji. Maana hakuna wanachokuja kuwekeza
 
Wewe ni uchafu. Yaani wewe ni takataka
Leta hoja leta ujinga bandari imeka miaka mingapi hatuna faida nao wakati serikali inahitaji pesa kununua dawa, na kutoa huduma kwa wana nchi
 
..badala ya kununua ma-V8 serikali ikajenge hiyo multi storage car park.

..tukiwaruhusu Dp wajenge hiki au kile iko siku watakuja kutuliza.
Serikali kulipa madeni yake shida, kutoa huduma shida za jamii inajikwamua. Ikawekeze tena bandarini wakati kuna mtu yupo tayari. Ambae kwanza anaweka hela yake, analipia kodi ya eneo bandari, anagawana mapato yake na TPA, na anaongeza volumes za mizigo TRA ipate kodi zaidi kwenye forodha.

Na akisharudisha hela yake na kutupa uzoefu maeneo yenyewe aliyopewa anawarudishia TPA; unataka nini tena kama ndio serikali.

Issue hapo ni kuingia mikataba mizuri ya utekelezaji; lakini IGA aina shida yoyote.
 
Yaani mpaka leo hujui kwenye mkataba kuna tatizo gani!!? Wewe ulitakiwa uwe milembe
Unaleta cheap propaganda! Jibu swali tatizo specific ni lipi? Wewe si unao mkataba hapo?
 
Basi serikali iseme inakodi kampuni ya kusimamia uendeshaji wa bandari kama vile Mkapa alivyowaleta Net group Solution waendeshe TANESCO na isiseme inaleta wawekezaji. Maana hakuna wanachokuja kuwekeza
Hapana hao DP world wana kuja na mitambo yao pamoja na technology yao wana fanya oparation mantainance and investment manaake wata panua bandari iwe kubwa zaidi
 
Let us agree to disagree, usinilazimishe niamini unacho amini, hoja yangu ni kwa DP world itaongeza ufanisi na mapato serikalini yataongezeka.......sisi wabongo tumeshindwa kuendesha bandari kwa mda mrefu
Hivi hao wanaoendesha bandari wanapatikana kwa utaratibu gani?!

Sikubaliani na wewe kuwa Watanzania tumeshindwa kuendesha bandari. Labda ujisemee wewe mwenyewe lakini si ku- generalize.
 
Mtu ambae kazi yake ni kusimamia uendeshwaji wa bandari ya Dar na amekuonyesha kilichofanyika.

Mtu ambae atakuwa kwenye team ya concession agreement itakayoamua muda wa mikataba na share of revenue ya sehemu watakazowapa DPW.

Wewe unajua kushinda huyo mtu kisa Maria Sarungi amekwambia; wow just amazing.
 
Fikra ndogo sana!!

Kama ndiyo hivyo, basi tuwaulize Waingereza na Wajerumani kama wanaweza kurudi na kutufanya koloni lao, halafu wakatupatia maendeleo. Kama wakisema wanaweza, basi tubakie koloni lao milele. Tuingie nao mkataba usio na mwisho, maana tunachotaka ni wananchi wetu tu wapate huduma bora. Unalipnaje hilo bwana Covax?
 

..una mawazo mazuri sana.

..sasa labda ungetupa na mifano ya nchi ambazo Dp imefanya hayo uliyoeleza.

..ni nchi gani Dp waliwekeza, wakaendesha bandari, halafu wakarudisha thamani ya uwekezaji wao, na mwisho wakakabidhi bandari kwa nchi husika?

..Na sio lazima iwe Dp. Unaweza kutupa mfano wa nchi nyingine yoyote ambako hayo mema unayodai tutatafanyiwa na Dp yamefanyika?

..Kama suala la kuongeza UFANISI wa bandari yetu ushauri mzuri ni Dp kuwa management company na sio wamiliki na wajenzi wa miundombinu hapo bandarini.
 

kama ni ufanisi basi hata serikali yenyewe ibinafsishwe maana imeshindwa kuuleta huo ufanisi na yenyewe pia sio fanisi.
 


Kwani kitu mbaya hapo ni nini hao jamaa wa DP world wakipewa kuwekeza au kuisimamia Bandari yetu kwa mujibu wa Sheria?
Mbaya iko upande gani nami nipate kuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…