Kumbe Tanzania ilikopa fedha World Bank kuendeleza bandari, DP World anakuja kutumia fedha hizo kufanya kazi ambayo Tanzania imeikopea fedha WB-SOMA

Uuuwiiiiiiiiiii!!!!!Walaaniwe hawa viongozi wote waliohusika na ujinga huu wao pamoja na vizazi vyao. Ee Mungu ikupendeze,uwaondoe mmoja mmoja.
 
Tunaweza kufanya yote hayo wenyewe.

Si tunakopa tu kama SGR na JNHEP?
 
Nadhani tusikurupuke namna hii.Kama kuna hoja ya msingi ni vizuri kuijadili.Aliyekopa ni DP au ni serikali.na atakaye lipa ni serikali.Hao DP ni wakandarasi tuu.sema kandarasi imeingiwa kwa mtindo ambao una maswali mengi sana.

Halafu hii naona kama imekaa namna hii CEO ameasaini Framework Agreement halafu anairudisha kwa evaluation committeee wajiridhishe kama iko poa.Ili specific projects contracts zinaweza kuendelea.
 
Tunaweza kufanya yote hayo wenyewe.

Si tunakopa tu kama SGR na JNHEP?
Nchi imeshafikia threshold ya kukopa.

Magufuli was different nchi inapokuwa middle income ata status zake za kukopa zinapanda anaweza pewa mikopo sokoni na private banks.

Hatuko huko tena, sasa hivi mikopo ni ya IMF, WB na donor countries tu; tena ni kwa ajili ya kuziba budget deficit na miradi yao ya kusaidia nchi maskini. Ukipata huko ndio ufanya re-allocation ya matumizi.

Besides DPW ana uzoeufu na strategy yake ya bandari ni game changer kwenye kuifungulia biashara na ufanisi juu. Bandari kwa sasa kila tsh 10 wanayopata tsh 8.5 ni operation expense. Hizo taasisi za umma zikiachwa zenyewe huwa awaoni shida kutumia hela ovyo kwa sababu faida sio kipaumbele chao.

DPW ni mwarobaini hapo bandarini kama tunataka tu maximise matumizi ya hiyo bandari na nchi kuongeza mapato. Huo ndio ukweli wenyewe.
 
Sina Imani na ccm sio kwenye kuuza bandari zetu tu , hawa watu kila mkataba upitiwi upya ndio mamaana tunaomba Lissu popote alipo ajiandae kukabidhiwa ikulu.
 
Maoni yako ni sawa na maelezo uhalalai wa deal la EPA aaminiwe Lowasa na waliohusika kuliandaa. Hivi unategemea serikali ijipinge yenyewe? Hata wakati wanaingia mikataba ya na makampuni ya madini na gas ingetokea wapingaji bado serikali ingetetea kile inachofanya.
 
Bado.

Hivi majuzi tulifanyiwa tathmini na taasisi ya nje Wanasema tunakopesheka.

Waziri wa fedha nae akadai deni la Taifa ni himilivu, unless alikua anadanganya.
 
Let us agree to disagree, usinilazimishe niamini unacho amini, hoja yangu ni kwa DP world itaongeza ufanisi na mapato serikalini yataongezeka.......sisi wabongo tumeshindwa kuendesha bandari kwa mda mrefu

Hudhani kuwa utawala umetushinda ukiwamo urais?
 
Bado.

Hivi majuzi tulifanyiwa tathmini na taasisi ya nje Wanasema tunakopesheka.

Waziri wa fedha nae akadai deni la Taifa ni himilivu, unless alikua anadanganya.
We unawasikiliza wanasiasa B1+ ni junk bond; hakuna mtu atakukopa hapo ni default risk na akikukopa basi ni high interest rate.
 
Naijua Konecrane na nimeshapanda na kui Guide.

Kampuni zote kubwa zina Exclusivity usitegemee, kampuni XXX iingize Trilioni kadhaa Konecrane halafu mzigo huo huo wapewe kampuni YYY lazima kuwe na period ya miaka kadhaa watumie kisha wapewe na wengine,

pia kuna personalization nyingi sana zinafanywa. Kuanzia Software itakayotumika, size ya Bandari, Crane zitakazotumika, controller, sehemu za Kuhifadhia na mambo kibao, hivi vitu ni Complex sana.

Huwezi ku Achieve same System kama Dp world na player wengine wa kubwa wa Bandari. There is a reason kwanini bandari zote zinapewa kampuni binafsi mpaka Nchi ambazo hazi entertain hizi mambo kama China.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…