Kumbe Tanzania ilikopa fedha World Bank kuendeleza bandari, DP World anakuja kutumia fedha hizo kufanya kazi ambayo Tanzania imeikopea fedha WB-SOMA

Sasa kwanini tusiseme huna akili? Yani eti kwa credibility ya maria ? Aisee unamwamini kiasi gani huyo Maria unashindwa kuiamini serikali inayokwambia mambo yatakuaje? Hao wakina Maria ndio wanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja sasa endelea kuwaamini utaona mwisho wake wenzako wapo kazini wale.
 
Mama anaupiga mwingi mama anaona mbali 2025 hakuna mpinzani ndio maneno kenge fulani huongeaga mm nawatizama tu. Hata kama sote ni ccm lakini kusifia ujinga nimeshindwaga ccm imenipa pesa kwa kazi fulani lakini sio chanzo cha mm kuwasifia na kuwa chawa wao kisa ninafanya nao kazi
 
Mhh, ngumu kuamini hii
 
Hii serekali ya ccm labda kichaa ndio anaweza kuwaamini.
 
Ukisikia hela kumtawala mtanzania maana hana tofauti na maiti, maiti wenyewe ndiyo wewe na kundi lako, mnaotufanya watanzania tuzalaulike
 
Kwa hiyo kwenye haya, huyu muwekezaji atacontribute kitu gani?
 
Na hii ndio moja ya hoja za wananchi, kwama DP hatawekeza hata 100, ni pesa tulizokopa sisi ndio watatumia, na faida yote watabaki nayo wao, ila deni tutalipa sisi!
 
Let us agree to disagree, usinilazimishe niamini unacho amini, hoja yangu ni kwa DP world itaongeza ufanisi na mapato serikalini yataongezeka.......sisi wabongo tumeshindwa kuendesha bandari kwa mda mrefu
Lakini kama ni ufanisi mdogo, hauko bandarini pekee, bali ni taasisi karibu zote za umma. Kwanini hizo nyingine hakuna mwekezaji? Mfano mrahisi ni Uduni wa mahakama zetu. Kwanini tusiweke mwekezaji ili tupate ufanisi. Fuatilia vizuri utakuta huo mkataba ni wa viongozi wetu wako ndani, na hao waarabu wamekerwa kama bortion tu.
 
Let us agree to disagree, usinilazimishe niamini unacho amini, hoja yangu ni kwa DP world itaongeza ufanisi na mapato serikalini yataongezeka.......sisi wabongo tumeshindwa kuendesha bandari kwa mda mrefu
Kwahiyo tunakubaliana huyu hawekezi kitu si ndio?
 
Kilichosainiwa na kupitishwa bungeni ni nini?
 
Bado.

Hivi majuzi tulifanyiwa tathmini na taasisi ya nje Wanasema tunakopesheka.

Waziri wa fedha nae akadai deni la Taifa ni himilivu, unless alikua anadanganya.
Tunasahau haraka: tuliwahi ambiwa tunajenga kwa fedha zetu (mwigulu huyu huyu) leo vp? Tuliambiwa ni mzima anachapa kazi (ikawaje?), tuliambiwa umeme possible kwa 27,000/= (nini kilifata). But maisha kila mtu ana yake na kuwaamini ni hiari!
 
Let us agree to disagree, usinilazimishe niamini unacho amini, hoja yangu ni kwa DP world itaongeza ufanisi na mapato serikalini yataongezeka.......sisi wabongo tumeshindwa kuendesha bandari kwa mda mrefu
Mfano wasipoongeza hayo mapato na huku serikali inazidi kuweka pesa?
 
hapana sio kwa miaka mia uo ni utumwa we need win to win situation.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…