Kumbe Tanzania ilikopa fedha World Bank kuendeleza bandari, DP World anakuja kutumia fedha hizo kufanya kazi ambayo Tanzania imeikopea fedha WB-SOMA

Kumbe Tanzania ilikopa fedha World Bank kuendeleza bandari, DP World anakuja kutumia fedha hizo kufanya kazi ambayo Tanzania imeikopea fedha WB-SOMA

Wanajazana ujinga tu.
Kutwa kushindana kuanzisha threads mpya humu but ukisoma unakuta ni marudio kwa styles tofauti tofauti
Msigwa kaanzisha club house sio marudio hayo? Mkurugenzi wa bandari sio marudio?
 
Una uthibitisho wa hili?
DP World wanafanya kazi Kwa maslahi ya kibiashara pekee..
Lengo kubwa ni ku control trade kupitia mikataba yenye ahadi hewa na zisizotekelezeka..

Silaha Yao kubwa ni mikataba mibovu yenye kuwalinda ,Kinyonyaji na kutisha nchi zinazoingia Kwa ushawishi wa ahadi kemukemu..
Na wewe thibitisha tuhuma hizo
 
Let us agree to disagree, usinilazimishe niamini unacho amini, hoja yangu ni kwa DP world itaongeza ufanisi na mapato serikalini yataongezeka.......sisi wabongo tumeshindwa kuendesha bandari kwa mda mrefu
Kulikuwa na ulazima gani wa kuongeza kodi kwenye saruji, mafuta, magari n.k kama ufanisi ukiboreshwa bandarini, mapato yataongezeka?

Nchi ngapi zinaendeshwa kwa bandari tu na ziko mbali mno kiuchumi?

Kama lengo ni kuwa kama hizo nchi kwa kutumia bandari ya DPW, kwanini hatu-project kuwapunguzia wananchi utitiri wa kodi zisizo na kichwa wala miguu?

"Zidumu fikra za mwenyekiti" itategemea na mwenyekiti mwenyewe aiseee, huyu wenu, msikilizeni Ndugai
 
Let us agree to disagree, usinilazimishe niamini unacho amini, hoja yangu ni kwa DP world itaongeza ufanisi na mapato serikalini yataongezeka.......sisi wabongo tumeshindwa kuendesha bandari kwa mda mrefu
Umeshindwa wewe na familia yako!
 
..badala ya kununua ma-V8 serikali ikajenge hiyo multi storage car park.

..tukiwaruhusu Dp wajenge hiki au kile iko siku watakuja kutuliza.
Sure mkuu,kuna wahindi walikuja hapa kwa jina hilohilo la wawekezaji, tukawapa treni yetu,reli yetu,na fedha zetu,akina flani hawahawa wakawaimbia mapambio na nyimbo za kuwasifu,matokeo yake wote tuliyaona, leo tukiwauliza wale wahindi wana tofauti gani na hawa waarabu tunatukanwa!!
 
Hii ni kutoka report ya Worl Bank .................................BY MARIA SARUNGI

Muhimu kuhusu DPW na mradi wa Benki ya Dunia

Pesa za mkopo wa @WorldBankAfrica zimetumika (na kukamilika)
👉🏽 kupanua na kuimarisha Gati 1-7 na kujenga gati mpya Gerezani
👉🏽kupanua mlango wa bandari hadi Gati 11
👉🏽kuboresha na kuunganisha na reli
👉🏽 Kupanua na kuimarisha Gati 8-11
👉🏽Kuna RORO terminal ilijengwa na kukamilishwa

Sasa tuangalie wanachodai DP World kufanya kwa mujibu wa IGA
Cha kwanza kikubwa eti kujenga, kuendesha na kusimamia RoRo terminal na Gati 1-4 na gati 5-7
🙄
Yaani pesa zote zimewekezwa za walipa kodi kupitia mradi wa sasa wa WB alafu wao wanakuja kuendesha na kusimamia? Wanawekeza nini??

Ndiyo maana mkataba haujawekwa thamani ya uwekezaji wao 😄 kumbe wanadandia mradi unaoelekea kukamilika waje wajisifu!

YAANI KIUFUPI WANAKUJA KUTEKELEZA MRADI WA PESA ZA MKOPO WA WORLD BANK

Nyieeeeeeeeee!
Mnaotetea mkataba huu mnajua kuwa mnatumika kutetea ulaji wa genge ndogo!?
Ila #TutaelewanaTu
Wengi tunalijua hilo. Ni wizi na kupora bandari zetu. Mama hana budi kukatisha hili ama sivyo hatutamsamehe.
 
Unadhani DP WORLD Hizo Pesa watazitoa Wapi?!!! Au unadhani kuna mwekezaji anatumia his own money ? Usishangae yeye akatumia collateral ambao ni huo mradi kwenda kukopea kwa financiers kwahio mwisho wa siku ni asset yako wewe mwenyewe ambayo ime-facilitate huo mradi..
Mambo ya Leverage Buying, Man Utd wanalizwa na Glazer Family
 
Hao WB nduo wapuuzi wakubwa, kwa sababu mambo kama haya ndiyo wanayoyapigia chapuo sana kwa sasa hivi.

Wao WB wanachojari ni kuwa pesa yao italipwa tu basi. Hayo mengine ya nchi kunufaika au la hawana habari nayo.

Hawa WB na IMF ndio wanaowahimiza akina Samia wa dunia hii kuziuza nchi zao bila kujitambua.

Hawa ndio wanaotuingiza kwenye ukoloni mpya kwa lazima kwa jina la maendeleo.

Hii 'model' ya maendeleo hawatuonyeshi mifano ya nchi zilizoutumia muundo huo na nchi hizo zikapata maendeleo.
Walitushikia bastola kichwani kusaini mikataba yao ya mikopo au ni utashi wetu
 
Siyo hapo tu hata Taifa gas anawekeza 200 million dollars Kenya lkn fedha ni ya kwetu sisi ndiyo tume guarantee mkopo maana yake ni kwamba akishindwa kulipa deni anayedaiwa ni Serikali ya JMTZ na siyo Taifa gas ingawaje faida inakwenda kwake na ajira Kenya, think about that kama siuo evil ni nini?
Mhhhh, chanzo cha hii habari ni nini Mkuu
 
Kwa hivyo kusema watakuwa na mkataba kama wetu wakati aupo bado ni upotoshaji.

Kilichopo kwa sasa ni framework ya kuingia mkataba lakini hakuna mkataba wowote wa utekelezaji ambao wameshakubaliana mpaka sasa katika maeneo ya ushirikiano yaliyo orodheshwa.
Asante sana kwa ufafanuzi, Mkuu. Umeliweka vizuri.

Nikukumbushe tu kuwa baadhi ya viongozi wa serikali wanasema ni mkataba (Kuna mahali Waziri Mkuu alinukuliwa) ingawa hapa unatwambia ni framework (kiswahili chake sijui).

Sasa ninaomba kama itawezekana kutupatia frameworks ambazo zilitumiwa na nchi ambazo DP World wanaendesha Biashara Yao hasa kwenye hayo majiji uliyotaja. Lengo tuone kama na sisi tupo kwenye right track kuelekea kwenye "Rotterdam Mpya" !!!
 
Possible

Lakini serikali yako ipo restricted ndio kwanza credit ratings wameipa B+ it’s a junk bond hakuna bank atakayokupa hela. Wewe unabaki na makusanyo yako, IMF, WB na donor countries; kama source yako ya revenue.

Sasa kama DPW anaweza pata mkopo huko shida yako ni good terms za ‘project agreement’ na transferable skills anazowaachia vijana wako nchini muda wake ukiisha na kuamua kutokuongezeka.
Kuna mfano wa nchi alikowekeza DP W na kuwaachia wenyeji bandari hizo na ufanisi juu...

Hii mifano ingesaidia kuelewesha wasioelewa. La tunayoyaona ni mifano ya migogoro na kesi za mahakaman
 
Walitushikia bastola kichwani kusaini mikataba yao ya mikopo au ni utashi wetu
Ni utashi wa viongozi wetu wasiokuwa na maslahi nchi yetu.

Lakini pia elewa masharti yanayo ambatana na mikopo hiyo. Umejaribu kuangalia masharti yanayomtoa jasho jirani yetu hapo kaslkazini?
Siyo tofauti kubwa sana na "kushikiwa bastola kichwani" unakokueleza wewe hapa.

Unapokuwa huna njia ya kukataa "masharti" kutokana na hali inayokukabili, sini sawa na kushikiwa bastola?
 
Ni takwa gani la mkataba huo ni la hovyo? Taja nijifunze kitu
Niambie wewe, kwa mjibu wa mkataba, DP word anawekeza kwa mtaji gani kwenye bandari zetu?

Je, mkataba huo unachokipengele cha kutambua uwekezaji wetu na matrilion tuliyowekeza yamenyambulishwaje kwenye mkataba huo?

Niambie, ni lini ukomo wa mkataba huo?
 
Leta hoja leta ujinga bandari imeka miaka mingapi hatuna faida nao wakati serikali inahitaji pesa kununua dawa, na kutoa huduma kwa wana nchi
Mkuu,kumbuka kuwa shirika la reli lilidhoofu kabisa,na likakiza tu ile point ya kuitwa daktari ili athibitishe kuwa limekufa tulifukie, hatukuliuza,miaka mingi baadae akaja Magufuli na kulitoa kwenye comma na kulipa pumzi,leo trc ipo hai,japo ufanisi wake bado upo chini,la its promising,Tanesco ilishachoka beyond repair,haikuuzwa,leo mitaa inan'gaa usiku na mchana,Rtd ilshachoka dhoofu kabisa,hatukuiuza,leo tunaselebuka huku tukihabarishwa bila shida,sasa kwa nini suluhu iwe ni kuuza tu?kwani mama yetu Tanzania amekuwa tasa? Hawatazaliwa tena wenye mawazo chanya ya kukwamua kilichokwama? Ama kila kinachosuasua tukiuze tu? Think twice
 
Hii ni kutoka report ya Worl Bank .................................BY MARIA SARUNGI

Muhimu kuhusu DPW na mradi wa Benki ya Dunia

Pesa za mkopo wa @WorldBankAfrica zimetumika (na kukamilika)
👉🏽 kupanua na kuimarisha Gati 1-7 na kujenga gati mpya Gerezani
👉🏽kupanua mlango wa bandari hadi Gati 11
👉🏽kuboresha na kuunganisha na reli
👉🏽 Kupanua na kuimarisha Gati 8-11
👉🏽Kuna RORO terminal ilijengwa na kukamilishwa

Sasa tuangalie wanachodai DP World kufanya kwa mujibu wa IGA
Cha kwanza kikubwa eti kujenga, kuendesha na kusimamia RoRo terminal na Gati 1-4 na gati 5-7
🙄
Yaani pesa zote zimewekezwa za walipa kodi kupitia mradi wa sasa wa WB alafu wao wanakuja kuendesha na kusimamia? Wanawekeza nini??

Ndiyo maana mkataba haujawekwa thamani ya uwekezaji wao 😄 kumbe wanadandia mradi unaoelekea kukamilika waje wajisifu!

YAANI KIUFUPI WANAKUJA KUTEKELEZA MRADI WA PESA ZA MKOPO WA WORLD BANK

Nyieeeeeeeeee!
Mnaotetea mkataba huu mnajua kuwa mnatumika kutetea ulaji wa genge ndogo!?
Ila #TutaelewanaTu
report ya world bank by maria sarungi? pdf kama ipo ndio itasaidia
 
Back
Top Bottom