Kumbomolea machinga ni sawa na kumuachisha mtu kazi bila malipo yoyote

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Machinga kujaa kila sehemu mijini ni tatizo kubwa ila hoja ya kuwaondoa katika maeneo yao kiholela ni unyama usiofikiria athari za kimaisha kwa hawa watu na kujiuliza tumefikaje hapa tulipo?

Suluhisho la machinga ni kwa miji yote kutengeneza masta plani za miji na kuainisha maeneo ya wafanya biashara and then tutoe mda kama mwaka watu wahame kutoka maneneo ya sasa kurudi maeneo rasmi.

Umachinga ni maisha ya watu, kumbomolea ni sawa na kumsimamisha mtu kazi ghafla bila malipo yoyote, je huyu ataishije na familia yake?

Hoja ya kwamba wamekaa mahali pasipokuwa sahihi haina mashiko kwani ni lazima tujiulize wamefikaje hapa tulipo? bila shaka uzembe wetu wa kutotenga maeneo halali na kusimamia taratibu ndivyo vimetufikisha hapa.
 
Hadi unajenga kibanda sehemu isiyotakiwa, ulikuwa unafikiria nini?

Unajenga banda juu ya mtaro au sehemu imewekwa pavings za waenda kwa miguu, halafu unasingizia hakuna master plan!!!

Kuna maeneo kama Kariakoo, Mbezi Mwisho watu wameweka biashara zao juu ya lami, sasa hii inahitaji masterplan kweli?
 
Mimi naona hawa watu serikali kama itaamua kuwasaidia ni kukaa nao na kuwaambia kitambulisho kwa mwaka itakua 50000.Hiyo hela waitenge wanunue maeneo ama nyumba zilizo mjini penye mizunguko ya watu na serkali iongeze kiasi kidogo ijenge ghorofa pawe kwa ajiri ya machinga tu harafu ndo wahamishwe itasaidia kwa kiasi kikubwa kero za hawa watu ila sio kila mara kufukuza tu harafi sehem unazo wapeleka si rafiki kwa biashara.
 
Kabla hujaanza umachinga ulikuwa wapi? Kila mtu arudi alipotoka. Mje mjini mkiwa mmejipanga kufanya biashara kwa kufuata utaratibu.

Walikuwa jobless na wakaamua kujiajiri. bahati mbaya umachinga hauna mfumo maalumu ni popote unapoona wateja unawahudumia. Serikali iwarasimishe kwa taratibu za kudumu.

Watu wajue maeneo ya kufanyia biashara ni sehemu fulani na pale unapofanyia sehemu tofauti unachukuliwa hatua hapohapo. kwa sasa serikali ianishe maeneo maalumu ya biashara na izuie biashara holela na iwape mda wa kuhama kama mwaka mmoja.

Kwa mtu ambaye hajawi kuzunguka mwaka mzima na bahasha akitafuta kazi na hapati hawezi kuwaelewa machinga ila wengi wameangukia huko baada ya kukosa ajira.

Kijana ana familia inabidi aihudumie na labda kibarua kimekoma sasa anafanyaje? inabidi akauze chochote sehemu ambayo ana uhakika atauza. mama wa nyumbani kafiwa na mume hana njia huyo uji hata katikati ya barabara atauza ili watoto wale.

Shida kubwa ni kwa serikali kutokuweka utaratibu mapema kuwa ni marufuku kuuza chochote popote ili wale wanaolazimika kuingia huko waende maeneo maalumu.
 
Hadi unajenga kibanda sehemu isiyotakiwa, ulikuwa unafikiria nini?

Unajenga banda juu ya mtaro au sehemu imewekwa pavings za waenda kwa miguu, halafu unasingizia hakuna master plan!!!

Kuna maeneo kama Kariakoo, Mbezi Mwisho watu wameweka biashara zao juu ya lami, sasa hii inahitaji masterplan kweli?
Jaribu kupita na gari umburuze kwa bahati mbaya sasa, unaweza kuyaacha maisha yako pale pale. Machinga na bodaboda ni watu ninaowaogopa sana, hawana reasoning, wanakuuwa in just a minute.
 
Hadi unajenga kibanda sehemu isiyotakiwa, ulikuwa unafikiria nini?

Unajenga banda juu ya mtaro au sehemu imewekwa pavings za waenda kwa miguu, halafu unasingizia hakuna master plan!!!

Kuna maeneo kama Kariakoo, Mbezi Mwisho watu wameweka biashara zao juu ya lami, sasa hii inahitaji masterplan kweli?
Suala la kutafuta rizki ni kama vita, na vita haina macho.

Si kwamba naunga mkono uvunjaji wa sheria au Mtu kufanya mambo kiholela lakini sijui wewe utafanya nini pale utakapokuwa huna namna yoyote ya kupata rizki na unatakiwa tu kusimama pembeni na kumtazama Mwingine aliyeshiba akipita na Prado lake akiyafurahia maisha barabarani....kwa nini tusigombanie nae hiyo barabara?....akishinda vita ataniondoa au kuniua ila na mimi nikimshinda vita nitabaki hapo barabarani yeye akatafute kwa kupita na Prado lake.

Pia usisahau kwenye hili kuna pande mbili za kuwajibika, kabla hujatamani kuona ujinga wa Mmachinga au Mama mboga unapitiliza...vipi hao wenye Mamlaka waliomuahidi Mmachinga na Mama mboga kuwa atapata rizki yake kwa uhuru iwapo tu atamuwezesha kupata hiyo Mamlaka?.

Je Mamlaka mnatimiza wajibu wenu zaidi tu ya kujenga hizo barabara mnazotaka wakae nazo mbali na kuziogopa kama ukoma?.

Hivi mliwahi kujenga Viwanda ili hao wanaozagaa barabarani wapate njia mbadala ya kupata rizki zao, ili kesho ukiamka na kumkuta amesimama barabarani ndio umuwajibishe?.

Ni rahisi sana kwa Watu mnaoshiba kuona kama Machinga nikazi rahisi sana ya starehe na ya kujitakia tu ambapo mkiwaambia acha wataacha wakalale.

Mkitimiza wajibu wenu kila kitu kitakuwa sawa, mna rasilimali zote hata hiyo World Bank inawatambua nyie na si Wamachinga au Mama mboga...THINK na TIMIZENI WAJIBU WENU.
 
Machinga kujaa kila sehemu mijini ni tatizo kubwa ila hoja ya kuwaondoa katika maeneo yao kiholela ni unyama usiofikiria athari za kimaisha kwa hawa watu na kujiuliza tumefikaje hapa tulipo?

Suluhisho la machinga ni kwa miji yote kutengeneza masta plani za miji na kuainisha maeneo ya wafanya biashara and then tutoe mda kama mwaka watu wahame kutoka maneneo ya sasa kurudi maeneo rasmi.

Umachinga ni maisha ya watu, kumbomolea ni sawa na kumsimamisha mtu kazi ghafla bila malipo yoyote, je huyu ataishije na familia yake?

Hoja ya kwamba wamekaa mahali pasipokuwa sahihi haina mashiko kwani ni lazima tujiulize wamefikaje hapa tulipo? bila shaka uzembe wetu wa kutotenga maeneo halali na kusimamia taratibu ndivyo vimetufikisha hapa.
Ndani ya mwaka mmoja.atakua ameshajenga Banda la tofali na kuliezeka kabisa...usitegemee atahama huyo..dawa yake ni kuwabomolea ili wengine wenye mawazo ya kufungua mabanda kama Yao waachane na hayo mawazo
 
Je ni lazima tuendelee kuwa na Machinga ?

Yaani akili zetu tuwekeze ni wapi pa kuwapeleka au kuwapanga..., au busara zaidi ni kuhakikisha kwamba Tunakuwa hatuna Machinga.

Umachinga sio sifa wala watu hawafurahii kuwa machinga, ni kutafuta mkate wao wa kila siku..., kwahio kwa watunga Sera kuwapanga ili waendelee kuhangaika sio kuwasaidia wao wala taifa..., bali ni kama tu kufunika moto unaowaka kwa kutumia majani ili usionekane (lakini uhalisia ni kwamba unazidi kuchochea moto huo)
 
Ndani ya mwaka mmoja.atakua ameshajenga Banda la tofali na kuliezeka kabisa...usitegemee atahama huyo..dawa yake ni kuwabomolea ili wengine wenye mawazo ya kufungua mabanda kama Yao waachane na hayo mawazo
mantiki ya kumpa mwaka ni kumfanya ajiandae kutoka katika mfumo wa sasa na kuingia mfumo mpya. ajipange katika kipindi cha mpito ataishije na kama ni kutafuta kitu kingine cha kufanya aanze.

lakini na mamlaka husika ndani ya mwaka ziweke mazingira mapya kwa watu kuelekezwa eneo lenu ni hili na baada ya mwaka hakuna mtu kuruhusiwa kuuza ovyo mitaani. ndani ya mwaka watahamia na kuanza maisha mapya.

shida ni mambo ya ghafla yanaathiri maisha ya watu
 
Je unafahamu kwa mwaka wamachinga wangapi wanazalishwa...labda unambie kwamba waki aandaa huo mpango uzuie kabisa wamachinga kuzalishia kitu ambacho hakiwezekani...ukiisha mwaka mmoja ukihamisha hao..watakuja wengine kureplace hao waliondoka...huo mpango hautafanikiwa..Cha msingi watu wafanye biashara maeneo yanayoruhusiwa full stop...if huwawezi basi wakalime..kikichopo sasa hv vijana hawataki tena kazi vijijini kila mtu anataka kuja mjini kuuza soksi na leso na kukaanga chips barabarani
 
Mimi naona hawa watu serikali kama itaamua kuwasaidia ni kukaa nao na kuwaambia kitambulisho kwa mwaka itakua 50000.Hiyo hela waitenge wanunue maeneo ama nyumba zilizo mjini penye mizunguko ya watu na serkali iongeze kiasi kidogo ijenge ghorofa pawe kwa ajiri ya machinga tu harafu ndo wahamishwe itasaidia kwa kiasi kikubwa kero za hawa watu ila sio kila mara kufukuza tu harafi sehem unazo wapeleka si rafiki kwa biashara.

Sent from my SM-M305F using JamiiForums mobile app
Zile 20,000 za mwanzo zilifanya kazi gani? nchi haina mipango miji? Kila anayekuja anakuja na plan mpya?
 
Tatizo la machinga ni la serkali kupitia taasisi zake zote.
Hakuna mpango mji
Hakuna usimamizi wa sheria

Mtu amejenga sehemu isiyo sahihi lkn Serkali kupitia taasisi zake inapeleka hapo huduma ya Umeme. Hiyo maana yake Inabariki uovu.

Serkali inachukua kodi ya ardhi, kodi zote sitahiki. Ni sawa na kuchukua kodi kwenye madawa ya kulevya.
Kama ni HARAMU serkali isiombe hata mia. Ili hata kipavunja ijulikane ilichukuia.

Serkali ichukue hatua mwanzoni mwa tatizo, sio inaacha linakuwa na kuenea.
Mfano mtu amejenga kwenye service road, serkali za eneo kuanzia mtaa,kata hadi wilaya hawaoni? Inakuwaje wananyamazia.

Kwa sasa serkali lipe fidia kwa kuchuka kodi kwa shughuli zisiso halali. PERIOD
 
Hadi unajenga kibanda sehemu isiyotakiwa, ulikuwa unafikiria nini?

Unajenga banda juu ya mtaro au sehemu imewekwa pavings za waenda kwa miguu, halafu unasingizia hakuna master plan!!!

Kuna maeneo kama Kariakoo, Mbezi Mwisho watu wameweka biashara zao juu ya lami, sasa hii inahitaji masterplan kweli?
Hapo hata mm siwatetei
 
Sio Kila Mtu Nchi hii hutengewa Eneo la Biashara....Ni ajabu sana Kuwaza kwa ufinyu wa Mawazo ya aina hiyo kwamba Machinga asaidiwe..Kila mtu anawajibu kujipambania lakini afuate sheria za nchi....

Hamwezi Kujaza mabarabara yoote na mitaro kisa tu mtasema wanyonge hata huyu Mama asipowatoa atakuja Mwingine atawatoa... Ni sheria sio suala la mtu ni la kisheria.
 
...
Umachinga ni maisha ya watu, kumbomolea ni sawa na kumsimamisha mtu kazi ghafla bila malipo yoyote, je huyu ataishije na familia yake?
...
... hapo red ndipo hoja yako inapokosa mashiko! Watu hadi kujenga wamejenga halafu wanaitwa machinga? Umachinga ni kutembeza bidhaa mikononi na sio kuwa na permanent settlement.
 
Machinga kujaa kila sehemu mijini ni tatizo kubwa ila hoja ya kuwaondoa katika maeneo yao kiholela ni unyama usiofikiria athari za kimaisha kwa hawa watu na kujiuliza tumefikaje hapa tulipo?

Suluhisho la machinga ni kwa miji yote kutengeneza masta plani za miji na kuainisha maeneo ya wafanya biashara and then tutoe mda kama mwaka watu wahame kutoka maneneo ya sasa kurudi maeneo rasmi.

Umachinga ni maisha ya watu, kumbomolea ni sawa na kumsimamisha mtu kazi ghafla bila malipo yoyote, je huyu ataishije na familia yake?

Hoja ya kwamba wamekaa mahali pasipokuwa sahihi haina mashiko kwani ni lazima tujiulize wamefikaje hapa tulipo? bila shaka uzembe wetu wa kutotenga maeneo halali na kusimamia taratibu ndivyo vimetufikisha hapa.
Machinga anabomolewaje kibanda wakati tunajua machinga huwa anazunguka na bidhaa? Machinga yupi kavunjiwa kibanda?
 
Hoja dhaifu hizi, nchi haiwezi endeshwa kwa kubembelezana ikiwa vitu na sheria ziko wazi. Haya mambo ya kuleana ndiyo yametufikisha hapa. Machinga kazi yao ni kutembeza bidhaa mtaan, sasa huyo aliyejenga hadi makazi ya kudumu si machanga tena. Ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni viongozi kanyaga twende tumechelewa sana.
 
Machinga kujaa kila sehemu mijini ni tatizo kubwa ila hoja ya kuwaondoa katika maeneo yao kiholela ni unyama usiofikiria athari za kimaisha kwa hawa watu na kujiuliza tumefikaje hapa tulipo?

Suluhisho la machinga ni kwa miji yote kutengeneza masta plani za miji na kuainisha maeneo ya wafanya biashara and then tutoe mda kama mwaka watu wahame kutoka maneneo ya sasa kurudi maeneo rasmi.

Umachinga ni maisha ya watu, kumbomolea ni sawa na kumsimamisha mtu kazi ghafla bila malipo yoyote, je huyu ataishije na familia yake?

Hoja ya kwamba wamekaa mahali pasipokuwa sahihi haina mashiko kwani ni lazima tujiulize wamefikaje hapa tulipo? bila shaka uzembe wetu wa kutotenga maeneo halali na kusimamia taratibu ndivyo vimetufikisha hapa.
Tatizo huelewi kuwa wanaosababisha hii adha ni sisi ambao tunatumia daladala. Tuna tabia ya kufanya shopping tukitelemka kutoka katika daladala. Tukiacha tabia hiyo na wamachinga watahama. Hukomeshi tabia kwa kupambana na matokeo bali chanzo.
 
Huu mzozo wa machinga ulichochewa zaidi na mwendazake.

Aliwapa uhuru wa kuuza popote wanapotaka akawapa na gatepass ya kitambulisho kutimba popote pale.
Mjini walipigwa stop, lakini wakapewa uhuru wa kuuza popote sasa hivi posta ni kama kariakoo tu.
Serikali ijilaumu yenyewe kuruhusu madudu, saivi wakiguswa tu wanalalamika kuonewa coz dola iliyowarhusu ndio hiyo inawafurumua sasa hivi.
 
Back
Top Bottom