Kumbukumbu: Leo ni miaka 10 tangu Simba amfunge Yanga 5-0

Kumbukumbu: Leo ni miaka 10 tangu Simba amfunge Yanga 5-0

Mtani Shadeeya nadhani ulikuwa mpenzi wa somo la historia shuleni.

Practical yake ni kama hivi sasa.... na kukumbusha tu historia ni nini kwa lugha ya wazungu wa Uingereza

History is the study of the past, present in order to determine the future.

Naipenda historia😍😍
Hahahaaaa. Lol.
 
Tuwaombe TFF waongeze hizi goli 5 na points 3 kwenye msimamo wa msimu huu utatu boost
 
Mtani wangu Shadeeya na wengine niwape historia sasa ambapo Yanga ndiye alianzisha mbio hizi za magoli mengi ila akilipwa na kupewa nyongeza na mtani wake😁☝️


1. Yanga 5 vs 0 Simba, June 1, 1968

Yanga iliifunga Simba jijini Dar es Salaam mabao 5-0. Wakati huo Simba ikiitwa Sunderland. Mabao ya Yanga yalifungwa na Maulidi Dilunga (2) Salehe Zimbwe (2) Kitwana Manara (1).

2. Simba 6 vs 0 Yanga. July 19, 1977

Simba iliipiga Yanga mabao 6-0 jijini Dar es Salaam na ndiyo mechi iliyoweka rekodi ya mabao ambayo hadi leo hayajafungwa kwenye mechi za watani wa jadi. Ndiyo rekodi ya juu zaidi. Abdallah Kibadeni aliweka rekodi ya kufunga ‘hattrick’ kwenye mechi za watani akifunga mabao katika dakika ya 10, 42 na 89, Jumanne Hassan ‘Masimenti’ akifunga mawili, moja Yanga ilijifunga kupitia kwa beki wake Selemani Sanga.

3. Simba 2 vs 1 Yanga, July 23, 1988.
Hii sio mechi ya magoli mengi ila ina mambo yake mawili makubwa. Simba angefungwa angeshuka daraja na kama Yanga angeshinda au kutoka sare angetwaa ubingwa wa bara. Mechi muhimu kwa kila timu. Simba aliitundika Yanga mabao 2-1 na kubaki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara. Wakati Yanga ikihitaji japo sare pekee kutwaa ubingwa, Simba ilihitaji mno ushindi. Edward Chumila aliifungia Simba na Issa Athumani aliisawazishia Yanga kabla ya John Makelele ‘Zig Zag’ dakika ya 58 kuifungia Simba bao muhimu lililoibakisha kwenye ligi. Yanga ikakosa ubingwa uliokwenda kwa Coastal Union.

4. Simba 1 vs 1 Yanga. Machi 5, 2011.
Kama unavyoona, timu zilitoka sare lakini umuhimu wa hii mechi unakuja kufuatia matumizi ya VAR (TV).😁. Mwamuzi Oden Mbaga alilikataa bao lililogonga nguzo ya juu na kudunda chini, kabla ya kurejea uwanjani. Lilionekana si bao. Sasa ndani ya Uwanja wa Taifa, kwenye TV kubwa upande wa Kaskazini mechi ilionyeshwa mubashara. Wachezaji wa Simba walimfuata mwamuzi na kumtaka aangalie marudio. 🤣😍. Mpira ulionekana kwenye marudio ukivuka mstari wakati ukidunda chini. Mwamuzi alibadili maamuzi na kuweka mpira kati. Musa Hassan Mgosi ndiye mfungaji wa goli la kusawazisha, la Yanga likifungwa na Stefano Mwasika.

5. Simba 5 vs 0 Yanga. Mei 6, 2012.
Jijini Dar es Salaam na kwa mara ya pili Yanga ilikubali kichapo cha mabao matano (5G) bila majibu toka kwa Simba. Emmanuel Okwi hatasahaulika mitaa ya Jangwani kwa msiba huo kwani aliitesa, kuihadaa na kuivuruga kabisa ngome ya Yanga. Okwi alifunga magoli mawili, Patrick Mafisango, Juma Kaseja na Felix Sunzu. Kaseja na Sunzu walifunga kwa mikwaju ya penati.

6. Simba 3 vs 3 Yanga. Okt 20, 2013
Hadi mapumziko yaani dakika 45 za kwanza Yanga iliongoza kwa mabao 3 kwa bila yaani Yanga 3 vs 0 Simba. Wengi wakiamini Yanga anaenda kulipa kisasi cha 5G ya Mei, 2012 mambo yalibadilika kipindi cha pili. Simba ilipopata sare ya kishujaa.
Mechi ilipigwa jijini Dar es Salaam. Magoli ya Yanga yalifungwa na Mrisho Ngasa (dk. 14) na Hamisi Kiiza (dk 35, 45). Simba ilirudisha bao moja baada ya jingine kwa magoli ya Betram Mombeki (dk 54), Joseph Owino (dk. 57) na Gilbert Kaze (dk 83).

Hii ndio historia.
 
Mtani wangu Shadeeya na wengine niwape historia sasa ambapo Yanga ndiye alianzisha mbio hizi za magoli mengi ila akilipwa na kupewa nyongeza na mtani wake😁☝️


1. Yanga 5 vs 0 Simba, June 1, 1968

Yanga iliifunga Simba jijini Dar es Salaam mabao 5-0. Wakati huo Simba ikiitwa Sunderland. Mabao ya Yanga yalifungwa na Maulidi Dilunga (2) Salehe Zimbwe (2) Kitwana Manara (1).


Hii ndio historia.
Mtani kumbe sisi ndio waanzilishi wa hizo tano eee?
 
mnajifariji tu goli moja limewauma mno na leo mtalala na viatu mkimuota Feisaaaaaaaaalll!!

ngoja nikukumbushe mtani mechi ya goli 5 nadhani ilikuwa 2012 kulikuwa na mgogoro mkubwa Jangwani klabuni wa Yanga Asili na Yanga kampuni na siku moja kabla ya mechi Mzee Akilimali aliongea mbele ya TV mimi nikishuhudia akavua kofia akaweka juu ya meza akasema kwa hasira tutaona nani mbabe kesho derby!

msijisifu wala hamkuifunga Yanga kwa kuizidi ufundi bali maelekezo! fikisha kumbukizi hii Msimbazi wengi wenu hamuijui!!

ukinibishia nenda Jangwani kaulize wazee!
 
Back
Top Bottom