Kumbukumbu nzuri kwenye maisha yangu(Baba yangu)

Kumbukumbu nzuri kwenye maisha yangu(Baba yangu)

Awesome. Nadhani anafurahi huko alipo kwa ushuhuda huu. Apumzike kwa amani. Wababa wenzangu,tujitahidi kuwa na amani ktk familia zetu. Mbegu nzuri humea.
Kwakweli Hana deni na Mimi kabisašŸ˜
 
Hongera sana mkuu kwa kuwa na baba bora Mungu aendelee kumpumzisha pahala pema. Sisi wengine malezi ya Baba tunayasikia tu kwa watu but sitotaka mtoto wangu apitie hayo maisha namuomba Mungu sana
Pole sana njia nzuri kuufanya moyowako kuwa na amani ni kuwa bababora Kwa wanao
 
Ni Kweli lakin Kuna ambao hawakupata nafas kulelewa Kwa sababu za kibinadamu au mpango wa Mungu
Nina mdogo wangu Kwa mama Mkubwa nine years hajamuona Wala kwenda kumsalimia babayake na baba Hana time na mtoto na hawakai mbali sana nauli ni kmaa elf 20 tu
Kwahyo hapo inategemeana na bond iliyopo ya mshure na mtot?

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Baba yangu ni adui yangu namba moja.
Kama umetazama series ya Brigerton, chuki aliyonayo huyo mtu aliyopo kwenye avatar yangu kwa baba yake. Namimi ni hivo hivo.

No love from my daddy, 'cause the coward wasn't there
He went away and I didn't cry, 'cause my anger
Wouldn't let me feel for a stranger
-Dear Mama, 2Pac
Chuki ni mzigo mzito kwa anaye ubeba...hizo childhood traumas unaweza kuziachia mkuu.. ni rahisi mnoo,naweza kukusaidia.
 
Nawasalimu natumaini tukopoa na wagonjwa Mungu atujaalie afyazetu ziimarikemnisamehe Kam sitakuwa na mtiririko mzuri
Leo imekuwa sikunnzuri ya kumbukumbu nzuri maishani mwangu
Kama kitu nilibahatika ni kuwa mtotowake
Mama aliwahi kunambia kabla ya kuzaliwa kwangu babayangu alikuwa asiejali Kabisa kuhusu future yake ila baada ya mama kushika ujauzitowangu alibadilika sana
Nilivozaliwa na kuanza kupata akili sijawahi kumuona babaang akigombana na mama Wala kumrushia kibao marazote Huwa anarudi kazini mapema hata akichelewa Huwa lazima ale chakula Cha usiku na sisi

Nikiwa na miak 6 Nakumbuka nilipata ajali ya kukatwa na chupa mguuni nikicheza kwenye mvua niliumia vibaya alinibeba mgongon kutoka Kwa mfipa had tumbi hakuona aibu Wala hakujali watu watamuonaje na alihakikisha napata matibabu tukarudi wote akiwa kanibeba hivohivo [emoji3059]
Kipind hiki Cha ugonjwa sikuweza kutembea alikuwa anamsaidia mama kuniogesha akirudi kazin jioni na kunifundisha maana sikuwa naenda shule kabisa

Ilikuwa lazima Kila mwisho wa mwez arudi na vinywaji na nyama nyingi nyumbani
Alikuwa Mpenz wa supu na nyama choma hivo sikuhiyo tunabaki mm na yeye jikoni ananifundisha kuchoma nyama tunapika na ugali mama tunamuita aje kula tu [emoji7]

Licha ya kuwa mkali(jeshi) na kuwa na hasira lakini alikuwa hatoi adhabu Zaid yafimbo Kwa watoto,alikuwa anahakikisha mnaenda shule smart kufua kilasiku na kupiga pasi Ilikuwa ni lazima na akiona unazubaa anakupigia pas mwenyew

nakumbuka alishindwa kula sababu sikuonekana nyumbni Kwa mud nilopangiwa nilicheza kupitiliza alinitafuta sanaile siku na alivonipata hakuongea chochote Zaid y kunambia nikalale

Kiukweli maishayngu na babayngu yamenifanya niwe positive kilasiku Kwa wanaume naona nina bahat kulelewa na babayule pia nilikuwa naona namna anavopambana kuhakikisha tunaishi vizuri

Alipata ulemavu wa vidole viwili akiwa kazini ila nilielewa ni katika kuhakikisha tunakuwa katika mazingira safi
Sijawahi msikia mamayangu akimsema vibaya hata baada ya kifo chake
Matukio ni mengi sitaki niwachoshe [emoji3590]
Kiukweli Nina bahat sana
Natamani watotowangu wapate baba mzuri kama alivokuwa babuyao [emoji3059][emoji3059][emoji3059]
Na Mungu awalinde wanaume mnaolea vizuri watoto wenu
Nimegundua namna tunavolea watoto Ndio matokeo ya mienendo na tabia zawatoto zinavyopatikana

I didn’t have to go searching for a role model when I grew up, I’ve always had one since the day I was born–my hero dad is my first and only role model.ā€[emoji3590][emoji3590][emoji3590]
Allah aendelee kumpa kauli thabiti , mwanaume mwenzetu hakika alituwakilisha vizuri mno

Ninyi wenzangu na mimi tunalo la kujifunza hapa sio kutwa mikwara uchwala
 
Allah aendelee kumpa kauli thabiti , mwanaume mwenzetu hakika alituwakilisha vizuri mno

Ninyi wenzangu na mimi tunalo la kujifunza hapa sio kutwa mikwara uchwala
šŸ˜€Mikwara uchwara ipi Tena
 
Sawa mkuu, japo ni Asubuhi sana kuletea Chai mjengoni. Pamoja na kwamba ni chai ika umesaidia kuwakumbusha kuwa wanaume wanaojali familia zao wapo.
 
Wanaume tuna bahati mbaya sana kwenye hii sayari.....wengi tunakufa kabla hata hatujaona matunda ya juhudi zetu hapa duniani.
Hii inakatisha tamaa sana!
Kifo ni haki ya Kila mmoja mkuu usisikitike Kuna wanaokufa baada ya kuzaliwa tu
 
Sawa mkuu, japo ni Asubuhi sana kuletea Chai mjengoni. Pamoja na kwamba ni chai ika umesaidia kuwakumbusha kuwa wanaume wanaojali familia zao wapo.
Pole sana mkuu Kwa yaliyokukuta
Niletee chai Kwa faida ipi
 
nimeattach nyimbo hiyo kula chuma
 
Eti baba inabidi muda wote ndani umekunja sura [emoji16]

Eti baba mkipika nyama yeye ale kubwa kuliko wengine wakati ni wajibu kuwalisha watu wake yeye iwe badae

Eti ili uwe baba basi uwe mkali mkali
🤣🤣🤣Nimecheka
Au ukitak kumtisha mtoto utasikia ngoja baba aje uone🤣🤣
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Nimecheka
Au ukitak kumtisha mtoto utasikia ngoja baba aje uone[emoji1787][emoji1787]
Ndiyo hivyo sikatai kuwa sura nyingi za wababa ndiyo hutumika kumtisha mtoto alale ila ni wajibu kuwafanya watoto watuone marafiki regardless of our face
 
Back
Top Bottom