Dejane
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 50,587
- 71,492
Kuna kaka nilikutana nae kitaan wakati nasoma kipindi hicho akaniomba tutoke siku, nikakubali .Siku imefika kanifata hao tukaondoka picha linaanza tumefika sehemu kuna vinywaji na chakula akaniambia niagize chakula haya nikajiagizia ndizi na kuku choma. Sasa nikawa nashangaa mbona yeye haagizi akaniambia yupo fresh hana njaa anakunywa tu soda.
Chakula kimekuja nimekula kiasi nashangaa mzee baba nae kasogea anakula chakula changu yaani sahani moja ila mtu mbili khaaa nikamuuliza vipi tena? Ananiambia nakula kidogo tu [emoji47] jamani. Nikamuambia basi tuagize kingine akaniambia hamna anakula kidogo tu. Nilikula kiasi tu nikaacha yeye akamalizia chote. Nilipotoka pale akawa anapiga piga simu tutoke tena nikamuambia nipo busy sina nafasi khaaa tabia gani ile.
Au ile unatoka na mtu unashangaa anakuagizia kila kitu [emoji23][emoji23][emoji23] bor aaseme kuwa tuagize tutakuka wote inatosha
Ila pia inaweza kuwa hakuwa na pesa mngeshea kulipa ukaagiza nusu nyingine mle wote sio mbaya