Kumdhibiti mpenzi wako!!...ni woga au ndo mapenzi??

wasiwasi unakusaidiaje?,unakupa amani ya moyo? unaishi vipi na mwenzi usiemuamini?
simuamini mwanake!wasiwasi ndo silaha kabla mambo hayajawa mabaya niyadhibiti
 
ha haaa, na yeye haondoki, basi mmebaki mmegandana kama luba, lol!
ila mkishafikia uzeeni raha sana..... mnabaki kuwa marafiki tu
 
Dadaangu nakuelewa ila nataka tupanue mjadala na tuguse maeneo yote.
Kwa mfano hapa sidhani kama neno 'mipaka' linaweza kuwa sawa kwa watu wote.
Mfano unaposema kumdhibiti mwenzio ni ruksa mradi kuwe na 'mipaka'...Sasa mwengine aweza kuhoji mipaka hapa ni ipi?..Kwa mfano..kuna mwingine anataka kila jina kwenye phonebook ya mwenzi wake alijue ni la nani?..kwake huyu naye atakuambia sijavuka mipaka nalinda ndoa yangu..nadhani tafsiri ya 'udhibiti' ni pana sana.
Lengo kuu la mada yangu lilikuwa kujua hii 'motive' ya udhibiti inatokana na nini?..woga? au hisia mbaya tu?
Nashukuru umeieleza kwenye posts za mwanzo..lakini (kiuchokozi lakini) huoni kuwa mara nyingi 'woga' unaotokana na matukio ya wenzetu ndio unatupelekea huku kwenye udhibiti kuliko matuko halisi yaliyo kwenye mahusiano yetu???


 

Nyamayao unadhani sijui hilo dear?

Nikimwacha mdogo wangu wa kike atahalalisha kuwa ni mke na jamii inaweza ona sawa, na hata ndugu zake wanaweza wasiingilie kivilee, nikimwacha ndugu yake wa kike watafanya siri - ndugu zao wakijua panaweza kuwa hata padogo, na believe me you once najua narudi moja kwa moja huyo mwanadada namtafutia utaratibu ambao ni bora zaidi kwake - kama some sort of shukrani kwa kunilelea familia wakati sipo. For sababu najua tabia ya wanaume deep down within me naweza nikawa najiuliza kama they did it or not.

Mie najua, nikiwa mbali na mwanaume wangu for more than 6 months, yeye kuwa hajagusa mwanamke mwingine siwezi kuamini. Suala ambalo kwa kweli sipendi na linaweza niuma ni mwanamke aliyelala nae awe ndugu yangu. Alale tu anavyotaka (kwa heshima na nisijue) but ndugu zangu wa karibu naomba awaache tu. Inauma sana.
 
sidhani kama utataka hicho kwenye RED kitokee...
niliwahi soma hapa kuwa kuna watu wana simu zinakaa ofisini tu, hiyo namba wenzi wao hawaijui, ni special kwa ajili ya kuchakachulia mahusiano....
 
hapa tuelewane kuwa sijasema kukaa nje ya familia ni bora kuliko kuwa na familia unaweza kaa na familia na mambo yasiwe kama vile unavyotaka yawe, fanya kitu unachoona kinafaa kwa manufaa ya familia yako

Nilikuelewa kabisa, na lile halikua applicable wala si maelezo ya kua wanao kaa mbali na familia wanakosea. Nilikua nagusia vitu kama hivyo ni moja ya sababu huwakwamisha baadhi.
 
hapana dada yangu hata mi hayo maisha ya hivyo yananichefua na wala hayafai hata kidogo na huyo mzee wako alipitiliza na mara nyingi ukikuta mtu anamchunga sana mwenzie wallahi ukija kuambiwa yake unaghairi kusihi naye siku hiyo hiyo,pole dada Nyamayao ila tena hongera maanake naona uliamua kuuvaa uso wa mbuzi na kuwa an iron woman hapo nilipobold nimepapenda kwa kweli maanake kuna watu wanazidi aisee.
 
Last edited by a moderator:
ha haaaa, sisi hatukukutana disco lakini anajua wazi kuwa napenda mno disco......
yaani atakuwa hajanitendea haki kama kasafiri kwa muda halafu ategemee siku zote hizo nisiende disco. kwa hiyo ni bora awe na amani tu aniruhusu.
na kuna siku kabisa inatokea tupo wote, yeye anatamani kwenda disco but miimi sijisikii kabisa. au yeye ana rafiki zake wamepanga kwenda disco halafu nianze kuambatana naye, hasa kama wenzie hawapo na wake zao.
ni sawa tumeoana, lakini kila mtu ni mmoja (wanatuambiaga tu kuwa tumekuwa mwili mmoja, lol!), kila mtu anaweza fanya lolote popote, la maana ni kujitambua, na hasa kujiheshimu...... yaani nikiwazaga kufanya upuuzi, jambo linalonijia kichwani kwanza wala siyo mume wangu, ni mimi mwenyewe.... hivi sioni aibu kufanya hayo? yaani aibu ikinijia tu akili inarudi, ingawa najua kabisa uwezekano wa kukutwa hapo haupo.
 
Kama kuna kitu unataka kuthibitisha ..unaweza weka huo udhibiti ili ujiridhishe
Ila kama ni hisia mbaya tu..inaweza pelekea mwenzi wako kujishrukia zaidi..
Na hata kile unachokipigania unaweza usikipate..

 
Nilikuelewa kabisa, na lile halikua applicable wala si maelezo ya kua wanao kaa mbali na familia wanakosea. Nilikua nagusia vitu kama hivyo ni moja ya sababu huwakwamisha baadhi.
nilikuelewa pia.....
nilikuwa natoa changamoto tu kwa wadogo zangu ambao watapatwa na vishawishi vya kuogopa kujiendeleza sababu ya familia....
Pamoja sana!
 

kidude cha like mie kwangu sikioni jamani, hizi hofu za kuwalinda hawa wanaume zinatupeleka mbali sana!
 
Ninachojiuliza hapa ni kuwa ..je,wakti unaweka huo udhibiti wa kulinda ,ali yako na yeye mlengwa anakuwa anajua kuwa hiki alichonifanyia mwenzi wangu ni kwa kuwa ananipenda?..au kaniona ni 'easy go' nisiyeweza kujisimamia..kuna uzuri wa mkubwa sana wa kuhakikisha mali yako inabaki kuwa ya kwako..Tatizo linaweza kuwa njia unazotumia 'kudhibiti' hiyo mali ibakie kuwa ya kwako..je, zinawaweka karibu au zinaacha maswali mengi kuliko majibu..Fikiria unamzuia mkeo kwenda hata kwenye vikao vya kina mama kisa atakutana na 'mishangingi' ya mjini..

 

baada ya kumbania akalegeza kidogo, alivyopumzika kufanya ule ufirauni wake, akaanza kuniletea za "ubaba ubaba" kwamba hakuna kwenda huko, mbona mitoko imekuwa mingi, nilimwambia weee hii mitoko ndio iliniliwaza kipindi cha masika, sasa hivi yupo level, nikimwambia leo nikitoka job ntaenda mahali fulani kupiga moja atakuambia poa, na mie napiga sijui wapi huku, basi siku zinaenda maisha yanasonga.
 
kidude cha like mie kwangu sikioni jamani, hizi hofu za kuwalinda hawa wanaume zinatupeleka mbali sana!
ha haaa, pole...
reflesh page kitakuja.
kuna dadangu mpaka leo anajuta kupoteza nafasi ya masomo sababu ya mume (siyo watoto)....
mume kamuacha na walikuwa wanabanana kila wanakoenda...... anabaki kunishangaa tu.......
 
sidhani kama utataka hicho kwenye RED kitokee...
niliwahi soma hapa kuwa kuna watu wana simu zinakaa ofisini tu, hiyo namba wenzi wao hawaijui, ni special kwa ajili ya kuchakachulia mahusiano....

hakuna mwanadamu anayependa au anayetaka kitu kinachomuumiza kitokee............kumbuka ule usemi "if you dont know ,it doesnt exist",,,,,,,,,,,,,, na kwa dhana ile ile ya kumuacha mtu free kwa kusema binadamu hachungiki , lakini hapo ameenda extra mile kwa kuyaacha hayo mawasiliano ya hovyo hovyo huko nje ya nyumba na akifika nyumba ni mimi na yeye na siyo mawasiliano na mtu mwingine na zaidi kwasababu kuna tahadhari basi , she/he cant bring the shits at the door steps............ at least ndani ya nyumba amani inakuwepo.
 
Ninachojiuliza hapa ni kuwa ..je,wakti unaweka huo udhibiti wa kulinda ,ali yako na yeye mlengwa anakuwa anajua kuwa hiki alichonifanyia mwenzi wangu ni kwa kuwa ananipenda?..a

ha haaaaa, kama unanipenda, utanilinda..... siyo kunidhibiti, lol!
 
wow!
hiki ndo unataka?
I thought unataka kwa kumdhibiti basi aachane na wasiliano yasiyofaa, kumbe ruksa kuyafanyia nje ya nyumba?
 

mie nadhani wote ni wanawake, alale na nduguyo, nduguye, housegirl etc kwa upande wangu wote itaniuma sana, mana nilitoka huko hakuwa ndugu ila niliumia sanaa, hata kwa ndugu yake unadhani hiyo fedheha ya familia yake haitakuumiza, maneno ya familia yake, unadhani hawatasema/hawatakusema? zamani nilikuwa nikisafiri napeleka watoto na dada kwa dada yangu, kwasasa nawaacha hapo jinsi walivyo, dada aandae kila kitu cha ndani, aweke panapostaili, msukuma abebe funguo zote kuanzia za room kwetu mpaka getini/milangoni, akichelewa afanye yake bila kusumbua wengine, kitanda changu afanyie usafi yeye mpaka nitakaporudi, wakafanya yao "nisigundue tu" dada ni mtu mzima kwangu, nilishamuita kama dada nikaongea nae kiutu uzima, nadhani wote walinielewa, wakiamua wameamua kunifanyia, sitataka tena kuteseka kwa kuhofia "kitaliwa" kisipoliwa ndani "kitalia hata huko nje" nahitaji heshima/adabu yake nyumbani kwangu, akishindwa hilo nadhani nitafikia tamati, kama anahisi ni lazima kufanya basi akafute hukoooo sio kwa kiumbe chochote kilichopo ndani ya nyumba yangu, nina amani kwasasa.
 

katika watu walisumbukaga basi ni mimi, yaani wakati ule ningeendelea na ile tabia ningechizika, simu yake ikiita roho ilikuwa inanipaa, vidole vinawasha kusoma msg, na nilikuwa nazikuta, hahaha nikikuta msg ninayoihisi na save no kwangu, lol phonebook yangu ilijaa kuliko ya mtuhumiwa, siku nilivyoenda kuleta vagi, ndio siku nilikuwa nikafutilia mbali ma namba yote, sasa hivi hata akisahau simu itaitaaa mpaka akome, hata nikiona ni no ya landline ya ofisini kwake, sipokei apige kwangu aniambie nimpitishie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…