Hili la wanaume kua na mzigo wanaoubeba kwenye familia na ukoo kusaidia watoto, ndugu, jamaa na marafiki sio kwamba halipo ila nitakuja kulielezea ni jinsi gani wanaume wana msongo wa mawazo ila wanaweza kuishi na kukabiriana na huo msongo wa mawazo tofauti na jinsi ilivyo kwa wanawake walio wengi. Ingiwa unapozungumzia mzigo lazima uangalie pande zote mbili yaan wanaume na wanawake kila mmoja ana nafasi yake kwa namna yake.
Nikituulia nitakuja kueleza kwanini wanaume wanaishi na msongo wa mawazo ila hawaonyeshi km wana msongo wa mawazo na huwezi jua km ana msongo wa mawazo tofauti na ilivyo kwa mwanamke. Mwanamke akiwa na msongo wa mawazo utajua na lazima atakuonyesha aidha kwa maneno, kwa vitendo au kwa ishara.