Kumekucha: Baraza la Mawaziri kivuli - Mbatia out

Kuliko kuwa na bunge la "opposition" NCCR, bora kujipanga tuanze upya 2025, Magufuli atapita, upinzani halisi utarejea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna uhakika wa 100% wa uwepo wa uchaguzi Octoba 2020 kama hali ya maambukizi ya CORONA itazidi
 
Pascal,umetoa point nzuri na pia tuangalie upande mwingine mpaka hili linafanyika yawezekana hao mawaziri vivuli wa vyama vingine kwa uzembe,au kwa maelekezo hawajaandaa budget mbadala.je ungekuwa wewe ndio KUB ungefanyaje ?
 

Mbowe anaendeshwa na mihemko, hisia na wapambe.

CDM inaporomoka, bado wanamsifia

nyakati zaja ambazo atakuwa 'joker'
 
Na huu ndio ukweli mchungu ambao huwez kuta unajadiliwa kwa uwazi na chombo chochote cha habar hapa bongo.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu upuuzi wa pasco eti 'managing diversity', juzi ccm wamemtimua Membe na kuwakaripia wazee sikuona Uzi wa pasco kuishauri ccm management of diversity

Mkuu P unachemka
Mkuu Mliberali, tunaweza kujadiliana kwa hoja bila kutukanana.
Hili somo la managing Diversity sikulianza leo.
Kwa Membe nimelisema
Membe, Japo Umeonewa, Usifanye Kosa la Lowassa!, Ila CCM ya Ajabu!, Uamuzi based on Illegal Evidence ni Void Ab Initial!. - JamiiForums

Na kabla ya hapo pia nimelisema
Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako linahitajika - JamiiForums
P
 
Pascal,umetoa point nzuri na pia tuangalie upande mwingine mpaka hili linafanyika yawezekana hao mawaziri vivuli wa vyama vingine kwa uzembe,au kwa maelekezo hawajaandaa budget mbadala.je ungekuwa wewe ndio KUB ungefanyaje ?
Wewe ni baba, hao ni watoto wako, wakikuny.a mkono hauukati, unausafisha na kuendelea kumbeba mtoto, kama hawaja andaa unawaandalia na sio kuwatumbua.
P
 

Twende taratibu ili unapotoa ushauri usitoe ili ionekane umetoa ushauri, huku ushauri wako ukiwa unafumbia macho ukweli. NCCR ni sehemu ya Ukawa, na sasa bunge linaenda kufikia mwisho. Common enemy wa Ukawa ni ccm. Iweje Mbatia akutane na Magufuli, halafu ndani ya masaa 24 aanze kupewa favour ambazo hakupewa huko nyuma na serekali, kisha sehemu ya siasa zake aanze na madiwani waliotoka cdm? Ngoja nikupe mfano mzuri, ww na jirani yako mnadai shamba, kimsingi hilo shamba kila mtu anaweza kulipata kivyake, lakini mazingira yanaonyesha mnaweza kulipata kirahisi iwapo mtalidai mkiwa pamoja. Wakati mkiendelea kulidai shamba, ghafla unaona jirani yako anakutana na mnayemdai shamba, halafu huyo jirani yako baada vya kukaa na huyo adui anakuchukulia mkeo! Katika mazingira hayo unamfumbia macho huyo jirani yake ili iweje?

Hivi Paskali unaposema selfishness unamaanisha nini? Maana cdm kama cdm wamelazimishwa kuchukua hatua baada ya kuona hakuna umoja tena. Kuna umoja gani katika mazingira hayo kama sio wendawazimu? Unataka hao walioondoka cdm, au cdm iachie wagombea wanaokubalika wa wapinzani wengine, je hilo lifanyike kwa makubaliano gani na kipimo gani? Halafu sikuelewi unaopoonyesha kuwa wapinzani wasipoungana basi mfaidika ni ccm. Ccm hii ambayo tunaona mabox ya kura yakitolewa vituoni kwenda kujazwa kura za ccm, kwa uratibu wa vyombo vya dola? Paskali nadhani ni vyema tukadai tume huru ya uchaguzi, then baada vya hapo kila mtu ashinde mechi zake.
 

Kipi kilifanya Nape au January wapoteze uwaziri kama utetezi wako ndio huo?
 
Halafu anashangiliwa..
 
Wewe ni baba, hao ni watoto wako, wakikuny.a mkono hauukati, unausafisha na kuendelea kumbeba mtoto, kama hawaja andaa unawaandalia na sio kuwatumbua.
P

Mkuu umetoa jukumu, mtu hajalitekeleza, na unaona kabisa mwenendo wake una walakini, hapo unamuacha na hilo jukumu ili iweje? Paskali ni kwamba kuna mahali unaenda, hivyo unachangia tu ili uwahi huko uendako? Ni kwanini usiende kisha ukirudi ndio uchangie?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…