Kumekucha: Baraza la Mawaziri kivuli - Mbatia out

Kumekucha: Baraza la Mawaziri kivuli - Mbatia out

Wafuta miguu wa mwenyekiti unasikia misemo yao eti yupo SMART.

Alafu kesho watakuja kusifu uSMART wa mandela.



Roho ya visasi imewajaa si Ccm si Chadema hata wapiga kura ndo mana wana shindwa wamuamini nani.


#Bravo_mkuu.

Siasa za Tanzania kichekesho sana.
Si upinzani wala CCM ni vituko tupu.

Sasa bunge lenyewe ni la mwisho kabla ya serikali mpya, hao mawaziri vivuli wapya watakao ziba nafasi hizi watafanya nini?
Na wa zamani waliotemwa wangekuwa na athari gani?

Kuna wakati unatakiwa kuwaacha watu kama hao na kutumia nafsi hiyo kujiimarisha kisiasa kwa kujisifu majukwaani hawa walitutendea ubaya huu lakini kwa vile sisi wakomavu wa kisiasa na sio watu wa visasi tumewaacha kwenye nafasi hizi ingiwa sababu na uwezo wa kuwatosa kama kisasi tulikuwa nao.

Mambo madogo kama haya ya uvumilivu ndiyo yana kuwezesha kuvuna pointi muhimu kwenye siasa, hasa kwenye masanduku ya kura.
You can act like you live what you preach.

Wapiga kura ni watu wa ajabu sana, wanaweza kukupa kura sababu umewataja kwa majina angalau watu wawili tu wa kawaida wa eneo lao, au umewapa msamaha watu waliokutendea ubaya.

Huenda sipo sahihi kabisa katika hili, ngoja niamini KUB yupo sahihi.
 
Hapana, hii ni political message. Hii ni siasa, alichofanya KUB ni sahihi kabisa.

Pia. Kubwa zaidi, amemnyima Mbatia nafasi ya kutumia platform ya upinzani wakati wa kusoma hotuba mbadala ya upinzani katika bajeti hii ya mwisho. Angeitumia kuwafurahisha CCM kwa kufanya kazi waliyomtuma, kwa gharama za upinzani. Hotuba yake ingeshangiliwa sana na kusemwa ndio ya kuigwa na wapinzani. Mbowe sio zuzu kiasi hicho.
 
Hapo wamecheza mcheza nne wa hatari zaidi kwa upande wao,wametoa nafasi nzuri kwa CCM kuendelea kushinda,maana Chedema wakigomea chochote CUF,NCCRA,TLP watakubali.
Wapinzania sijui kuna pepo gani linawaandama.
 
Hapa hata magufuli kawapiga bao. Maana kwenye nafasi za uongozi anao hadi waliokuwa upinzani na kugombea uraus kama kina anna mghwira.
Mbowe ye ukitofautiana nae tu ujue out. Hana uvumilivu wa kisiasa. Acha Magufuli awanyooshe tu maana wao wangeshika dola wangenyanyasa sana watesi wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao alowachukua Magufuli siyo wapinzani, bali ni wachumba tumbo. Wanapiga kulingana na matakwa ya anayewadhamini au kuwalipa. Lakini moyoni hawana sera zaidi ya tumbo.

Eehee! Kwaiyo Magufuli ana uvumilivu wa kisiasa? wangapi wametimuliwa kwa kutoa ushauri kinyume na matakwa yake?

Anawavumilia wapinzani ambao wapo kisheria? Hata kukutana nao tu hataki
 
Duh...!. Ndondi ni ulingoni, kipimo cha bondia mwenye nguvu ni kwa makonde anayorusha. Kwenye serikali za mitaani, bondia wa upande wa pili hakupanda ulingoni hivyo bondia wetu kupata ushindi wa mezani wa kishindo cha asilimia 99 9%.
2020 watu tunataka kuona mpambano.
Mabondia wapande ulingoni, mimi mwenyewe naingia ulingoni
Kama ni mechi, ni uwanjani sio mtu anaweka mpira kwapani halafu anaanza kupiga kelele za faulo
P
Hata kama ungelikuwa wewe bondia ungeingia ulingoni kupigana wakati referee kakushikilia ili mpinzani wako akupige vizuri ?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom