Kumekucha bomoabomoa Ubungo-Kimara ndani ya 90m za hifadi ya barabara

Magufuli asingeruhusu upuuzi wa aina hii, watu walikuwa wanaogopa kupeleka proposal za kipumbavu maana angezipiga chini tu😅!

Watamkumbuka sana tu maana sahizi wapigaji hawatakuwa wanawajibishwa zaidi ya kuandikishwa barua tu
Ninacho shangaa wanadai kupeleka umeme vijijini yaan mawazo ya mwigulu anadhan watanzania bado wajinga miaka yote tunachangia REA sasa hiki walicho leta cha kazi gani
 
Ninacho shangaa wanadai kupeleka umeme vijijini yaan mawazo ya mwigulu anadhan watanzania bado wajinga miaka yote tunachangia REA sasa hiki walicho leta cha kazi gani
Maji tyr kwani?

Sola zinatosha kijijini Nani anatumia friji?
 
Hawapewi hata mia maana inasemekana huko nyuma walishapewa wengine wakajauzia hao waliopo sa hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa yetu alishawahi kutuambia alilipwa mara ya kwanza lakini hakuhama aliendelea kuishi hapo tena, baadhi ya majirani walihama na kuuza maeneo yao kwa watu wengine. Ukapita muda mrefu ikaja tathimini nyingine wakalipwa tena baadhi ya majirani wakauza tena maeneo yao. Asilimia kubwa ya watu waliokuwa wanaishi maeneo hayo kabla ya bomoa bomoa ni wale waliouziwa yale maeneo kutoka kwa watu ambao waliokwisha kulipwa.
 
Hilo wengi hawajui kama wale wazee wa mwanzo washakulaga hela

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini mnakimbilia kusema wanataka kumgombanisha na Raisi? Yeye so aingilie kato? Na kama unakumbuka wote humu tulikuwa tunamsifu kwa kuunda timu yake, kama hao watendaji hawamheshimu huo uraisi atauweza vipi tena?
 
Wakati mwingine watanzania hatufuati taratibu, kuna wakati fulani nilienda Tabata nikakuta watu wengi wamejenga nyumba juu ya bomba kubwa la maji. Bomoa bomoa ikipita watu hao watakuwa wa kwanza kulalamika na wanasiasa watatumia hiyo fursa.
 
Nimegundua humu watu huwa hawasomi habari bali wanachangia tuuu.... ukisoma hiyo barua utagundua hakuna ubomoaji mpya bali ni ule ule na mita ni zile zile 90 kwa sababu toka ya enzi za JPM WALISHABOMOLEWA labda kama walirudi kwenye hifadhi ya barabara tena..... kimsingi waliobomolewa kipindi kile ndio hao hao wanaambiwa tena kwenye hii barua kuwa kama walirudi wajua wenye eneo wanataka kulitumia.
 
Gwajima anaondoka
 
hawa walishabomolewa na alama za x ziliwekwa kama walirudi ni kosa lao maana tanroads waliwawekea x toka mwaka 2017
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…