GE2025 Kumekucha, Leo Ndio Leo, Ndio Ile Siku Tuliyo Isubiria Sana, Japo Wako 17, Ni CCM, Ni Samia! Huu Ndio Ukweli Wenyewe!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi

Hauchi, hauchi, hatimaye kumekucha, leo ndio leo, ile siku ya siku tuliyoisubiri sana kwa miaka 5.
Ninachokifanya hapa ni kuwapatia tena jf, ile the jf advantage of being the first to know, kuwa japo kuna wagombea 17 wa urais, ukweli wa mambo, mgombea ni mmoja na chama ni kimoja, ni CCM, ni Samia!.

Kuna vitu vinafanyika, watu wanaujua ukweli wa mambo lakini wanaogopa kuusema ukweli bayana kwa kuhofia kuwaudhi wale ambao hawatapendezwa na ukweli huo.

Mimi siku zote ni mkweli daima, na ukiwa mkweli sana, katika jamii inayopenda hadaa, unakuja kuonekana wewe ndio adui, na kuna wakati ukweli usiowapendeza wengine, unaweza kukugharimu, kama kinachowakuta baadhi ya watu mnaosikia wana tekwa au kupotezwa, ila mimi ni muumini wa ukweli, na ni ukweli ndio utatuweka huru.

Sasa katika ukweli wa uchaguzi mkuu wetu huu wa leo, kwa sisi wasomaji wa mielekeo ya kisiasa, (political trends) ya siasa za Tanzania, kwenye urais, japo kuna wagombea urais kutoka vyama 17, lakini ukweli wa mambo, huu ni uchaguzi wa CCM na CCM only, na utathibitishwa na matokeo, ni CCM, ni Samia!, hivyo wewe kama mwana jf, ndio wa kwanza kujua.

Kwa kawaida mimi kama mwandishi wa habari, kwa Tanzania, sikutakiwa kusema ukweli huu kuwa uchaguzi mkuu wetu ni CCM pekee, na ni Samia tuu, kwasababu kwenye msingi wa maadili ya uandishi wa habari kwenye uchaguzi, chombo cha habari hakitakiwi kuegemea upande wowote, Ila mimi kama mwandishi wa makala, ninaruhusiwa na maadili kuweka maoni yangu, tena vyombo vya habari vya nchi za wenzetu zilizoendelea, vinaruhusiwa kuchukua mrengo na kuunga mkono chama fulani au mgombea fulani ila vinachotakiwa kufanya ni kutangaza wazi maslahi, kwa kufanya kitu kinachoitwa media endorsements, kuwa chombo chetu cha habari kinaunga mkono chama fulani au mgombea fulani.

Tanzania japo hatuna media endorsements, ila ukweli unajulikana, kuna vyombo vya habari vinajulikana kabisa vinaegemea wapi.

Vyombo vya Habari vya umma, yaani public broadcasting stations, ndivyo havitakiwi kuegemea upande wowote, ila chama chenye nguvu na ukwasi wa kutosha kinalipia matangazo, hivyo kinatangazwa zaidi kuliko vyama vingine vyote au vyama makapuku!.

Nimesema uchaguzi mkuu wa leo wa rais wabunge na madiwani, ni uchaguzi wa CCM na CCM pekee, na mshindi ni CCM na Samia, kwasababu CCM inaingia dimbani ikiwa na mtaji wa utekelezaji wa ilani yake iliyopita, hivyo ina kitu cha kuonyesha, inaingia kushindana na vyama 16 ambayo havina chochote cha kuonyesha.

Siku za nyuma niliandika makala humu kuhusu katiba ya JMT ya mwaka 1977, ni katiba ya mfumo wa chama kimoja, hivyo uwanja wetu wa uchaguzi ni uwanja tenge, umeegemea upande mmoja wa chama tawala, na chama hicho ni CCM.

CCM inaingia kwenye uchaguzi kikiwa ni chama cha siasa kwa upande mmoja na ni chama dola kwa upande mwingine, hivyo chama dola kinaingia dimbani kushindana na vyama makapuku, unategemea nini?.

Niliwahi kusema uchaguzi mkuu wetu ni mashindano ya kugombea kisu cha makali kuwili, huku mgombea mmoja ameshika kwenye mpini anavutana na wagombea wanaoshika kwenye makali kuwili.

Niliandika makala kuipongeza Tume Huru ya Uchaguzi INEC kwa angalau kusawazisha kidogo uwanja tenge kwa wagombea wote 17 wa urais kwa kuwapatia magari, dereva na ulinzi, bila kuwapatia mafuta, wala waandishi wa habari wa kuandamana nao.

Hawa wagombea makapuku 16, wanashindana na mgombea mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa Chama tawala na wakati huo huo ni rais wa JMT aliyepo madarakani na ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi, anagombea huku ana nyota mabegani mwake.

Nimehesabu magari msafara wa mgombea Urais wa CCM Mwanza jana, wakati wa kuhitimisha kampeni za CCM, pale uwanja wa CCM Kirumba, ni magari zaidi ya 200!, huku yanaingurumishwa AC wakati wote wa kampeni!, baadhi ya magari hayo tunayajua yalikuwa ST, sasa ni namba za kiraia, nani atashindana?.

Niliandika humu kuhusu kwanini CCM inashinda, licha ya kushinda kwa makubwa mazuri na mema inayoyatekeleza, CCM pia inashinda kwa kukosekana upinzani imara, upinzani uliopo Tanzania ni upinzani legelege usio na uwezo wa kushindana na CCM.

Nikashauri, CCM na serikali yake ina wajibu wa kuulea upinzani ili tupate upinzani imara utaolifanya Bunge letu liweze kuisimamia serikali kikamilifu.

Bila upinzani makini na upinzani imara, CCM itabweteka, Bunge letu litaendelea kuwa Bunge butu na Bunge kibogoyo lisilo na meno.

Nimalizie kwa kuipongeza CCM na kumpongeza Rais, kwa ushindi wa kishindo, ila namuomba kwenye zile nafasi zake 10 za uteuzi wa wabunge, angalau atuteulie japo wapinzani 4, akiwemo yule mwanae wa Kigoma, kwenda kutuchangamshia like Bunge letu pale Dodoma.

Hongera CCM
Hongera Rais Samia
Hongera Watanzania Wote.
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Nikijiandaa kwenda kituoni kwangu kupiga kura

Update
Nimepiga kura yangu salama, katika kituo changu, sasa nimerudi home kusubiria matokeo.
P
 
Wanabodi

Hauchi, hauchi, hatimaye kumekucha, leo ndio leo, ile siku ya siku tuliyoisubiri sana kwa miaka 5.
Ninachokifanya hapa ni kuwapatia tena jf, ile the jf advantage of being the first to know, kuwa japo kuna wagombea 17 wa urais, ukweli wa mambo, mgombea ni mmoja na chama ni kimoja, ni CCM, ni Samia!.

Kuna vitu vinafanyika, watu wanaujua ukweli wa mambo lakini wanaogopa kuusema ukweli bayana kwa kuhofia kuwaudhi wale ambao hawatapendezwa na ukweli huo.

Mimi siku zote ni mkweli daima, na ukiwa mkweli sana, katika jamii inayopenda hadaa, unakuja kuonekana wewe ndio adui, na kuna wakati ukweli usiowapendeza wengine, unaweza kukugharimu, kama kinachowakuta baadhi ya watu mnaosikia wana tekwa au kupotezwa, ila mimi ni muumini wa ukweli, na ni ukweli ndio utatuweka huru.

Sasa katika ukweli wa uchaguzi mkuu wetu huu wa leo, kwa sisi wasomaji wa mielekeo ya kisiasa, (political trends) ya siasa za Tanzania, kwenye urais, japo kuna wagombea urais kutoka vyama 17, lakini ukweli wa mambo, huu ni uchaguzi wa CCM na CCM only, na utathibitishwa na matokeo, ni CCM, ni Samia!, hivyo wewe kama mwana jf, ndio wa kwanza kujua.

Kwa kawaida mimi kama mwandishi wa habari, kwa Tanzania, sikutakiwa kusema ukweli huu kuwa uchaguzi mkuu wetu ni CCM pekee, na ni Samia tuu, kwasababu kwenye msingi wa maadili ya uandishi wa habari kwenye uchaguzi, chombo cha habari hakitakiwi kuegemea upande wowote, Ila mimi kama mwandishi wa makala, ninaruhusiwa na maadili kuweka maoni yangu, tena vyombo vya habari vya nchi za wenzetu zilizoendelea, vinaruhusiwa kuchukua mrengo na kuunga mkono chama fulani au mgombea fulani ila vinachotakiwa kufanya ni kutangaza wazi maslahi, kwa kufanya kitu kinachoitwa media endorsements, kuwa chombo chetu cha habari kinaunga mkono chama fulani au mgombea fulani.

Tanzania japo hatuna media endorsements, ila ukweli unajulikana, kuna vyombo vya habari vinajulikana kabisa vinaegemea wapi.

Vyombo vya Habari vya umma, yaani public broadcasting stations, ndivyo havitakiwi kuegemea upande wowote, ila chama chenye nguvu na ukwasi wa kutosha kinalipia matangazo, hivyo kinatangazwa zaidi kuliko vyama vingine vyote au vyama makapuku!.

Nimesema uchaguzi mkuu wa leo wa rais wabunge na madiwani, ni uchaguzi wa CCM na CCM pekee, na mshindi ni CCM na Samia, kwasababu CCM inaingia dimbani ikiwa na mtaji wa utekelezaji wa ilani yake iliyopita, hivyo ina kitu cha kuonyesha, inaingia kushindana na vyama 16 ambayo havina chochote cha kuonyesha.

Siku za nyuma niliandika makala humu kuhusu katiba ya JMT ya mwaka 1977, ni katiba ya mfumo wa chama kimoja, hivyo uwanja wetu wa uchaguzi ni uwanja tenge, umeegemea upande mmoja wa chama tawala, na chama hicho ni CCM.

CCM inaingia kwenye uchaguzi kikiwa ni chama cha siasa kwa upande mmoja na ni chama dola kwa upande mwingine, hivyo chama dola kinaingia dimbani kushindana na vyama makapuku, unategemea nini?.

Niliwahi kusema uchaguzi mkuu wetu ni mashindano ya kugombea kisu cha makali kuwili, huku mgombea mmoja ameshika kwenye mpini anavutana na wagombea wanaoshika kwenye makali kuwili.

Niliandika makala kuipongeza Tume Huru ya Uchaguzi INEC kwa angalau kusawazisha kidogo uwanja tenge kwa wagombea wote 17 wa urais kwa kuwapatia magari, dereva na ulinzi, bila kuwapatia mafuta, wala waandishi wa habari wa kuandamana nao.

Hawa wagombea makapuku 16, wanashindana na mgombea mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa Chama tawala na wakati huo huo ni rais wa JMT aliyepo madarakani na ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi, anagombea huku ana nyota mabegani mwake.

nimehesabu magari msafara wa mgombea Urais wa CCM Mwanza jana, wakati wa kuhitimisha kampeni za CCM, uwanja wa CCM Kirumba, ni magazine zaidi ya 200!.
Niliandika humu kuhusu kwanini CCM inashinda, licha ya kushinda kwa makubwa mazuri na mema inayoyatekeleza, CCM pia inashinda kwa kukosekana upinzani imara, upinzani uliopo Tanzania ni upinzani legelege usio na uwezo wa kushindana na CCM.
Nikashauri, CCM na serikali yake ina wajibu wa kuulea upinzani ili tupate upinzani imara utaolifanya Bunge letu liweze kuisimamia serikali kikamilifu. Bila upinzani makini na upinzani imara, CCM itabweteka, Bunge letu litaendelea kuwa Bunge butu na Bunge kibogoyo lisilo na meno.
Nimalizie kwa kuipongeza CCM na kumpongeza Rais, kwa ushindi wa kishindo, ila namuomba kwenye zile nafasi zake 10 za uteuzi wa wabunge, atuteulie japo wapinzani 4, akiwemo yule mwanae wa Kigoma, kwenda kutuchangamshia Bunge letu.
Hongera CCM
Hongera Samia
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Du mzee hukomi uchawa! Tafuteni kazi ya kuwaingizia riziki hata kama mmeishastaafu badala ya kutudhalilisha wazee wenzenu. Hivi, kwa muda wote uliofanya kazi hukuweka akiba au kupata kiinua mgongo? Mtaramba matako hadi lini mwanangu Pasko? Umesomea nini wewe ambaye unaunga mkono uchafu na uchawa. Eti hupaswi kuonyesha upande wakati umeuonyesha tena kibwege! Eti unasema CCM imekeleza sera zake zipi? Eti CCM inashindana na vyama 17 wakati vyote ni matawi yake. Hata kama unakimbizia uteuzi, tumia lau akili japo kidogo. Shame on you. Sitaki hata hiyo like yako ya kujionyesha kuwa unatukanwa kwa ajili ya haya majizi yanayowafunga nyinyi machawa. Ni unafiki kiasi gani kuniwekea dole wakati moyoni unaungua na kuugua?
 
Wanabodi

Hauchi, hauchi, hatimaye kumekucha, leo ndio leo, ile siku ya siku tuliyoisubiri sana kwa miaka 5.
Ninachokifanya hapa ni kuwapatia tena jf, ile the jf advantage of being the first to know, kuwa japo kuna wagombea 17 wa urais, ukweli wa mambo, mgombea ni mmoja na chama ni kimoja, ni CCM, ni Samia!.

Kuna vitu vinafanyika, watu wanaujua ukweli wa mambo lakini wanaogopa kuusema ukweli bayana kwa kuhofia kuwaudhi wale ambao hawatapendezwa na ukweli huo.

Mimi siku zote ni mkweli daima, na ukiwa mkweli sana, katika jamii inayopenda hadaa, unakuja kuonekana wewe ndio adui, na kuna wakati ukweli usiowapendeza wengine, unaweza kukugharimu, kama kinachowakuta baadhi ya watu mnaosikia wana tekwa au kupotezwa, ila mimi ni muumini wa ukweli, na ni ukweli ndio utatuweka huru.

Sasa katika ukweli wa uchaguzi mkuu wetu huu wa leo, kwa sisi wasomaji wa mielekeo ya kisiasa, (political trends) ya siasa za Tanzania, kwenye urais, japo kuna wagombea urais kutoka vyama 17, lakini ukweli wa mambo, huu ni uchaguzi wa CCM na CCM only, na utathibitishwa na matokeo, ni CCM, ni Samia!, hivyo wewe kama mwana jf, ndio wa kwanza kujua.

Kwa kawaida mimi kama mwandishi wa habari, kwa Tanzania, sikutakiwa kusema ukweli huu kuwa uchaguzi mkuu wetu ni CCM pekee, na ni Samia tuu, kwasababu kwenye msingi wa maadili ya uandishi wa habari kwenye uchaguzi, chombo cha habari hakitakiwi kuegemea upande wowote, Ila mimi kama mwandishi wa makala, ninaruhusiwa na maadili kuweka maoni yangu, tena vyombo vya habari vya nchi za wenzetu zilizoendelea, vinaruhusiwa kuchukua mrengo na kuunga mkono chama fulani au mgombea fulani ila vinachotakiwa kufanya ni kutangaza wazi maslahi, kwa kufanya kitu kinachoitwa media endorsements, kuwa chombo chetu cha habari kinaunga mkono chama fulani au mgombea fulani.

Tanzania japo hatuna media endorsements, ila ukweli unajulikana, kuna vyombo vya habari vinajulikana kabisa vinaegemea wapi.

Vyombo vya Habari vya umma, yaani public broadcasting stations, ndivyo havitakiwi kuegemea upande wowote, ila chama chenye nguvu na ukwasi wa kutosha kinalipia matangazo, hivyo kinatangazwa zaidi kuliko vyama vingine vyote au vyama makapuku!.

Nimesema uchaguzi mkuu wa leo wa rais wabunge na madiwani, ni uchaguzi wa CCM na CCM pekee, na mshindi ni CCM na Samia, kwasababu CCM inaingia dimbani ikiwa na mtaji wa utekelezaji wa ilani yake iliyopita, hivyo ina kitu cha kuonyesha, inaingia kushindana na vyama 16 ambayo havina chochote cha kuonyesha.

Siku za nyuma niliandika makala humu kuhusu katiba ya JMT ya mwaka 1977, ni katiba ya mfumo wa chama kimoja, hivyo uwanja wetu wa uchaguzi ni uwanja tenge, umeegemea upande mmoja wa chama tawala, na chama hicho ni CCM.

CCM inaingia kwenye uchaguzi kikiwa ni chama cha siasa kwa upande mmoja na ni chama dola kwa upande mwingine, hivyo chama dola kinaingia dimbani kushindana na vyama makapuku, unategemea nini?.

Niliwahi kusema uchaguzi mkuu wetu ni mashindano ya kugombea kisu cha makali kuwili, huku mgombea mmoja ameshika kwenye mpini anavutana na wagombea wanaoshika kwenye makali kuwili.

Niliandika makala kuipongeza Tume Huru ya Uchaguzi INEC kwa angalau kusawazisha kidogo uwanja tenge kwa wagombea wote 17 wa urais kwa kuwapatia magari, dereva na ulinzi, bila kuwapatia mafuta, wala waandishi wa habari wa kuandamana nao.

Hawa wagombea makapuku 16, wanashindana na mgombea mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa Chama tawala na wakati huo huo ni rais wa JMT aliyepo madarakani na ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi, anagombea huku ana nyota mabegani mwake.

nimehesabu magari msafara wa mgombea Urais wa CCM Mwanza jana, wakati wa kuhitimisha kampeni za CCM, uwanja wa CCM Kirumba, ni magazine zaidi ya 200!.
Niliandika humu kuhusu kwanini CCM inashinda, licha ya kushinda kwa makubwa mazuri na mema inayoyatekeleza, CCM pia inashinda kwa kukosekana upinzani imara, upinzani uliopo Tanzania ni upinzani legelege usio na uwezo wa kushindana na CCM.
Nikashauri, CCM na serikali yake ina wajibu wa kuulea upinzani ili tupate upinzani imara utaolifanya Bunge letu liweze kuisimamia serikali kikamilifu. Bila upinzani makini na upinzani imara, CCM itabweteka, Bunge letu litaendelea kuwa Bunge butu na Bunge kibogoyo lisilo na meno.
Nimalizie kwa kuipongeza CCM na kumpongeza Rais, kwa ushindi wa kishindo, ila namuomba kwenye zile nafasi zake 10 za uteuzi wa wabunge, atuteulie japo wapinzani 4, akiwemo yule mwanae wa Kigoma, kwenda kutuchangamshia Bunge letu.
Hongera CCM
Hongera Samia
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Uchaguzi upi? Wapi?
Tanzania hakuna uchaguzi maana wapinzani wa kweli Tundu lisu na John Heche wapo Jela, Dunia nzima wanajua Tanzania hakuna Uchaguzi bali kuna maigizo ya uchaguzi kuchezea pesa za walipa kodi tu
 
Tanzania hakuna uchaguzi bali ccm wamechezea pesa za walipa kodi kuzunguka Nchi nzima wakati wana kura mifukoni mwao watajitangazia ushindi Haramu usio na Baraka za wapiga kura
Kuanzia leo, tusome nyuzi za chawa Pasko na kutochangia. Tukimtolea uvivu kumbe tunampa chati kwa mabwana zake wanaoona kama anateseka kwa ajili yao. Ni ushauri tu.
 
Mimi nakwenda kutiki. Hawa ma key board warriors wa maandamano hawana lolote.

Sijui MangeKimambi, Maria Sarungi, Roma Mkatoliki na Sativa wanajisikiaje huko.

Hakuna maandamano yanaanza baada ya saa 12 asubuhi
Maandamano tayari yamefanyika kwani week yote Polisiccm wanazunguka zunguka na pia kuyafanyia promotion kwa kutoa vitisho kwa kifupi Polisiccm wameandamana kwa niaba ya wananchi na ujumbe umeifikia Dunia yote, Sasa mandamano makubwa yapo moyoni walioteswa walioumizwa walioonewa waliozuliwa walioporwa haki zao wanaandamana moyoni kwa nguvu kubwa huku wengine wakisindikiza mandamano kwa Alibadiri na visomo vingi pia maombi mengi kumlilia mungu
 
Hapa ni mgombea wa CCM ataibuka mshindi. ushindi wa kihistoria. Samia atapata kura nyingi, naangalia sura za wapiga kura naona wengi watampigia kura , wamevutiwa na kampeni zake
 
Kuanzia leo, tusome nyuzi za chawa Pasko na kutochangia. Tukimtolea uvivu kumbe tunampa chati kwa mabwana zake wanaoona kama anateseka kwa ajili yao. Ni ushauri tu.
Pascal mayala huwa anajua ukweli lakini ni muoga sana anahofia kuunganishwa jela na Lisu na Heche ingawa sasa atajifunza kupitia hizi comment za wachangia mada hapa jukwaani
 
Hapa ni mgombea wa CCM ataibuka mshindi. ushindi wa kihistoria. Samia atapata kura nyingi, naangalia sura za wapiga kura naona wengi watampigia kura , wamevutiwa na kampeni zake
Kwa uchaguzi upi? Wapi?
Kwani Tanzania kuna uchaguzi?
Maigizo ya uchaguzi kura mnazo mfukoni jitangazieni ufalume tu hakukuwa na haja ya kufanya kampeni kupoteza pesa za walipa kodi
 
Back
Top Bottom