GE2025 Kumekucha, Leo Ndio Leo, Ndio Ile Siku Tuliyo Isubiria Sana, Japo Wako 17, Ni CCM, Ni Samia! Huu Ndio Ukweli Wenyewe!

GE2025 Kumekucha, Leo Ndio Leo, Ndio Ile Siku Tuliyo Isubiria Sana, Japo Wako 17, Ni CCM, Ni Samia! Huu Ndio Ukweli Wenyewe!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Nimefuatilia kampeni zote za ccm za uchaguzi huu. Safari hii itashangaza kama watadondosha hata kiti kimoja kwa wagombea wake kwa namna walivyopanga ilani na sera zao. Kampeni zao walizipanga zikapangika, kama wataachia kiti hata kimoja basi ni wao wametaka kupunguza ushindi wao. Uchaguzi utakuwa huru na haki wananchi wajitokeze tu kupiga kura kuchagua viongozi
 
Usijekupata minyoo kweli😎

Cc: Mimi Wewe Yule
Uwezo wako wa kufikiri umefika mwisho kojoa Ulale wewe inaelekea ni mvuta Bangi kwani kipimo cha Ufala hapa JF huwa ni Juha zuzu kama wewe kuisengenya ID ya JF kwani si umeona ID yako ni ya kifala lakini mimi sijaigusa nimekomaa na issue ya uchaguzi tu, ebu acha Upumbavu komaa na mada ingawa njaa zako zimekutoa fahamu zote , Tambua kuwa Tanzania hakuna uchaguzi bali kuna maigizo ya uchaguzi kucheza pesa za walipa kodi
 
Ukiona hivyo jua wewe ni chwa, funza, au kunguni kama siyo mseeenge kkkk.
 
Nimefuatilia kampeni zote za ccm za uchaguzi huu. Safari hii itashangaza kama watadondosha hata kiti kimoja kwa wagombea wake kwa namna walivyopanga ilani na sera zao. Kampeni zao walizipanga zikapangika, kama wataachia kiti hata kimoja basi ni wao wametaka kupunguza ushindi wao. Uchaguzi utakuwa huru na haki wananchi wajitokeze tu kupiga kura kuchagua viongozi
Uchaguzi upi? Wapi? Kampeni gani?
Tanzania hakuna uchaguzi kuna maigizo ya uchaguzi kuchezea pesa za walipa kodi
 
Uwezo wako wa kufikiri umefika mwisho kojoa Ulale wewe inaelekea ni mvuta Bangi kwani kipimo cha Ufala hapa JF huwa ni Juha zuzu kama wewe kuisengenya ID ya JF kwani si umeona ID yako ni ya kifala lakini mimi sijaigusa nimekomaa na issue ya uchaguzi tu, ebu acha Upumbavu komaa na mada ingawa njaa zako zimekutoa fahamu zote , Tambua kuwa Tanzania hakuna uchaguzi bali kuna maigizo ya uchaguzi kucheza pesa za walipa kodi
Dawa inakuingia taratibu, ha ha ha😂

Cc: Mimi Wewe Yule
 
Uchaguzi upo, wananchi wanajitokeza kwa wingi kupiga kura kuchagua viongozi. Ni uchaguzi huru na haki, jitokezeni kushiriki uchaguzi huu wa kihistoria, chagua maendeleo
 
Wanabodi

Hauchi, hauchi, hatimaye kumekucha, leo ndio leo, ile siku ya siku tuliyoisubiri sana kwa miaka 5.
Ninachokifanya hapa ni kuwapatia tena jf, ile the jf advantage of being the first to know, kuwa japo kuna wagombea 17 wa urais, ukweli wa mambo, mgombea ni mmoja na chama ni kimoja, ni CCM, ni Samia!.

Kuna vitu vinafanyika, watu wanaujua ukweli wa mambo lakini wanaogopa kuusema ukweli bayana kwa kuhofia kuwaudhi wale ambao hawatapendezwa na ukweli huo.

Mimi siku zote ni mkweli daima, na ukiwa mkweli sana, katika jamii inayopenda hadaa, unakuja kuonekana wewe ndio adui, na kuna wakati ukweli usiowapendeza wengine, unaweza kukugharimu, kama kinachowakuta baadhi ya watu mnaosikia wana tekwa au kupotezwa, ila mimi ni muumini wa ukweli, na ni ukweli ndio utatuweka huru.

Sasa katika ukweli wa uchaguzi mkuu wetu huu wa leo, kwa sisi wasomaji wa mielekeo ya kisiasa, (political trends) ya siasa za Tanzania, kwenye urais, japo kuna wagombea urais kutoka vyama 17, lakini ukweli wa mambo, huu ni uchaguzi wa CCM na CCM only, na utathibitishwa na matokeo, ni CCM, ni Samia!, hivyo wewe kama mwana jf, ndio wa kwanza kujua.

Kwa kawaida mimi kama mwandishi wa habari, kwa Tanzania, sikutakiwa kusema ukweli huu kuwa uchaguzi mkuu wetu ni CCM pekee, na ni Samia tuu, kwasababu kwenye msingi wa maadili ya uandishi wa habari kwenye uchaguzi, chombo cha habari hakitakiwi kuegemea upande wowote, Ila mimi kama mwandishi wa makala, ninaruhusiwa na maadili kuweka maoni yangu, tena vyombo vya habari vya nchi za wenzetu zilizoendelea, vinaruhusiwa kuchukua mrengo na kuunga mkono chama fulani au mgombea fulani ila vinachotakiwa kufanya ni kutangaza wazi maslahi, kwa kufanya kitu kinachoitwa media endorsements, kuwa chombo chetu cha habari kinaunga mkono chama fulani au mgombea fulani.

Tanzania japo hatuna media endorsements, ila ukweli unajulikana, kuna vyombo vya habari vinajulikana kabisa vinaegemea wapi.

Vyombo vya Habari vya umma, yaani public broadcasting stations, ndivyo havitakiwi kuegemea upande wowote, ila chama chenye nguvu na ukwasi wa kutosha kinalipia matangazo, hivyo kinatangazwa zaidi kuliko vyama vingine vyote au vyama makapuku!.

Nimesema uchaguzi mkuu wa leo wa rais wabunge na madiwani, ni uchaguzi wa CCM na CCM pekee, na mshindi ni CCM na Samia, kwasababu CCM inaingia dimbani ikiwa na mtaji wa utekelezaji wa ilani yake iliyopita, hivyo ina kitu cha kuonyesha, inaingia kushindana na vyama 16 ambayo havina chochote cha kuonyesha.

Siku za nyuma niliandika makala humu kuhusu katiba ya JMT ya mwaka 1977, ni katiba ya mfumo wa chama kimoja, hivyo uwanja wetu wa uchaguzi ni uwanja tenge, umeegemea upande mmoja wa chama tawala, na chama hicho ni CCM.

CCM inaingia kwenye uchaguzi kikiwa ni chama cha siasa kwa upande mmoja na ni chama dola kwa upande mwingine, hivyo chama dola kinaingia dimbani kushindana na vyama makapuku, unategemea nini?.

Niliwahi kusema uchaguzi mkuu wetu ni mashindano ya kugombea kisu cha makali kuwili, huku mgombea mmoja ameshika kwenye mpini anavutana na wagombea wanaoshika kwenye makali kuwili.

Niliandika makala kuipongeza Tume Huru ya Uchaguzi INEC kwa angalau kusawazisha kidogo uwanja tenge kwa wagombea wote 17 wa urais kwa kuwapatia magari, dereva na ulinzi, bila kuwapatia mafuta, wala waandishi wa habari wa kuandamana nao.

Hawa wagombea makapuku 16, wanashindana na mgombea mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa Chama tawala na wakati huo huo ni rais wa JMT aliyepo madarakani na ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi, anagombea huku ana nyota mabegani mwake.

Nimehesabu magari msafara wa mgombea Urais wa CCM Mwanza jana, wakati wa kuhitimisha kampeni za CCM, pale uwanja wa CCM Kirumba, ni magari zaidi ya 200!, huku yanaingurumishwa AC wakati wote wa kampeni!, baadhi ya magari hayo tunayajua yalikuwa ST, sasa ni namba za kiraia, nani atashindana?.

Niliandika humu kuhusu kwanini CCM inashinda, licha ya kushinda kwa makubwa mazuri na mema inayoyatekeleza, CCM pia inashinda kwa kukosekana upinzani imara, upinzani uliopo Tanzania ni upinzani legelege usio na uwezo wa kushindana na CCM.

Nikashauri, CCM na serikali yake ina wajibu wa kuulea upinzani ili tupate upinzani imara utaolifanya Bunge letu liweze kuisimamia serikali kikamilifu.

Bila upinzani makini na upinzani imara, CCM itabweteka, Bunge letu litaendelea kuwa Bunge butu na Bunge kibogoyo lisilo na meno.

Nimalizie kwa kuipongeza CCM na kumpongeza Rais, kwa ushindi wa kishindo, ila namuomba kwenye zile nafasi zake 10 za uteuzi wa wabunge, angalau atuteulie japo wapinzani 4, akiwemo yule mwanae wa Kigoma, kwenda kutuchangamshia like Bunge letu pale Dodoma.

Hongera CCM
Hongera Rais Samia
Hongera Watanzania Wote.
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Nikiandaa kwenda kituoni kwangu kupiga kura
Media za kenya na Nchi nyingi Duniani zinaongea kuandika kuwa Tanzania kuna uchaguzi wa ccm vs ccm yaani uchaguzi wa maigizo tu, wanashangaa kupoteza mabilioni ya walipa kodi kuzunguka Nchi nzima
 
Watanzania waamua kujitokeza kupiga kura leo kuchagua viongozi wa kuwaongoza, ni uchaguzi wa amani na haki
Watanzania wapi?
Viongozi wapi?
Uchaguzi upi?
Amani ipi wakati wapinzani wa kweli Lisu na Heche wapo jela na akina mdude na wenzao umewaua na kuwateka
 
Back
Top Bottom