Kumfanyisha Interview Medical Doctor aliyethibitishwa na Baraza la Madaktari (MCT) ni dharau kubwa sana

Kama ni wachache na wote ni proven kuwa wana vigezo vinavyo hitajika interview haina haja.
Mkuu hadi hapa sina swali kwako nimeridhika na hoja zako

Interview haina maana kama wanahitaji kuchuja idadi kwa kuangalia marks nawatumie kigezo cha GPA wenye gpa kubwa waanze kuajiriwa wenye ndogo waachwe kwani assessment wanayoifanya ni sawa na ile iliyofanywa na NECTA na TCU
 
Nimeshasema hapo juu wanapanga rank in descending order from highest marks to lowest kwahiyo wanaendelea kuchukua kwa kushuka chini kwa kadri nafasi zinapopatikana, nasikia database ni valid kwa mwaka mmoja.
Mi nilifanya interview nikapita mpaka oral. Ile kazi sikupata ila ilitokea nafasi taasis nyingine ya serikali nikaja kupata ( miezi kama 6 baadae) na barua ya kazi ilielekeza kabisa kuwa ni kwa matokea ya interview ile niliyokuwa nimefanya na kufaulu ila nikakosa nafasi kwa sababu ya competition.
Tulikuwa kadhaa na wote tulitokea kwenye ile ile interview.
NB Sina connection yeyote, hakuna mtu aliyeni connect, niliona tangazo la nafasi, nika omba, nika itwa interview nikapambana kwenda kwa shida shida hivyo hivyo na Mungu akasaidia nikapata.
Na nafasi ya engineer, nami nilipata div 1 shule, chuo nikafaulu vizuri, ni registered ERB ila interview nilifanya.
 
Sasa nimekuelewa.
Wewe itakuwa ndio wale somasoma ambao wanategemea numbers za kwenye vyeti vyao ndio Ziwatoe kimaisha.
Mwajili yetote mwenye akili hawezi kamwe kutumia kigezo cha ufaulu mkubwa kwenye cheti kukupa ajira, toa hilo akilini dogo.
Tena waajiri wengine wakiona una marks kubwa kwenye cheti hakupi kazi anajua wewe ni somasoma hauna skills out of your books.
 
Hongera mkuu hakika umepambana na siku zote ukipambana Mungu hakuachi hivi hivi

Ila kiuhalisia hukutakiwa kufanyiwa interview ingetakiwa uajiriwe direct maana assessment waliokufanyia kwenye interview ni ile ile waliokufanyia NECTA na TCU hadi ukapata div 1
 
Ndio maana shule za kata zimejaa wallimu vilaza kutokana na hakuna usaili
Nenda Shule kama IST au Feza, kama utapewa kazi bila interview hata kama una Phd ya jalalani !
Kuna jamaa angu anafundisha feza hata hajafanyiwa interview alichukuliwa moja kwa moja alipomaliza chuo tu maana wanakuwa na taasisi zao za kuwasimamia graduates vyuoni

Na kila ajira zikitoka huwa anaomba ili aingie serikalini. Kwahiyo sio kweli kuwa shule za kata zina vilaza na hizo feza zina magenius hapana ni utofauti wa kimazingira tu na usimamizi
 
mkuu, uwekewe ulinzi.

only in shithole countries. Na zaidi hapo kwenye salary ndipo panaudhi zaidi.


JESUS IS LORD&SAVIOR
 
nawe pia usikilizwe!

ila sijaelewa sana mambo yanayotakiwa zaidi ya taaluma yenyewe ya utabibu. Au ujasusi
 
Mwaka huu tutaona mengi sana.

Any way elimu yetu ipo chini sana mno kama mtu anapewa lesen ya kumaliza kitu fulani na bado haaminiwi hili liangaliwe upya

Sema kingine dakatr wa bongo akienda nchi za wenzetu mfano canada ni wazi kuwa utarudia masomo baadhi au utaenda training mwaka mmoja mwingine

Kuwafanyisha interview ni kuwa waombaji wamekuwa wengi nafasi ni chache hivyo ni ngumu kumfanyia direct placement mtu kwa kuona either Gpa

Interview is the best way to get more competent and suitable candidate
 
Ni dharau ya kiwango Cha SGR 🤔
 
According to waasisi wa mchakato huu, ni idadi kupunguzwa.
 
Kwan maana ya interview n nn??

INTERVIEW NI KUMTAFUTA MTU ALIYE BEST & COMPETENT KULIKO WOTE. Ndio maana huwa pia wanaangalia APPEARANCE na CONFIDENCE.

Au mleta mada ulimaanisha nn?
 
Daktari anachujwa kwenye kundi la daktari. Ubaya upo ?
Washinde wenzii ipate chance. Ulimwengu ni wa ushindani.
 
Dah maisha haya angalia tunavyowapigania madogo humu mpaka mishipa ya shingo inatutumka wakishapata nao wanaturundika kwenye mafoleni huku masikioni wameweka ma earphone hawana habari na sisi 😪😪😪
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…