Kumlipa Clinical Officer laki 6 sio haki hata kidogo

Sababu ulizotoa hazina msingi sana,
Kwamba wanasaidia watu,wamesoma kwa gharama kubwa.
Ili maisha yaende unahitaji taaluma na wataalamu wengi,wahasibu,wahandisi nk,na wote hao wamesoma kwa gharama kubwa!!
Swala la mshahara mkubwa inategemea umeajiliwa wapi?
Upo serikalini,muhimbili,bugando nk,au upo nje ya nchi
 
Watu wa afya mnajimwambafai sana Kumbe Scale zenu ndo utopolo ivi!? Wakati tunamaliza School Kuna masela wa PCB walienda Advance na Kugonga MD wengine wamesukuma CO yani nimepitia huu Uzi nimeona jamaa hawakupita Njia sahihi, Yani Usome MD 5 yrs uje uvute 1.5. Serious kweli!??
 
Clinical officer anafanya kazi nyingi kuliko registered nurse[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]....dogo simama jipige kifua useme mimi ni bwegemtozeni.
Daaaaah! Sipendi kucheka ila kwa hii quote yako nimecheka sana. Ajipige kifua aseme nini??[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi sekondari zetu ada zinapishana kulingana na masomo?Kwamba hapa Bagamoyo sekondari anaesoma PCB analipa ada kubwa kuliko yule wa HGK?.Hii mimi leo ndiyo naisikia
 
Ukisema anaokoa maisha ya watu kwa taaluma yake, usisahau kuna watu walimfuta kamasi na kumwekea maarifa kichwani ndipo akafika hapo.

Hao nao wasemeje? Maana wanapata chini ya hiyo laki sita.

Pigania haki badala ya kujikweza kitaaluma. Taaluma zote ni bora kwa nafasi yake.

Hebu fanya tusiwe na mgambo wa darasa la saba tu, halafu vibaka wanasumbua. Utalala wewe?
 
MD halipwi 1mil mkuu acha ubishi usio na maana.
 
Ubishi wako ni wa kitoto (wa kusubiria pilau la Krismas). Kwa hiyo unafikiri MD wa BOT, Bandari, UN naye analipwa 1.5 M kwa mwezi? Mishahara yote ya fani fulani huwa ina range.
MD halipwi 1mil mkuu acha ubishi usio na maana.
 
We shule ilikushinda sasa kwa nini ung'ang'ane na vitu havina maslahi?
 
Nabishana na mbumbumbu. Yaani hauna hata akili ya kujua kuwa mishahara ya fani fulani huwa ina range, siyo figure moja!! Basi kataa kujifunza. Kaa na hicho ulichokaririshwa (1.5 M).
Una hakika full MD mshahara wake ni 1mil? Una akili kweli?
 
Hao hao form 4 failures waliopata div.3 na 4 ndio unataka walipwe zaidi?

Si haki kabisa kuwapeleka watu wenye ufaulu mdogo kushughulika na usalama wa Afya zetu.Serikali komesheni huu upuuzi.
Ndio ata ma MD wengi sasa hivi, yani nawafahamu watu ata darasani walikuwa so average alafu leo ni madaktari kabisa, mi hanigusi mtu wa hivo.
 
Wapi huko - serikalini, UN, halmashauri, kwa Kairuki, Aga Khan, vijiweni? Haziwezi kufanana huko kote.
MD 1480000. Nimecheka sana yaani Co hawa wanaoiba mitihani. Nao wanalalamika. Kama anaona anafanya kazi kubwa aache kazi. Au aongeze shule 5 years. [emoji23] [emoji23]
 
Kamuulize mwalimu wa degree analipwa sh ngap alafu wew CO diploma unalipwa sh ngapi
 
Clinical Officer/ CO akipanda daraja mara moja anakuwa na mshahara sawa na Doctor of Medicine anaeanza kazi?
 
Kuna taaluma gani inayovuta mshahara mkubwa serikalini ( kwa payscale za serikali ) kuzidi MD ???
 
Kasome
Nenda kasome bro uongeze elimu,CO ni cheo kidogo sana ktk fani ya udaktari.
Hivyo nakushauri rudi shule ukasome.
 
Clinical Officer/ CO akipanda daraja mara moja anakuwa na mshahara sawa na Doctor of Medicine anaeanza kazi?
Hapana. Akipanda anaenda kuwa sawa na Lab/HSM/EHS anayeanza kazi.
 
Kwahiyo unataka kusema nurse ndie anayetengeneza diagnosis? na treatment plan? au sio? mgonjwa anapokwenda hospitalini anaanza kwa nurse anampa matibabu alafu daktari anafuata au sio? tunapopataga dharura pale emergency usiku yule kwenye chumba cha daktari kumbe ni nurse asanteni kwa kutufungua sisi wasomi tusioelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…