Kumruhusu binti akajitafutie maisha ni kumfanya awe Malaya

Kuna familia bana wamefanya hili, tukashangaaa ila ndiyo hivyo!! Watu tukabaki kusema wana mambo ya kale sana, ila imeunganishwa familia yenye mafanikio na familia iliyofanikiwa zaidi...
Huyo jamaa yako hakuwa na misingi mizuri tu ya kimaisha (kiuchumi), na pengine hakuwa anapendwa maana watoto wa kike wa vigogo wakikupenda wamekupenda for real (hawajafata mali kwako).
 
Huyo jamaa yako hakuwa na misingi mizuri tu ya kimaisha (kiuchumi), na pengine hakuwa anapendwa maana watoto wa kike wa vigogo wakikupenda wamekupenda for real (hawajafata mali kwako).
Atakuwa alikuwa haeleweki na binti kwao wanaona umri unaenda.
Angeweka misimamo na kwenda kujitambulisha mapema anagalau wangejua yupo serious
 
Halafu wewe mleta mada huna wazazi wakukemee uache kuandika mambo ya wanawake

Una Tatizo gani?
Kutwa kuandika mambo ya kike

Mambo ya wanawake waachie wenyewe
Wanajua cha kufundishana kitchen party unatia aibu.Mwenye ndugu anayemfahamu Huyu mleta mada mwambieni ya wanawake aache
 
Kwako na Kwa watu masikini ndio hayawezekaniki.

Ila Familia zote kubwa zinatumia kanuni hizo...
Usi-generalize hivyo mkuu ilikuonyesha tu kuwa yote uliyoyasema kwenye uzi wako ni valid, swala la kusema matajiri WOTE huwachagulia mabinti zao sio kweli (wapo ila sio wote), mara nyingi wao huangalia mtu smart kiakili na aliyeridhiwa na binti yao.

Kuna jamaa mmoja kule mwanza alikuwa anadate na binti wa katibu wa wozara fulani enzi za JPM na sasa SSH, alikuwa ni msomi ila hakuwahi kuajiriwa kwahiyo maisha yake yalitegemea bishara za kawaida tu. Binti alimuelewa jamaa kiasi kwamba hakuna alilosikia kutoka kwa wazazi wake juu ya yule jamaa.

Kilichofanyika jamaa aliozeshwa yule binti kisha akaingizwa kwenye system ya biashara za yule mzee na baadae akadaka kitengo srikalini, sasahivi ni mwendo wa V8 na Range tu.

Yule mchengerwa ni mkwe wa mtu fulani mzito serikalini (kaoa binti wa kigogo) na anakula maisha tu, mbona hakukataliwa? Maana hakuwa na maisha mazuri huko nyuma.
 

Unatatizo la Msingi!

Huna ufahamu wa kusoma makala?
Hapo ulichoona wanaozungumziwa ni wanawake tuu, hujaona wajibu wa Baba Kwa binti yake?

Au ndio umevurugwa na maisha?
 
Mbona zinaoana Mkuu!

Binti anaweza akaleta Mkwe ukaweka mazingira ya Mkwe kuelewana na wewe na kukuheshimu. Mbona rahisi sana
Mapenzi hayawezi kutengenezewa mazingira mazuri na wazazi bila ya wao wapenzi wawili kuelewana na kuridhiana mkuu, na haiwezi kuwa rahisi huko kwenye ndoa kama unavyodai.

Kwamba watu fulani wapendane na waishi kwa amani kwakua wazazi wametaka, kwa miaka mingapi, vipi hao wazazi ikifikia wakati wasiwepo?
 

Ninakuelewa Mkuu!
Ila tunajumuisha mambo Kwa kuangalia wingi/mzani ulipoegemea
 

Lisilowezekana kwako Kwa wengine yanawezekana.

Alafu zingatia, mapenzi ni maamuzi tuu!
Unaweza kujiamulia mwenyewe au kuamuliwa na wazazi wako.
 
Atakuwa alikuwa haeleweki na binti kwao wanaona umri unaenda.
Angeweka misimamo na kwenda kujitambulisha mapema anagalau wangejua yupo serious
Ndio nilichomaanisha , au kama angekuwa na uhakika kabisa kuwa huyu binti ndiye atekaemuoa na kuisha nae isipokuwa mambo bado anajipanga angeenda tu kwakina binti kujitambulisha kisha akamjaza hata kibendi (kwa kumshawishi yule binti).
 
Hata Mungu amepiga marufuku mabinti wadogo kuwa wajane, wakifiwa na waume zao na waolewe mapema, hilo suala la kulea wenyewe sio haki yao.

Hivyo hoja inaendelea kusimama kwenye ukweli kuwa mwanamke hajaumbwa kujitafutia maisha…. kwa hayo machache naunga mkono hoja.
 
Hayo yalikuwa ni ya enzi za Ujima na yaliwezekana kipindi hicho.

Ila sasa mambo yamebadilika, huwezi kumchagulia binti mtu wa kuolewa nae na wala huwezi kumlazimisha kuolewa.

Kwa kifupi uliyoyaandika karibia yote hayawezekani.
Na wanaojichagulia wenyewe wanashindwa kudumu kwenye ndoa hata kwa miezi sita Mahakamani kila siku zinafunguliwa kesi za kuomba kutalikiana na vijana hao hao waliojichagulia wachumba wenyewe, sasa kipi bora ujima au usasa? Huu usasa tuwaachie wenyewe sisi waafrika tuna tamaduni zutu ivyo tuzienzi na kuwafundisha watoto wetu
 
Primitive thinking.
Usiseme hivyo jamani,sawa unaweza kusema maana hamna kanuni uliyoivunja.Lakini ujue(kwa mtazamo) siyo VYEDI!
Zaidi kama ulikuwa na hoja ya kupinga hayo ungeiweka au kwasababu zilizo nje ya uwezo,ungesema kwa ufupi kwamba kunasababu kadhaa ila sina uwezo wakuzieleza kwasasa!
 
Kila mzazi angependa hivyo ila tatizo linakuja, hauna uhakika kama huyo binti yako atakuja kuolewa na mtu sahihi. Anaweza akajituliza akaja kuolewa na mtu mshenzi ukaja kujuta kuwa bora mwanao angeweza kujitegemea hivyo angeepuka kunyanyasa. Si hivyo tu, utakuta familia nyengine binti ndio kasoma na ana nafasi amabayo akitumia vizuri atamsaidia familia, sasa kwa hali hiyo, unataka wazazi wamng'ang'anie aache kujitafutia fursa na riziki zake????!!!!!
 
Kati ya watu wanaojaza DIARY yangu nawewe ni miongoni kwa nyuzi zako(sisemi kwamba zote au kuna asilimia zote za ukweli) lakini baadhi ya nyuzi zoko ni MIONGOZO.
Kuna na yule wa " hatima ya maisha yangu ipo...(BM X6 ).Katika uzi wake nili-copy mistari mpaka baasi!
Mengi ni mema ila baadhi yanahitaji akili za kuambiwa uchanganye na zile zinazokujia kwa muda uliopo/mahsusi.

Tukumbuke watoto wa kike wakilelewa vizuri,mambo mengi yanaweza kubadilika katika jamii yetu!
Kwa wale walibahatika kuwapata watoto wa kike lazima wamakinike na uzi huu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…