Superb2014
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 9,266
- 7,426
Inategemea.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kila mzazi angependa hivyo ila tatizo linakuja, hauna uhakika kama huyo binti yako atakuja kuolewa na mtu sahihi. Anaweza akajituliza akaja kuolewa na mtu mshenzi ukaja kujuta kuwa bora mwanao angeweza kujitegemea hivyo angeepuka kunyanyasa. Si hivyo tu, utakuta familia nyengine binti ndio kasoma na ana nafasi amabayo akitumia vizuri atamsaidia familia, sasa kwa hali hiyo, unataka wazazi wamng'ang'anie aache kujitafutia fursa na riziki zake????!!!!!
Na wanaojichagulia wenyewe wanashindwa kudumu kwenye ndoa hata kwa miezi sita Mahakamani kila siku zinafunguliwa kesi za kuomba kutalikiana na vijana hao hao waliojichagulia wachumba wenyewe, sasa kipi bora ujima au usasa? Huu usasa tuwaachie wenyewe sisi waafrika tuna tamaduni zutu ivyo tuzienzi na kuwafundisha watoto wetu
Maisha ya kizamani hayo.
Kwanini usimruhusu binti ajitegemee??
Akifika umri wa mtu mzima wacha akapambane huko, kukaa ndani kama yai na kusubili kuletewa kila kitu kunamlemaza.
Hao ndo wakiolewa na bahati mbaya waume zao wakafariki mapema baada ndoa hushindwa kuendesha famili kwakua na misingi mibovu, hawezi kitu chochote kile ye kazoea kulishwa kama kinda la ndege.
Ushauri wako unatengeneza kizazi cha wanawake waoga wasioweza kthubutu na kuchangamkia fursa, wanawake waoga wasioweza kutunza familia zao wala kulea watoto wao.
Ukapange dada ukutane na masiharaPrimitive thinking.
Hukumuelewa kasema aolewe na mtu anayeelewana na mzaziNamba 3 unasema binti akifika umri wa kuolewa basi aolewe iwe ni kwa kupenda au kwa kulazimishwa, tena ukasisitiza ikiwa hajapata wa kumuoa basi wazazi wamtafutie mwanaume.
Namba 6 unadai mzazi ahakikisha mtoto wake anaolewa na mtu anayeeelewana nae, anaempenda na mwenye kujuia thamani ya ndoa, unadhani huyo mtu anaweza kupatikana tukiamua kutumia hiyo stratagy ya 3?
Huoni kama hizo aya mbili tayari hazirandani? Kwanza umri wa binti kuolewa ni upi, maana mimi sidhani kama upo fixed.
Uoga kwa maana ipi??Mwanamke bila uoga haitwi mwanamke.
Unasomea mwanamke jua unamzungumzia kiumbe gani!
We jamaa unaongelea maisha ya kizazi cha kina Musa.Hata Mungu amepiga marufuku mabinti wadogo kuwa wajane, wakifiwa na waume zao na waolewe mapema, hilo suala la kulea wenyewe sio haki yao.
Hivyo hoja inaendelea kusimama kwenye ukweli kuwa mwanamke hajaumbwa kujitafutia maisha…. kwa hayo machache naunga mkono hoja.
Wewe umenena vyema.Uko sahihi na pia mambo huwa yanaharibika kwa mabinti wakiwa chuoni sababu wazazi wanawachukulia tayri ni watu wazima kitu ambacho si sahihi.
Binti hata akiwa chuo lazima bado awepo chini ya uangalizi kwanza kwa kujua anaishi wapi na hata kumtembelea kwa kushtukiza ili kama kabadilika uweze rekebisha.
Malezi pia hayaishii kwa mabinti hata wavulana Kuna ndugu yetu mmoja alipata kazi mkoa mwingine mzee wake akamtafuta mtu anayemuamini kule akampokea akakaa kwake kwa muda ndio akajitenga.
Kwanza kama mtoto ana akili nzuri hata akioa naweza mshauri akae nyumbani ili aendelee kusave hela.
Hapo kwenye kumchagulia mtu wa kumuoa wakikosana atakulaumu Maisha yote nadhani tusiwape mabinti pressure yakuona ndoa ni Kila kitu na kwamba wasipokuwa nayo wamefeli.
daah hata nilizojenga mimi sio zangu tena mkuu???KUMRUHUSU BINTI AONDEKE NYUMBANI AKAJITAFUTIE MAISHA NI KUMFANYA AWE MALAYA!
Anaandika, Robert Heriel.
Mwanamke hatafuti maisha Ila anatafutiwa, maisha ya mwanamke yapo Kwa mume wake au Mzazi wake. Ni hatari na kosa kubwa kumruhusu binti yako akatafute maisha. Mwanaume ndiye anayekula Kwa jasho, neno Kula Kwa jasho linamaanisha "kutafuta" ili utafute basi itakupasa usijue kitu unachokitafuta kipo wapi na utakipata lini.
Mzazi unaanzaje kumruhusu Binti yako umpendaye akatafute maisha ambayo hajui yako wapi na atayapata lini, huo ni upumbavu, na kutokumpenda binti yako.
Binti anapaswa akishakua anaandaliwa mazingira ya kuolewa, Kama atakuwa amebahatika kupata kazi basi Alhamdulullah!
Kumruhusu binti akatafute maisha inamaanisha umeruhusu binti yako afanye umalaya,
1. Binti aombe kazi akiwa nyumbani kwako au nyumbani Kwa Ndugu yako unayemuamini bila kujali umri wa binti yako.
2. Usimruhusu binti kupanga chumba na kujitegemea ikiwa hana kazi maalumu, hajaajiriwa.
Mzazi ni Bora umuajiri binti yako mwenyewe ikiwa Ajira zinasumbua kuliko binti ajiajiri mwenyewe akiwa mbali na hapo nyumbani.
3. Binti akifikia umri wa kuolewa, hakikisheni anaolewa iwe Kwa Kupenda mwenyewe au kutokupenda.
Mwambieni umri wa kuolewa umefika, Kama anamchumba amlete nyumbani. Kama hana mwambie mnampa muda Fulani amlete mchumba akishindwa mwambieni mtamtafutia ninyi wenyewe.
4. Ni marufuku binti kufanya kazi za kujidhalilisha utu wake, au zenye mazingira ya kuudhalilisha utu wake. Kama Muziki wa kidunia. Sio binti anafanya vitu vya kipuuzi puuzi na kuanika uchi wake kwenye majukwaa Kama mwendawazimu.
5. Kama binti atapata kazi ya kuajiriwa mbali na nyumbani, akapanga nyumba basi muambieni mtampatia ndugu mdogo WA kuishi naye na kumsaidia kazi.
6. Ni vizuri umuozeshe binti yako Kwa kijana mnayeheshimiana hii itapunguza uonevu, unyanyasaji na hata kutalakiana kusiko Kwa muhimu.
Sio binti aokote wahuni wahuni wa uko mjini wasio ijua hata Imani na maana ya ndoa.
7. Mfanye binti yako akuelewe unataka nini kwake. Hii itapunguza mifarakano baina yako na yeye. Binti Yako asipokuelewa atakuwa mbaya zaidi.
8. Mtiishe mama yake na kumfanya mama yake awe Mke Bora ili aige kutoka Kwa Mama yake.
Mke wako akikushinda basi hata watoto wako watakushinda, hakikisha mkeo umemshepu vile unavyotaka ili isikusumbue katika malezi ya binti zako.
Madhara ya kushindwa kumtiiisha Mkeo utayaona Kwa watoto wako.
9. Usikubali mtu amchezee Binti Yako ungali upo hai.
Hakikisha Jambo hilo binti yako analifahamu. Hiyo itamfanya hata yeye asikubali mtu yeyote amchezee.
Ikiwa utashindwa kumlinda binti yako na kumpigania Kwa nguvu zote basi hata yeye atashindwa kujilinda na kujipigania.
Kitu chochote kisicholindwa kamwe hakiwezi ijua thamani yake. Hivyo hata chenyewe hakitaweza kujilinda.
10. Mfanye binti yako asiwe na Shaka juu ya Maisha. Mwambie hapo nyumbani ni kwao. Asiwe na presha ya kujitegemea kwani mwanamke hapaswi kuwa na fikra hizo. Mwambie, mwanamke ananyumba mbili, Kwao na Kwa mume wake.
Wakati mwanaume hana nyumba hata moja. Hata alizojenga sio zake.
Kuruhusu mwanamke kutafuta maisha NI Kumtupa kwenye shimo lenye nyoka wakali.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Safarini kuelekea Arusha,
hapana bro,nimeishasema kule post ya nyuma kidogo,utumie ushauri huu kulingana na mazingira pia hata hali ya mtendewa!Asante sana kwa mada nyingine nzuri nimeichukua jinsi ilivyo kwaajili ya binti yangu.
Ni vizuri maana umeibua fikra mpya,maana yake usimchunge bali mshibishe madini ya ubongoUkolini mtupu,mtu kasoma chuo uko ukiwa nae mbali ,akimaliza ndio uje ukamfuge nyumbani huoni Kuna mapungufu apo,kwaiyo nyumbani ndio salama au..ebu tusi danganyane mkuu,labda kama umemuwekea kufuli la gps na camera.