Kumruhusu binti akajitafutie maisha ni kumfanya awe Malaya

Kumruhusu binti akajitafutie maisha ni kumfanya awe Malaya

KUMRUHUSU BINTI AONDEKE NYUMBANI AKAJITAFUTIE MAISHA NI KUMFANYA AWE MALAYA!

Anaandika, Robert Heriel.

Mwanamke hatafuti maisha Ila anatafutiwa, maisha ya mwanamke yapo Kwa mume wake au Mzazi wake. Ni hatari na kosa kubwa kumruhusu binti yako akatafute maisha. Mwanaume ndiye anayekula Kwa jasho, neno Kula Kwa jasho linamaanisha "kutafuta" ili utafute basi itakupasa usijue kitu unachokitafuta kipo wapi na utakipata lini.

Mzazi unaanzaje kumruhusu Binti yako umpendaye akatafute maisha ambayo hajui yako wapi na atayapata lini, huo ni upumbavu, na kutokumpenda binti yako.

Binti anapaswa akishakua anaandaliwa mazingira ya kuolewa, Kama atakuwa amebahatika kupata kazi basi Alhamdulullah!

Kumruhusu binti akatafute maisha inamaanisha umeruhusu binti yako afanye umalaya,

1. Binti aombe kazi akiwa nyumbani kwako au nyumbani Kwa Ndugu yako unayemuamini bila kujali umri wa binti yako.

2. Usimruhusu binti kupanga chumba na kujitegemea ikiwa hana kazi maalumu, hajaajiriwa.
Mzazi ni Bora umuajiri binti yako mwenyewe ikiwa Ajira zinasumbua kuliko binti ajiajiri mwenyewe akiwa mbali na hapo nyumbani.

3. Binti akifikia umri wa kuolewa, hakikisheni anaolewa iwe Kwa Kupenda mwenyewe au kutokupenda.
Mwambieni umri wa kuolewa umefika, Kama anamchumba amlete nyumbani. Kama hana mwambie mnampa muda Fulani amlete mchumba akishindwa mwambieni mtamtafutia ninyi wenyewe.

4. Ni marufuku binti kufanya kazi za kujidhalilisha utu wake, au zenye mazingira ya kuudhalilisha utu wake. Kama Muziki wa kidunia. Sio binti anafanya vitu vya kipuuzi puuzi na kuanika uchi wake kwenye majukwaa Kama mwendawazimu.

5. Kama binti atapata kazi ya kuajiriwa mbali na nyumbani, akapanga nyumba basi muambieni mtampatia ndugu mdogo WA kuishi naye na kumsaidia kazi.

6. Ni vizuri umuozeshe binti yako Kwa kijana mnayeheshimiana hii itapunguza uonevu, unyanyasaji na hata kutalakiana kusiko Kwa muhimu.
Sio binti aokote wahuni wahuni wa uko mjini wasio ijua hata Imani na maana ya ndoa.

7. Mfanye binti yako akuelewe unataka nini kwake. Hii itapunguza mifarakano baina yako na yeye. Binti Yako asipokuelewa atakuwa mbaya zaidi.

8. Mtiishe mama yake na kumfanya mama yake awe Mke Bora ili aige kutoka Kwa Mama yake.
Mke wako akikushinda basi hata watoto wako watakushinda, hakikisha mkeo umemshepu vile unavyotaka ili isikusumbue katika malezi ya binti zako.
Madhara ya kushindwa kumtiiisha Mkeo utayaona Kwa watoto wako.

9. Usikubali mtu amchezee Binti Yako ungali upo hai.
Hakikisha Jambo hilo binti yako analifahamu. Hiyo itamfanya hata yeye asikubali mtu yeyote amchezee.

Ikiwa utashindwa kumlinda binti yako na kumpigania Kwa nguvu zote basi hata yeye atashindwa kujilinda na kujipigania.
Kitu chochote kisicholindwa kamwe hakiwezi ijua thamani yake. Hivyo hata chenyewe hakitaweza kujilinda.

10. Mfanye binti yako asiwe na Shaka juu ya Maisha. Mwambie hapo nyumbani ni kwao. Asiwe na presha ya kujitegemea kwani mwanamke hapaswi kuwa na fikra hizo. Mwambie, mwanamke ananyumba mbili, Kwao na Kwa mume wake.
Wakati mwanaume hana nyumba hata moja. Hata alizojenga sio zake.

Kuruhusu mwanamke kutafuta maisha NI Kumtupa kwenye shimo lenye nyoka wakali.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Safarini kuelekea Arusha,
Hapo mwisho kwnye Mwanaume hana nyumba hata 1 ht alizojenga nimekubali sana mkuu [emoji106][emoji106]
 
Hayo yalikuwa ni ya enzi za Ujima na yaliwezekana kipindi hicho.

Ila sasa mambo yamebadilika, huwezi kumchagulia binti mtu wa kuolewa nae na wala huwezi kumlazimisha kuolewa.

Kwa kifupi uliyoyaandika karibia yote hayawezekani.
Kwa ufupi huyu kijana ni theretical sana.
 
Kuna mtu wangu wa karibu Sana, kamruhusu binti yake kwenda moja ya jiji hapa nchini akatafute maisha binti hana kazi wala biashara,,, aisee ni aibu yani na busara zote ukali misimamo ya yule mzee ila bintiye kamshindwa,, Ni masikitiko
 
😂😂😂
Huko ni kumzingua tuu Binti wa watu.
Rushwa ya ngono kupata kazi,
Kama hajapata kazi, kuanza kujiuza ndio kunafuatia.

Hapo ndipo Waswahili wanapopata hoja kuwa, Kama mkwe wao Hana uwezo waje waishi palepale nyumbani na binti Yao, wakifanya vishughuli vyao vya hapa na pale
 
Nadharia nyingiii
Baadhi nzuri zinatekelezeka
Baadhi hazitekelezeki

Unadhani kuna mtu anapenda maisha ya misukosuko?
Kuandika ni kazi rahisi sana

Una binti?
 
Alhamdullilah umejaaliwa

Maisha yatakuonyesha uhalisia
Mark this thread afu uje uisome wakiwa arnd 30 yrs of age

Maisha yanaongozwa na Supernatural power, hayajiendeshi yenyewe.
Nilichokieleza ndichi kinapaswa kufanywa bila kujali matokeo yatakuwaje.
 
Maisha yanaongozwa na Supernatural power, hayajiendeshi yenyewe.
Nilichokieleza ndichi kinapaswa kufanywa bila kujali matokeo yatakuwaje.
Kupanga ni kuzuri sana
Ila uhalisia wote tunaujua
Na Mungu nae anapanga
Ngoja mabinti wakue kwanza

Saivi ni rahisi kuwasema wa wengine
 
Kupanga ni kuzuri sana
Ila uhalisia wote tunaujua
Na Mungu nae anapanga
Ngoja mabinti wakue kwanza

Saivi ni rahisi kuwasema wa wengine

Sisemi wawengine nasema vile Wababa wanavyotakiwa kuwa Mabaya Kwa kufanya wajibu wao kulinda na kutunza mabinti zao.

Watoto kuharibika 90% wazazi ndio chanzo, mzazi hawezi kukwepa Jambo hilo kivyovvyote.

Kauli za kusema subiri mtoto akue ni Kauli za watu walioshindwa na wenye mtazamo wa kushindwa

Unanikumbusha wakati ninakua nikiwa nawaambia watu sitokunywa pombe wala kuvuta sigara baadhi ya watu wakawa wananiambia vikauli mshenzi Kama vyako,
😂😂

Maisha Kwa sehemu kubwa 90% ni maamuzi na machaguo ya mtu, 10% ni Accidentally.
 
Hata mm siwez kumwacha binti yangu akajitegemee ili hali hana chakufanya wala ajira....ukimwacha unamtengenezea mazingira ya ushawishi natamaa...#kama mm kipindi sina ajira siku achwa nawazazi wangu kwann bint yangu nimwache...#
 
Mi walaaa

Langu moja tu subiri mabinti wakue
Ndipo utaelewa wazazi wengine

Kwa sasa naona bado unajadili the shoes ur not wearing

Pombe na sigara ni maamuzi binafsi mtu unaweza kujidhibiti

Ila hali na tabia ya watoto wako u cant control 100%
Hali yako ya kiafya,kiuchumi na kimaisha wakiwa wakubwa bado hujaijua
Hali ya maisha nchini,duniani ktk soko la ajira,kujiajiri na soko la ndoa bado hujalijua

Langu la mwisho
Tusubiri mabinti wakue

Wakishakua ndio utaelewa

Ni kama vile asiye na mtoto akufundishe kulea mwanao saivi
 
Hata mm siwez kumwacha binti yangu akajitegemee ili hali hana chakufanya wala ajira....ukimwacha unamtengenezea mazingira ya ushawishi natamaa...#kama mm kipindi sina ajira siku achwa nawazazi wangu kwann bint yangu nimwache...#
Akipata ajira mbali na nyumbani asiende?.
 
Mwanamke ananyumba mbili, Kwao na Kwa mume wake. Wakati mwanaume hana nyumba hata moja. Hata alizojenga sio zake
Daaaaah maisha ya mwanaume yamejaa tabu hadi anaingia kaburini
 
Umeshasema akipata ajira, inamaana atakuwa nakitu kinachomuingizia kitasababisha asiwe na tsmaa
Mtoa mada kasema akipata ajira ya mbali asiende ama aende na msindikizaji
Hao wasindikizaji wapo sikuhizi?
 
Mwanamke ananyumba mbili, Kwao na Kwa mume wake. Wakati mwanaume hana nyumba hata moja. Hata alizojenga sio zake
Daaaaah maisha ya mwanaume yamejaa tabu hadi anaingia kaburini
Ujenge afu usipaite kwako
Ni kwako na mkeo
Misalaba mingine mnajibebesha
 
Alhamdullilah umejaaliwa

Maisha yatakuonyesha uhalisia
Mark this thread afu uje uisome wakiwa arnd 30 yrs of age
Nafikir hakuna haja ya kumuapiza mtoa mada. Kimsingi aliyoyaongea yana ukweli kwa kiasi kikubwa. Kwa wanaoishi maeneo ya kinondoni, Sinza Kuna mabinti wengi wamemaliza chuo wamepangisha vyumba wanajitegemea wakiwa hawana kazi maalum. Ni aibu kwakweli, mdada anakuwa na wanaume wengi km Kijiji lkn anakwambia Hana jinsi maana anataka kulipa Kodi, umeme, maji, taka, ulinzi na chakula chake. Ni muhim wasichana kubaki nyumbani mpaka atakapopata shughuli ya uhakika ndo akajitegemee.
 
Back
Top Bottom