Kumshambulia Hayati Magufuli kunaweza ligawa Taifa na kupunguza nguvu ya CCM kanda ya Ziwa

Kumshambulia Hayati Magufuli kunaweza ligawa Taifa na kupunguza nguvu ya CCM kanda ya Ziwa

Nianze moja kwa moja kutoa maoni yangu kwa hali ya kisiasa nayoiona. Kifo cha Rais Magufuli imeacha pengo kubwa sana kwenye taifa. Kwa wale wasiopenda kusikia jina la magufuli niseme tu, Hayati alikuwa na wafuasi wengi kifo chake kimedhirisha hivyo na atakumbukwa siku zote kwa mambo mazuri aliyolifanyia taifa hili.

Niseme tu wazi si kila jambo alilolifanya hayati ni baya kwenye taifa hili. Ameacha alama kubwa sana. Licha ya kuwa na matatizo ya moyo alijitolea usiku na mchana kulipigania taifa lake.

Najua akili ni nywere na kila mtu ana zake. Watu wanaodai magufuli alikuwa fisadi unashindwa kuelewa jinsi walivyo na kumbukumbu ndogo ya aina ya ufisadi tuliyopitia kwenye taifa hili kabla ya magufuli kuingia madarakani. Kumbukeni ufisadi wa TEGETA ESCROW, EPA, BOMBA LA GAS MTWARA. Sote tunajua viongozi wa Afrika wakiiba pesa wanapeleka wapi. Wanakimbiza nchi za maghariba..kama Hayati aliiba hayo mabillioni yako wapi? Matrillion yako wapi?

Ameanzisha ujenzi wa reli kwa gharama ndogo sana uki compare na majirani zetu tena ya kutumia umeme.

Magufuli anatoka kanda yenye nguvu kiasiasa. Ukweli ni kwamba magufuli ameumiza sana watu wa kanda hiyo na taifa kwa jumla. Kitendo cha kuendelea kumshambulia kwa tuhuma ambazo watu wenye akili za kawaida kabisa wanajua zina malengo ya kisiasa nikutengeneza magawanyiko mkubwa huko mbeleni.

Kuna kitu magufuli kaacha kwenye mioyo ya watanzania. Nacho ni uzalendo. Wamejua kuhusu ukoloni mamboleo na jinsi baadhi ya viongozi wanavyotumika na nchi za magharibu kuhujumu mataifa yao either kwa ufisadi, mikataba mibovu etc.

Nimalizie kwa kusema, magufuli hakuwa malaika. Binafsi kuna mambo kadhaa niliyapinga kwenye utawala wake lakini niseme ni kiongozi mzalendo hili taifa kuwahi kupata.

Kama mnataka tuamini huo ufisadi mtueleze MAGUFULI KAFICHA HELA WAPI? Alizibeba kwenye sandarusi? Ana account ya pesa ulaya? MUNGU ATAMLIPA KIUMBE WAKE. KAKIKA KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.

Mwisho kabisa kabla haujaendelea na mkakati ovu wa kumshambulia magufuli labda ujiulize. MAUAJI YA ALBINO YAKO WAPI? UFISADI MKUBWA UKO WAPI? UJAMBAZI UKO WAPI? KUKATIKA UMEME JE? AU TUMESAHAU JINSI MAJENERETA YALIVYOKUWA YANATUUMIZA MASIKIO?

Hakika MUNGU ATAMLIPA JPM kwa kutetea wanyonge na watu wasiokuwa na nguvu. Miaka 100 ijayo utakuwepo? Basi jifunze na beba mema ya hayati JPM mabaya muachie Mungu wake atamuhukumu.

Daudi alimwaga damu lakini Mungu alimkumbuka.
CCM kanda ya ziwa ni Magufuli. Kama hayupo jibu mnalo
 
Kwani uraiani nako watu wanamchukia Magufuli kama ilivyo kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Twitter na Ufipa?

Bado naamini Rais Magufuli alikuwa anaungwa mkono na idadi kubwa ya watu walio wengi.

Na watu hao walituma ujumbe wao kipindi cha msiba wake.

Aliungwa mkono na watu wasiojua lolote, wenye maslahi binafsi na madaraka yake, na wale waliotekwa na propaganda zake baada ya kuzima uhuru wa habari. Hizo kura za watu wa kanda ya ziwa wataenda kuombwa, ni juu yao kutoa ama kuacha maana hiyo ndio demokrasia. Kujaa kwenye msiba wake sio tatizo maana sio watanzania wote walienda, na kwenda kwenye msiba sio dalili ya kukubalika, labda mtafute sifa nyingine. Na kama alikuwa anakubalika sana, kipi kinawafanya mlie hao wachache wakiweka udhalimu wake hadharani?
 
Wasingejaa iko Lugha ambayo ungeitumia kusema kuhusu msiba huo!! Maana wabongo bhana Ni shida!
 
Na bado na bado na bado mpaka huu mwaka uishe mtaongea na kutukana vyote ila ukweli uko pale palemwendazake keshaondoka tena kibaya zaidi sio kaondoka madarakani no kaondoka moja kwa moja
Usiumize akili yako kushindana na hiyo jamaa ni gasho.
 
Ufisadi ambao ni rahisi kuusema ni ule wa kubeba hela kwenye gari na kuhonga mabarabarani.
Kuchota mengine na kujenga int. airport kijijini, lakini chuki mnayovuna wapambe wake inatokana na bwana wenu kuwa katili sana.
Kipindi cha JK, Mkapa, Mwinyi ,, ufisadi ulokuwepo lakini hawakuwa wakatili na ndo maana huoni chuki dhidi yao.

Sasa huyu bwana wenu alokuwa
FISADI jumlisha UKATILI.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Sema wewe utamkumbuka,
Siwezi kumkumbuka daima Magufuli hata iweje,usipende kuunganisha eti tutamkumbuka.
Mkumbuke kwa lipi,muache huyo muuaji alale panapostahili.
Usingefuatilia huu mjadara kama Kweli hutaki umkumbuke Magu, na kuhusu yeye mwaka huu wote nyuzi za kumhusu yeye zitakuwa nyingi kuliko hata mradi wa kifisadi na Mkataba wa hovyo wa bandari ya Bagamoyo na kuliko propesa Muongo!!
 
kwa sababu walijitokeza wengi barabarani?.
Watanzania tunapenda matukio na wapo wengi waliokwenda kushuhudia tukio la kihistoria la rais kufa madarakani
Wasingejitokeza ndio ingekuwa matukano makubwa Sana kwa wapinzani wake kama wewe

Mnakosaga la kusema basi
 
1.5 tirion ilipotea kipindi cha nani?
Na usituchanganye kabisa , Kikwete aliruhusu watu kujadiri Wizi kwenye Nchi yao, yeye hata Kukopa alikuwa anakopa kwa siri

Uchumi wa Gizani

Yaani maufisadi yoooote ya Kipindi cha Kikwete uliyoyasema , tuliyajua kwasababu Kikwete mwenyewe alitaka tuyajue, angetaka kuficha angeweza na angetoka madarakani bila kuwa na rekodi unazosema,

Kuficha tatizo, haina maana kwamba hakuna tatizo, limefichwa
Mwendazake ndo alitengeza UFISADI MKUBWA za8di kuliko awamu zote.
Zile Escrow, EPA, IPTL etc ukijumlisha zoote ni BILLIONS tu hufiki kwenye huu ufisadi wa mwendazake!!! Yaani miaka 5 tu jamaa kakupigia 1.5 TRILLION!!!
 
Ufisadi ambao ni rahisi kuusema ni ule wa kubeba hela kwenye gari na kuhonga mabarabarani.
Kuchota mengine na kujenga int. airport kijijini, lakini chuki mnayovuna wapambe wake inatokana na bwana wenu kuwa katili sana.
Kipindi cha JK, Mkapa, Mwinyi ,, ufisadi ulokuwepo lakini hawakuwa wakatili na ndo maana huoni chuki dhidi yao.

Sasa huyu bwana wenu alokuwa
FISADI jumlisha UKATILI.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Uwanja wa Ndege wa chato, kama unajina la Magufuli, au mmiliki wake ni Magufuli huo ndi ufisadi haswaa

Yeye kajenga Kwa ajili ya nchi, hawautaki, waanzishe machimbo ya zege, maana zege lililolala hapo si mchezo
 
Unaweza kuwa unalaumu kitu lakini usijue Kiini chache marehemu aliligawa taifa akiwa mzima na anaendelea kuligawa akiwa kaburini
 
Mwendazake ndo alitengeza UFISADI MKUBWA za8di kuliko awamu zote.
Zile Escrow, EPA, IPTL etc ukijumlisha zoote ni BILLIONS tu hufiki kwenye huu ufisadi wa mwendazake!!! Yaani miaka 5 tu jamaa kakupigia 1.5 TRILLION!!!
CAG huyu kaja na ukaguzi wa miaka mitano yote, Je Hilo la Tr1.5 umeliskia Kwenye hii ripoti??
 
Unaweza kuwa unalaumu kitu lakini usijue Kiini chache marehemu aliligawa taifa akiwa mzima na anaendelea kuligawa akiwa kaburini
Ujinga tu na ufupi wa akili ndio unaona hivyo
 
Kanda ya nyonyo wenyewe wanamkataa na hawajawahi kuwa nae isipokuwa wale wapenda mtelezo waliojipendekeza kupata vyeo iweje taifa ligawanyike kwa kushambuliwa kwake?

Ona huyu nae,Message was sent clearly wakati wa msiba wake! Huu ndiyo ukweli na hauwezi kuuficha. Kanda ya Ziwa especially Mwanza-Geita to Chato walituma message kwa Taifa hili. JPM atabaki kuwa shujaa wetu.
 
Ufisadi ambao ni rahisi kuusema ni ule wa kubeba hela kwenye gari na kuhonga mabarabarani.
Kuchota mengine na kujenga int. airport kijijini, lakini chuki mnayovuna wapambe wake inatokana na bwana wenu kuwa katili sana.
Kipindi cha JK, Mkapa, Mwinyi ,, ufisadi ulokuwepo lakini hawakuwa wakatili na ndo maana huoni chuki dhidi yao.

Sasa huyu bwana wenu alokuwa
FISADI jumlisha UKATILI.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Hivi ile hela aliyokuwa akibeba mailioni kwenye Sandarusi halafu anagawa kama njugu mawe zilikuwa zinakuwa accounted kivp?? No cheque no any official transaction no nothing....!!! Halafu utasikia jiwe anasema....UKINUNUA DAI RISTI NA UKIUZA TOA RISTI......Lakini yeye akichukua au kutoa pesa ilikuwa hakuna cha receipt wala kumbukumbu yoyote....!! Je, ni fedha kiasi gani ya walipa kodi maskini imepotea kwa mtindo huo?
 
Kwani uraiani nako watu wanamchukia Magufuli kama ilivyo kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Twitter na Ufipa?

Bado naamini Rais Magufuli alikuwa anaungwa mkono na idadi kubwa ya watu walio wengi.

Na watu hao walituma ujumbe wao kipindi cha msiba wake.

Ukiingia kule Twitter wamejazana kwa Msemaji wao Kigogo wanadanganyana tu. Instagram kule huwaambii kitu kuhusu JPM,Hamis Kigwangalah kauona moto wake. Pale kwa Millard Ayo chochote kinachomuhusu JPM kikipostiwa ndiyo utajua watu walikuwa wanampenda kiasi gani.
 
Back
Top Bottom