Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA'

Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA'

Umeoa mwanamke unajua ni mama wa nyumbani, asubuhi anakueleza mahitaji ya nyumbani unamwambia mke wangu fanya maarifa. Haya maarifa ni maarifa gani unayotaka mtoto wa watu ayafanye?
Maarifa ya kwenda kukopa kwa mangi[emoji30]
 
Tena mwanaume anasema mke wangu fanya maarifa ilhali anarudi jioni unakuta mke wako amepiga pilau ya kuku na soda juu. Mke Huyu hana kazi huulizi pesa ametoa wapi?
 
Vita ya uchumi ambayo huwa anasema raisi Ndio hiyo Kwani huwa hamuelewi?
Unaachiwa buku mezani utajiongeza mwenyewe ufanyeje ili tumeze
Ukikuta dagaa wa kuchemsha usilalamike mkeo hujui kupika
 
Tena mwanaume anasema mke wangu fanya maarifa in arudi jioni unakuta mke wako amepiga polaubya kuku na soda juu. Mke Huyu hana kazi huulizi pesa ametoa wapi?
Dah duniani kuna mambo na dume linakaa vizuri linakula asalaleeeeee
 
Ukikuta dagaa wa kuchemsha usilalamike mkeo hujui kupika
Hamnaga jema nyie wanawake! ukiachiwa kidogo malalamiko kibao,ukiachiwa nyingi hiyo hiyo unabana kweli ufanye matumizi yako yasiyo ya lazima......
 
Mi najua kuwajibika mama, usinitemee makohozi hayo
Hongera Hii inawahusu wasiowajibika,
Kuna jirani yangu hapa ana mtoto wa kiume, mwanaume ana mke mtoto lkn Bado anaishi kwao na anatega mkono kwa baba yake kuombq hela ya matumizi
 
Ndiyo "afanye maarifa" hii ni kauli ya kiungwana sana toka kwa baba wa familia.
Kauli hii inampa hamasa mama ajiongeze kidogo kwa siku hiyo katika jukumu la kuihudumia familia kama vile jinsi afanyavyo baba.

Kauli hii haimaanishi kwamba mama uende kinyume na misingi ya ndoa wala kutomheshimu mmeo, bali ni kama kupewa ruhusa ya uhusika mkuu wa kung'amua ni namna gani mama utafanya makarateka na kuumiza kichwa familia ile.

Kinacho takiwa hapo mama ni kuvaa uhusika wa usingle mother, yaani una pretend as if mumeo hayupo au katoweka duniani ghafla so unapambana kukabiliana na hiyo hali na mwisho wa siku watoto wanakula.

Solution kuu ni kwamba tunapo wapa hela za manunuzi ya mahitaji nyumbani, muwe na desturi ya kutumia kiasi nyingine una save kama dharura kwa baadae.

Pia unaweza kumfuata jirani mwanamke mwenzio mkafanya butter trade.
Unampa mchele yeye anakupa mkaa ama kibaba cha maharage na mjali wa mafuta.

Nafikiri nimekupa jibu mujaarab kabisa bibie Sky Eclat.
 
Maarifa ya kwamba akope akirud mwanaume alipe deni ndo inavokua japo haitakiw kua mara nyingi
Kwanini usiende kukopa ww!!! Mwanamke akakope kwa mwanaume siku akimla ulalame tusivyo waaminifu nyie nyie wakati mwingine dharau mnajitengenezea
 
Kuna zile tunazochomoaga bhanaa kwenye matumizi!!! Kuna kubanwa pia kwa mwanaume ila sio kila siku aseme fanya maarifa!!!!
 
Sio kila alieoa alijiandaa/kuelewa vyema majukumu yanayokuja na ndoa.
 
Back
Top Bottom