Kuna anguko kubwa sana la kujua kuandika sentensi na herufi sahihi za maneno miongoni mwetu Watanzania

Kuna anguko kubwa sana la kujua kuandika sentensi na herufi sahihi za maneno miongoni mwetu Watanzania

Anza na hapa hapa jf. Kiswahili chetu kinazidi kuwa kibovu. Yaani sisi ni shida kwa mfano vijana ukiwasikiliza utagundua wanachanganya kueleza na kuelekeza. Kuahirisha wenyewe wanaandika kuhairisha iko siku wataandika kuharisha. Tunahitaji kuwekeza kwenye kukuza na kufundisha Kiswahili.
Sio kuhairisha ❎

Usahihi ni kughairisha✅
 
Walianza kuandika sentensi kwa ufupi kwenye kuandikiana meseji kwenye simu, ufupisho wa kihuni, tukaona ni uvivu tu wa kuandika full sentence kumbe ni anguko la kutokujua kuandika sentensi vizuri
 
Wewe mwenyewe upo katikati ya huo ubovu wa mawasiliano kwa njia ya maandishi. Siyo herufi tu, hata matumizi ya alama za vituo kama; nukta, mkato, kiulizo, na nyinginezo.

Japokuwa umeeleza jambo kubwa sana kimsingi kama taifa tulishajikwaa na kuanguka, hatuwezi kuinuka tena.
 
Jamani hali ni mbaya sana, watu wanajua kuhesabu lakini kusoma na kuandika ni utapia kichwa, utapia ujinga unaangamiza taifa nyakati za sasa katika uga wa mawasiliano kwa njia ya maandishi, sms, chats etc.

Mungu aingilie kati hili anguko, naogopa sana tuko tuendako.

Ni hayo tu.

Wadiz

Mimi mwenyewe naona limekuwa tatizo kubwa sana..

Ntaanza kukurekebisha wewe kwanza

Utapia ujinga -Ninaamini kabisa lengo lako lilikuwa kuandika watu waliozidi ujinga yaani utapia akili..
utapia maana yake ni ukosefu wa ubora wa kitu kwa mfano utapia mlo ni ukosefu wa mlo bora ..
Hivyo basi ukisema utapia ujinga maana yake ni ukosefu wa ujinga maana mtu huyo atakuwa na akili sana

Nyakati za sasa tumia tu neno wakati wa sasa nyakati huweza kumaanisha miaka mingi sana kama generation au enzi kwa english tungesema (era) na kwa maelezo yako umesema shida imeanza siku za hivi karibuni kwa hiyo neno zuri ni wakati wa sasa

Naogopa sana tuko-
Nina hakika ulitaka kusema huko...

Hoja yako!

Swala la kwanza
hoja yako ina mashiko na Pana sana ila ilipaswa kuangalia Swala moja kubwa ambalo ni swala la lahaja..

Tanganyika na nchi ya East Africa (Kipindi cha ukoloni) kwa pamoja ilipata azimio na Kwa pamoja Walikubaliana kutumia Lahaja ya Kiunguja kama lahaja ya kiswahili Sanifu...

Lakini hii haikuwa kifo cha lahaja zingine kama kihadimu(Kimakunduchi) , kimrina (Inayopatikana pangani), kimgao,kipate ,kingozi kibajuni,kipemba,kivumba (Tanga) ,kimtangang'ata (Tanga) ,Kingazija na etc..

Ambazo nazo kwa ongezeko la watu hao zinakua kwa kasi hivyo kudhibiti matumizi ya lahaja zingine inabidi liwekwe azimio jingine la chaguzi ya lahaja kimaandishi na kimisemo...

Swala la pili

kiufupi ni kwamba kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake na wote wakawa sawa ni Vyema aongozwe na wale Wanaoweza kuona...

Miongoni mwa lahja mbovu kimaumbo na kimatamshi zinatoka Tanzania Bara..

Huku lahaja bora zikitoka pwani na Visiwani kwa mujibu huo ni wazi sasa Sifa mojawapo ya walimu kufundisha kiswahili isiwe ufaulu wa kukariri ila iwe ni Mmoja atokaye katika moja ya lahaja bora ikiwemo Kiunguja na kimakunduchi ili kuokoa taifa hili...
Maana yake Wale wote wenye lahaja hizi wahimizwe kufundisha kiswahili kuliko Kumkuta mwalimu wa kiswahili ni Msukuma au Mkurwa lazma kiswahili cha wanafunzi kiharibike ...

Asanteni
 
Nimeshangaa walimu nao wanaandika
  1. Alima wakimaanisha Halima
  2. Muagama wakimaanisha Mhagama
  3. Asumani wakimaanisha Athuman
  4. Mwanaamis wakimaanisha Mwanahamisi
  5. Alamisi wakimaanisha Alhamisi
  6. Maali wakimaanisha Mahali
  7. Maharifa wakimaanisha Maarifa
  8. Maangahiko wakimaanisha Mahangaiko
  9. Nisamee wakimaanisha Nisamehe
🤣🤣🤣
 
Yaani hapa kuwaelimisha herufi tu miaka 100
Je kutengeneza vitu na kubuni itakuwa 200 mingine
Bado tuko nyuma sana kwa kweli
Kuna think tank wetu wao wanaumiza vichwa ili watoto wawe wapumbavu mpaka wanakuwa
Na hao ndio wameshika nchi
Roho zao mbaya wanahakikisha nchi na watu wake wabaki masikini daima
Nauona ukweli katika hili. Kuna Wakati tulikuwa na Waziri wa Elimu, asiye na Elimu, hatari sana aisee.
 
Anza na hapa hapa jf. Kiswahili chetu kinazidi kuwa kibovu. Yaani sisi ni shida kwa mfano vijana ukiwasikiliza utagundua wanachanganya kueleza na kuelekeza. Kuahirisha wenyewe wanaandika kuhairisha iko siku wataandika kuharisha. Tunahitaji kuwekeza kwenye kukuza na kufundisha Kiswahili.
100% pure fact!
 
Jamani hali ni mbaya sana, watu wanajua kuhesabu lakini kusoma na kuandika ni utapia kichwa, utapia ujinga unaangamiza taifa nyakati za sasa katika uga wa mawasiliano kwa njia ya maandishi, sms, chats etc.

Sijui labda ni mimi tu naliona hili. Uandishi mbovu na makosa ya herufi sahihi kwenye maneno.

Mungu aingilie kati hili anguko, naogopa sana tuko tuendako.

Ni hayo tu.

Wadiz
Nimekutana na tangazo 'Ukikojoa faini 500,00/='
 
Jamani hali ni mbaya sana, watu wanajua kuhesabu lakini kusoma na kuandika ni utapia kichwa, utapia ujinga unaangamiza taifa nyakati za sasa katika uga wa mawasiliano kwa njia ya maandishi, sms, chats etc.

Sijui labda ni mimi tu naliona hili. Uandishi mbovu na makosa ya herufi sahihi kwenye maneno.

Mungu aingilie kati hili anguko, naogopa sana tuko tuendako.

Ni hayo tu.

Wadiz
Tatizo kubwa Sana,inashangaza wanachofundishwa huko shuleni
 
Jamani hali ni mbaya sana, watu wanajua kuhesabu lakini kusoma na kuandika ni utapia kichwa, utapia ujinga unaangamiza taifa nyakati za sasa katika uga wa mawasiliano kwa njia ya maandishi, sms, chats etc.

Sijui labda ni mimi tu naliona hili. Uandishi mbovu na makosa ya herufi sahihi kwenye maneno.

Mungu aingilie kati hili anguko, naogopa sana tuko tuendako.

Ni hayo tu.

Wadiz
Wakati mwingine unakuta anayeandika hivyo ni msomi kabisa! Inasikitisha kwa kweli!
 
Ndo hya ninayosema 🤣🤣
Mwendo wa lahaja tu
Kuahirisha hutamkwa na lahaja nyingi za bara na kughairisha hutamkwa na lahaja nyingi za pwani kama Kiunguja,Kimakunduchi, kipate n.k
Ni kughairi na si kuahiri,kuahiri si kiswahili
 
Back
Top Bottom