Kuna anguko kubwa sana la kujua kuandika sentensi na herufi sahihi za maneno miongoni mwetu Watanzania

Ndo hya ninayosema 🤣🤣
Mwendo wa lahaja tu
Kuahirisha hutamkwa na lahaja nyingi za bara na kughairisha hutamkwa na lahaja nyingi za pwani kama Kiunguja,Kimakunduchi, kipate n.k
Ni kughairi na si kuahiri,kuahiri si kiswahili
 
Nauona ukweli katika hili. Kuna Wakati tulikuwa na Waziri wa Elimu, asiye na Elimu, hatari sana aisee.
Nacheka kama mazuri
Wanasiasa wanaona bora watu wawe watumwa kuliko kuwa na maendeleo
Inauma sana unakuta watu wanapokea elfu 10 na kofia, unajiuliza hawa ni binadamu kweli au
Wamekuwa dhalili tangu wadogo
Sijui kama itakuja tokea top 10 ya matajiri ni Blacks never
 
Kama kiswahili ulipata d au c huna mamlakaaa ya kutuelekezaa lugha
 
Think Tanks ndio hawa wanaoruka sarakasi bungeni?
Wao hawajali kama kuna uchafu umeziba kila kona na kusababisha mafuriko, hawajali umeme upo au haupo, hawana Habari na mama mjamzito anaekufa bila uangalizi,
Hao ndio wanaosubiri hela zilizotolewa kwa kuisaidia nchi kugawana tena misaada ya elimu na Afya

Mungu awalaani
 
Kuna mmoja japo simjui lkn ilibidi nimpe za uso
Screenshot_20231021-130724_1.jpg
 
Ni kughairi na si kuahiri,kuahiri si kiswahili
Mkuu mimi Si Mwalimu wa kiswahili wala si Mtaalamu wa kiswahili ila ni vile tu nilimsikiliza mwalimu wangu miaka na mikaka imepita takribani 30 na pia mimi ni mkazi wa pwani..

Kama nilivyosema kuwa kuna utofauti wa kilahaja katika maneno hayo japo inaonyesha kuna haja ya watu kuelewa mstari uliopo katika utofauti baina ya lahaja na Lugha..

Kwenye lahaja kuna vitu vinaitwa vizinga sifa, na kuna aina zake nne kama sijasahau..

ila kwa leo acha nizungumzie mbili kulingana na hoja yako..Kuna vizinga sifa msamiati na vizinga sifa mofu unavyotakiwa wewe kuvielewa...

Vizinga sifa ni mstari au mpaka unaochorwa kuonyesha tofauti ya matamshi baina ya lahaja moja na nyingine..

Mfano vizinga sifa vya Msamiati : neno nyanya kwa lahaja nyingi za bara humaanisha kiungo cha chakula lakini kwa lahaja za unguja na visiwani wanaiita tungule.
hata hivyo kwa lahaja za kimvita na zingine huko kenya nyanya humaanisha bibi au mzazi wa baba yako au mama yako na bibi huita mke..

Katika vizinga sifa mofu (na hapa ndo kwenye hoja yako inayokuchangany hasa) kwa mfano neno likubalikalo kama nakuja/Nitakuja kwa kiswahili sanifu kama ilivyokubaliwa..

Ukienda katika lahaja za Tanga ,Zanzibar hutamkwa Naja,

na kwa lahaja ya pemba hutamkwa takuja na kwa lahaja ya kitumbatu hutamkwa sakuja

Sasa huwezi mwita Anayesema Sakuja au takuja au naja hajui kiswahili ila utachora mstari wa kujua yupo katika lahaja yake na ni bora kuiheshimu japo na yeye inabidi ajue kuwa anayeongea anatoka upande upi kama ni public ni bora akatumia lahaja inayokubalika...

sasa narudi kwenye hoja yako tena kwamba
ghairi ni lahaja ya Unguja japo kwa lahaja zingine wanatumia ahiri kutokana na matamshi na jinsi ya kuumba herufi ..

kwahyo ukimsikia mtu anasema nimeghairisha na atakayesema Nimeahirisha wote wako sawa ila lahaja ni tofauti na maneno haya hutumika yote inategemea uko maeneo gani..

na ndo maana kuna wengine husema Shughuri wengine shuhuri..wengine shuguli (siwalaumu kwa sababu ya lahaja walizokuwa nazo na pia walimu waliowafundisha)

ndo maana nikasema kikubwa kutokana ma muingiliano huwa wa lahaja nyingi zenye miundo tofuti kuna haja ya kuweka Gold standard lahaja moja itakayofundishwa nchi nzima...

na walimu wanaofundish kuiishi lahaja hiyo..
kwa mfano Mwalimu hawezi kuwa Msukuma kwenye kuelekeza atumie lugha ya kiswahili na kilichoandikwa kimeandikaa kwa lahaja ya kiunguja ila anavyoelezea ni kwa lahaaja ya kivumba lazma wazalishwe pijini wengi wa kilahaja na hilo ndo tatizo...

Na kitu ambacho nampongeza NYERERE ni Vijiji vya ujamaa Tungekuwa kama Kenya Kwa sasa kwani kuna baadhi ya sehemu wangejua sana Kiswahili ila wangine wangeongea kiswahili kibovu sana...
 
Kwenye nafsi ya kwanza na uwingi ,mofimu zinazotumika ni "ni" kwa nafsi ya kwanza umoja na "tu" kwa nafsi ya kwanza uwingi na sio "tw" kama unavyotaka kumaanisha wewe.

Mfano 1)Mimi ninasoma.Sisi tunasoma.
2)Mimi ninaimba. Sisi tunaimba.

3)Huku niendako. Huku tuendako.✅

Huku twendako❎
Mkuu wako sawa wanaosema twende na tuende
 
Mkuu mimi Si Mwalimu wa kiswahili wala si Mtaalamu wa kiswahili ila ni vile tu nilimsikiliza mwalimu wangu miaka na mikaka imepita takribani 30 na pia mimi ni mkazi wa pwani..

Kama nilivyosema kuwa kuna utofauti wa kilahaja katika maneno hayo japo inaonyesha kuna haja ya watu kuelewa mstari uliopo katika utofauti baina ya lahaja na Lugha..

Kwenye lahaja kuna vitu vinaitwa vizinga sifa, na kuna aina zake nne kama sijasahau..

ila kwa leo acha nizungumzie mbili kulingana na hoja yako..Kuna vizinga sifa msamiati na vizinga sifa mofu unavyotakiwa wewe kuvielewa...

Vizinga sifa ni mstari au mpaka unaochorwa kuonyesha tofauti ya matamshi baina ya lahaja moja na nyingine..

Mfano vizinga sifa vya Msamiati : neno nyanya kwa lahaja nyingi za bara humaanisha kiungo cha chakula lakini kwa lahaja za unguja na visiwani wanaiita tungule.
hata hivyo kwa lahaja za kimvita na zingine huko kenya nyanya humaanisha bibi au mzazi wa baba yako au mama yako na bibi huita mke..

Katika vizinga sifa mofu (na hapa ndo kwenye hoja yako inayokuchangany hasa) kwa mfano neno likubalikalo kama nakuja/Nitakuja kwa kiswahili sanifu kama ilivyokubaliwa..

Ukienda katika lahaja za Tanga ,Zanzibar hutamkwa Naja,

na kwa lahaja ya pemba hutamkwa takuja na kwa lahaja ya kitumbatu hutamkwa sakuja

Sasa huwezi mwita Anayesema Sakuja au takuja au naja hajui kiswahili ila utachora mstari wa kujua yupo katika lahaja yake na ni bora kuiheshimu japo na yeye inabidi ajue kuwa anayeongea anatoka upande upi kama ni public ni bora akatumia lahaja inayokubalika...

sasa narudi kwenye hoja yako tena kwamba
ghairi ni lahaja ya Unguja japo kwa lahaja zingine wanatumia ahiri kutokana na matamshi na jinsi ya kuumba herufi ..

kwahyo ukimsikia mtu anasema nimeghairisha na atakayesema Nimeahirisha wote wako sawa ila lahaja ni tofauti na maneno haya hutumika yote inategemea uko maeneo gani..

na ndo maana kuna wengine husema Shughuri wengine shuhuri..wengine shuguli (siwalaumu kwa sababu ya lahaja walizokuwa nazo na pia walimu waliowafundisha)

ndo maana nikasema kikubwa kutokana ma muingiliano huwa wa lahaja nyingi zenye miundo tofuti kuna haja ya kuweka Gold standard lahaja moja itakayofundishwa nchi nzima...

na walimu wanaofundish kuiishi lahaja hiyo..
kwa mfano Mwalimu hawezi kuwa Msukuma kwenye kuelekeza atumie lugha ya kiswahili na kilichoandikwa kimeandikaa kwa lahaja ya kiunguja ila anavyoelezea ni kwa lahaaja ya kivumba lazma wazalishwe pijini wengi wa kilahaja na hilo ndo tatizo...

Na kitu ambacho nampongeza NYERERE ni Vijiji vya ujamaa Tungekuwa kama Kenya Kwa sasa kwani kuna baadhi ya sehemu wangejua sana Kiswahili ila wangine wangeongea kiswahili kibovu sana...
Notes nyingi,Ila ni ghairi,neno la kiarabu lenye maana hiyo pia,ni ghorofa neno la kiarabu pia na si orofa au gorofa,nyanya na tungule ni maneno mawili tofauti yanayomaanisha kitu kimoja
 
Umesoma nilichoandika mkuu, soma ukielewe usisome kujibu..
Ungesoma mpaka mwisho ungeelewa kama sio kujua nilichomaanisha
 
Anza na hapa hapa jf. Kiswahili chetu kinazidi kuwa kibovu. Yaani sisi ni shida kwa mfano vijana ukiwasikiliza utagundua wanachanganya kueleza na kuelekeza. Kuahirisha wenyewe wanaandika kuhairisha iko siku wataandika kuharisha. Tunahitaji kuwekeza kwenye kukuza na kufundisha Kiswahili.
Chakusikitisha na kushangaza,huo ugonjwa upo mpaka kwenye baadhi ya magazeti na media zingine.
 
Back
Top Bottom