Ni kughairi na si kuahiri,kuahiri si kiswahili
Mkuu mimi Si Mwalimu wa kiswahili wala si Mtaalamu wa kiswahili ila ni vile tu nilimsikiliza mwalimu wangu miaka na mikaka imepita takribani 30 na pia mimi ni mkazi wa pwani..
Kama nilivyosema kuwa kuna utofauti wa kilahaja katika maneno hayo japo inaonyesha kuna haja ya watu kuelewa mstari uliopo katika utofauti baina ya lahaja na Lugha..
Kwenye lahaja kuna vitu vinaitwa
vizinga sifa, na kuna aina zake nne kama sijasahau..
ila kwa leo acha nizungumzie mbili kulingana na hoja yako..Kuna
vizinga sifa msamiati na
vizinga sifa mofu unavyotakiwa wewe kuvielewa...
Vizinga sifa ni mstari au mpaka unaochorwa kuonyesha tofauti ya matamshi baina ya lahaja moja na nyingine..
Mfano vizinga sifa vya Msamiati : neno
nyanya kwa lahaja nyingi za bara humaanisha kiungo cha chakula lakini kwa lahaja za unguja na visiwani wanaiita
tungule.
hata hivyo kwa lahaja za kimvita na zingine huko kenya
nyanya humaanisha
bibi au mzazi wa baba yako au mama yako na bibi huita mke..
Katika
vizinga sifa mofu (na hapa ndo kwenye hoja yako inayokuchangany hasa) kwa mfano neno likubalikalo kama nakuja/Nitakuja kwa kiswahili sanifu kama ilivyokubaliwa..
Ukienda katika lahaja za Tanga ,Zanzibar hutamkwa
Naja,
na kwa lahaja ya pemba hutamkwa
takuja na kwa lahaja ya kitumbatu hutamkwa
sakuja
Sasa huwezi mwita Anayesema Sakuja au takuja au naja hajui kiswahili ila utachora mstari wa kujua yupo katika lahaja yake na ni bora kuiheshimu japo na yeye inabidi ajue kuwa anayeongea anatoka upande upi kama ni public ni bora akatumia lahaja inayokubalika...
sasa narudi kwenye hoja yako tena kwamba
ghairi ni lahaja ya Unguja japo kwa lahaja zingine wanatumia
ahiri kutokana na matamshi na jinsi ya kuumba herufi ..
kwahyo ukimsikia mtu anasema
nimeghairisha na atakayesema
Nimeahirisha wote wako sawa ila lahaja ni tofauti na maneno haya hutumika yote inategemea uko maeneo gani..
na ndo maana kuna wengine husema Shughuri wengine shuhuri..wengine shuguli (siwalaumu kwa sababu ya lahaja walizokuwa nazo na pia walimu waliowafundisha)
ndo maana nikasema kikubwa kutokana ma muingiliano huwa wa lahaja nyingi zenye miundo tofuti kuna haja ya kuweka Gold standard lahaja moja itakayofundishwa nchi nzima...
na walimu wanaofundish kuiishi lahaja hiyo..
kwa mfano Mwalimu hawezi kuwa Msukuma kwenye kuelekeza atumie lugha ya kiswahili na kilichoandikwa kimeandikaa kwa lahaja ya kiunguja ila anavyoelezea ni kwa lahaaja ya kivumba lazma wazalishwe pijini wengi wa kilahaja na hilo ndo tatizo...
Na kitu ambacho nampongeza NYERERE ni Vijiji vya ujamaa Tungekuwa kama Kenya Kwa sasa kwani kuna baadhi ya sehemu wangejua sana Kiswahili ila wangine wangeongea kiswahili kibovu sana...