Kuna baadhi ya wazazi wanaishi kwa siri na maumivu makubwa. Wanatamani wawaombe watoto wao msamaha lakini hawajui waanzeje

Kiujumla adui akitaka kupiga taifa, anaanzia kwenye unit ya taifa ambayo ni familia. Case zote hapa ni vita ya uzao wa mwanamke. Laana ile iliyotolewa pale bustanini. Uzao unalengwa kila leo ndo maana mara divorces, kataa ndoa, machukizo ya uharibifu, madawa ya kulevya, and many more. Mungu aturehemu sana maana kama kuna moto kweli basi kitaumana sana siku hiyo. Wanawake kwa wanaume, wababa kwa wamama, wote tunayo hatia ya kutosimama katika kuwajibika irrespective of the situation.

Na kwa yanayoendelea saivi ya single parenting hasa kwa wanawake sijui itakuwaje. Na sio kwamba wanawake ni victims, labda 20% tu, wengi ni masterminds. Yote kwa yote, pray to God, wewe baba, mama, kaka, dada hata kama kumetokea nini, simama vizuri kumlea mtoto wako. Ila duniani saivi kuna michanganyo mweee, ee Bwana tusaidie πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½
 
Mkuu ni ubinafsi ndio uliutujaa, mwanaume anamuacha mwanamke na mtoto kwa changamoto za baba na mama mtoto anaingia kwenye huo moto wakati hausiki
Uko sahihi, lakini hata mwanamke anamkimbia mwanaume na kumuachia watoto/mtoto kutokana na sababu zake ikiwemo za kiuchumi.
 
Ipo hivyo mkuu ubinafsi unagharimu sana.
 
 
Mm ni kama ww ,ila Bora ww unaongea naye ,mm mzee wangu alinikataa full nkiwa mdogo nakumbuka nlienda kufuata ada ya shule na madaftar baada ya kuambiwa na kielekezwa kua ndiye babangu ,bas nkajkoki nkiwa mdogo shule ya msingi kwenda Kwa mzee Wang maana alikua mtumishi wa umma mwenye kuheshmika na ukizngatia nmerudishwa nyumban kisa ada na michango mingine ,sare Sina alaf nipo mguu peku ,nkafka kweny ofsi yake nlio elekezwa bwana wee alnkana na kunifukuza niondoke hapo haraka sana ,,nlitoka macho yamejaa machoz ,mpka na nyumban Kwa wajomba zangu, na nkakaa kmya na sijawai kumwambia mtu yeyote na sjawai kuangaika naye Tena, juz juz ndo nmeskia watu wanasema eti ana mtot mkubwa ambaye yupo sehem na ni kijana wake pendwa ambaye ndiye mm ,, nkabak nashangaa sana ,,, maana nna miaka Zaid ya 20 hatujaonana ,na kabla ya hapo tulikua hatuongeleshani kabsaa ,,nkimuona nlkua namkwepa maana ilkua inanijia Ile picha ya kilio nlichokua nalia sku ilee nliokwenda ofsin kwake ,,,
 
Mkuu umetupa jiwe gizani na limewapata wengi. Mada yako ni kama upanga ukatao kuwili. Kuna watenda na watendewa wote wameguswa. Asante kwa ujumbe unaogusa ndani ya moyo.
 
Vipi mmeyamaliza ?
 
Asante Mshana kwa mada yenye kufikirisha. Lakini, bila kuondoa ukweli na uhalisia wa kile ulichokieleza, nawiwa kueleza machache.

Kimsingi, maisha yamebadirika sana zama hizi ukilinganisha na zamani. Changamoto ambayo naiona kwa sasa tunapoangazia changamoto za familia au Jamii zetu, bado tumeendelea kuwaza na kuzungumza changamoto za miaka 47 iliyopita ambapo, Mwanaume ndiye alikuwa anahusika zaidi kama chanzo cha changamoto husika, kwa kiwango kikubwa. Bado hatuangalii uhalisia wa sasa.

Tukiacha mbali sababu ya Watoto kulelewa na Ndugu wengine ili Mzazi wa Kike aende kuolewa, naomba ifahamike kwamba, siku hizi Wanawake wengi wanaojiweza kifedha, wamekuwa chanzo cha kuwaweka mbali Wanaume na Watoto wao. Wanatumia kama fimbo ya kuwaadhibu Wanaume waliozaa nao baada ya mahusiano kushindwa kuendelea kwa sababu zozote zile. Na haya yanafanyika kwa msaada mkubwa wa Ndugu wa Mwanamke.

Rai yangu, wakati umefika sasa tuyaangalie mambo haya ya Familia na Jamii kwa ujumla, kwa uhalisia wake na kutenda Haki ipasavyo. Haki sawa, kwa namna inavyochukuliwa na kutekelezwa, inaharibu Ustawi wa Familia, Jamii na Kizazi cha Kiume. Mwanaume, kama Kiongozi wa Familia, hawezi kuwa sawa na Mwanamke anayemuongoza na mambo yakawa sawa.
 
Rai yangu, wakati umefika sasa tuyaangalie mambo haya ya Familia na Jamii kwa ujumla, kwa uhalisia wake na kutenda Haki ipasavyo. Haki sawa, kwa namna inavyochukuliwa na kutekelezwa, inaharibu Ustawi wa Familia, Jamii na Kizazi cha Kiume. Mwanaume, kama Kiongozi wa Familia, hawezi kuwa sawa na Mwanamke anayemuongoza na mambo yakawa sawa.πŸ’ͺπŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ“ŒπŸ”¨
 
Nimetoka kusema hiki kitu kwenye moja ya threads zangu, hatuwezi kuwa na kizazi cha ufeminia bila kuiangaiza taasisi ya familia.

Hapa lazima tuchague tunataka kipi. 50/50 au ustawi wa familia.
 
Mkuu ni ubinafsi ndio uliutujaa, mwanaume anamuacha mwanamke na mtoto kwa changamoto za baba na mama mtoto anaingia kwenye huo moto wakati hausiki
Na hasa wanaume ndio wa kulaumiwa ktk kadhia yote hii, mimi naamini, mwanaume hapaswi kumuacha mwanae aliemleta duniani akateseka kwa sababu yoyote ile! lije jua ije mvua..
 
Na hasa wanaume ndio wa kulaumiwa ktk kadhia yote hii, mimi naamini, mwanaume hapaswi kumuacha mwanae aliemleta duniani akateseka kwa sababu yoyote ile! lije jua ije mvua..
Uko sahihi hata kama mwanamke alikutegeshea mimba ili umuoe
 
Mshana Jr mimi nashukuru Mungu kwetu tulilelewa na wazazi wawili, japo mwaka huu tumempoteza baba yetu akiwa ameshazeeka, tumebakia na mama tu. Lakini tunashuhudia watoto wanaolelewa na mzazi mmoja wanavyoteseka.
 
Mshana Jr mimi nashukuru Mungu kwetu tulilelewa na wazazi wawili, japo mwaka huu tumempoteza baba yetu akiwa ameshazeeka, tumebakia na mama tu. Lakini tunashuhudia watoto wanaolelewa na mzazi mmoja wanavyoteseka.
Mmebahatika sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…