Kuna baadhi ya wazazi wanaishi kwa siri na maumivu makubwa. Wanatamani wawaombe watoto wao msamaha lakini hawajui waanzeje

Kuna baadhi ya wazazi wanaishi kwa siri na maumivu makubwa. Wanatamani wawaombe watoto wao msamaha lakini hawajui waanzeje

Kiujumla adui akitaka kupiga taifa, anaanzia kwenye unit ya taifa ambayo ni familia. Case zote hapa ni vita ya uzao wa mwanamke. Laana ile iliyotolewa pale bustanini. Uzao unalengwa kila leo ndo maana mara divorces, kataa ndoa, machukizo ya uharibifu, madawa ya kulevya, and many more. Mungu aturehemu sana maana kama kuna moto kweli basi kitaumana sana siku hiyo. Wanawake kwa wanaume, wababa kwa wamama, wote tunayo hatia ya kutosimama katika kuwajibika irrespective of the situation.

Na kwa yanayoendelea saivi ya single parenting hasa kwa wanawake sijui itakuwaje. Na sio kwamba wanawake ni victims, labda 20% tu, wengi ni masterminds. Yote kwa yote, pray to God, wewe baba, mama, kaka, dada hata kama kumetokea nini, simama vizuri kumlea mtoto wako. Ila duniani saivi kuna michanganyo mweee, ee Bwana tusaidie 🙏🏽🙏🏽🙏🏽
 
Good message.Kuna kisa kimoja cha ndugu yangu ambacho pia ni funzo kubwa hasa kwa maamuzi ya Kiutu uzima kwa ajili ya kesho ya watoto.Mke wa jamaa ni mtumishi mkubwa tu serikalini na jamaa alipotaka wakae kwa pamoja Kagoma katakata maana wako mikoa tofauti na uhamisho inawezekana.Alichoamua jamaa ni kuwa na watoto na anaowasomesha vizuri tu na akaapa hatooa mke mwingine atafia umoumo kwenye ndoa yake.Ukimuuliza anasema kwake watoto wana thamani kubwa kuliko mateso anayoitoa.Kumbe watoto wengi wanateseka kwa sababu ya ubinafsi wa wazazi wao.
Ipo hivyo mkuu ubinafsi unagharimu sana.
 
Hii imenigusa mno mno baba na mama walitengana nikiwa miaka 6 tukatengana na mama mim na mdogo wangu Sasa tuko na miaka 30 sijuag upendo wa mama miaka yote yupo ni kuongea Kwa sim mara chache miaka hata miwil au mitatu tusimuone Sina Ile bond na mama Sina Ile feeling kwamba Kuna mtu anaitwa mama sijui mapenz ya mama yakoje yaan sijui kma Kuna mtu ananielewa Kwa Sasa mama akikutafuta nikukuambia shida za hela na sio kwamba Hana lahasha hakuna story yoyote zaid ya hela yaan naweza kaa hata wiki nisimkumbuke yaan hayupo Kwa akili yangu kabis na kinyume chake ni kwel ,Mimi baba yangu alikataa Kabla hata sijazaliwa ,yaan nimeteseka sana aisee ,yaan maisha yangu yamejaa Siri kubwa na nkisema watu watabaki mdomo wazi ,nna Hakka Kwa maisha na mateso nlio wai pitia Kuna uwezekano nkaingia kweny kitabu Cha rekodi za dunia ,am very serious with this ,,
 
Ni miaka 40 sasa sijaonana na mzee,najua alipo na tunawasiliana,siku ntakayonana nae ana kwa ana sidhani kama itakuwa siku yenye furaha, maana kuna maswali mengi sana ntataka anijibu.
Nahisi tutaishia kugombana ingawa sina nachohitaji kutoka kwake, nina hasira nae sana,kulelewa na mzazi mmoja wakati mzazi mwingine yupo inaumiza sana.
I will be like... " eeeh mzee ...what happened?".
Ntamuwashia moto asiponipa majibu ya kueleweka. Nina dukuduku sana, sipendi kumuuliza kwa njia ya simu nataka anijibu tukiwa tunaangaliana usoni.
Mm ni kama ww ,ila Bora ww unaongea naye ,mm mzee wangu alinikataa full nkiwa mdogo nakumbuka nlienda kufuata ada ya shule na madaftar baada ya kuambiwa na kielekezwa kua ndiye babangu ,bas nkajkoki nkiwa mdogo shule ya msingi kwenda Kwa mzee Wang maana alikua mtumishi wa umma mwenye kuheshmika na ukizngatia nmerudishwa nyumban kisa ada na michango mingine ,sare Sina alaf nipo mguu peku ,nkafka kweny ofsi yake nlio elekezwa bwana wee alnkana na kunifukuza niondoke hapo haraka sana ,,nlitoka macho yamejaa machoz ,mpka na nyumban Kwa wajomba zangu, na nkakaa kmya na sijawai kumwambia mtu yeyote na sjawai kuangaika naye Tena, juz juz ndo nmeskia watu wanasema eti ana mtot mkubwa ambaye yupo sehem na ni kijana wake pendwa ambaye ndiye mm ,, nkabak nashangaa sana ,,, maana nna miaka Zaid ya 20 hatujaonana ,na kabla ya hapo tulikua hatuongeleshani kabsaa ,,nkimuona nlkua namkwepa maana ilkua inanijia Ile picha ya kilio nlichokua nalia sku ilee nliokwenda ofsin kwake ,,,
 
Ni mpaka uishi hayo maisha ndio unaweza kupata hisia halisi za hii mada.

Hapa nazungumzia wale wazazi kwa sababu zozote zile waliwatelekeza watoto wao udogoni na kuja kuonana nao ukubwani.

Hapa nazungumzia wale wazazi ambao walitengena kwa sababu zozote zile na watoto kulelewa na mzazi mmoja ama mzazi wa kufikia.. Mzazi wa kambo.

Kuna unafuu kidogo kama huyo mtoto/watoto huko wanakolelewa wakapata mapenzi kama ya mzazi halisi. Kuna wachache wana hiyo bahati. Wengi wameambulia mateso, masimango na shida za kila aina
Kuna wazazi wa kike walipata ujauzito wakiwa shuleni..wakaacha masomo na kulea mimba na hatimaye kujifungua salama.

Baadhi walitaka kurudi na kuendelea na masomo hivyo kuwaachia ndugu zao walee mtoto mara nyingi ni mama dada au shangazi.

Makuzi ya mtoto katika umri wa awali ni muhimu sana kupata mapenzi ya wazazi wote wawili.. Mmoja ama wote wakiyumba mapenzi hayo huhamishiwa kwa walezi wanaowalea.

Kuna wazazi ambao walitengena wakiwa kwenye ndoa na watoto na baada ya hapo wakapata wenza wapya! Hapo watoto wanaenda kuanza maisha mapya mageni kwa mama/baba wa kufikia

Kuna tofauti kubwa sana kati mzazi halisi na mzazi wa kufikia.. Daima kuna kitu kitapungua. Kuna baadhi ya wazazi ambao walipata watoto kabla ya ndoa na sasa wakapata watu wa ndoa, hapo wengi waliwaacha watoto kwa ndugu ili wao wakajenge ndoa zao.

Kuna wazazi waliwatelekeza watoto kwa ndugu na wao kupotea kwenda kutafuta maisha. Scenario ni nyingi lakini mwisho wa siku watoto huwa wakubwa na kuja kukutana na wazazi wao halisi(kwa wale wenye bahati hiyo)

Hapo watoto huwa na maswali mengi sana ambayo wengi huwa hawayaulizi.. Na wazazi nao huwa na maelezo mengi sana lakini hawajui waanzie wapi. Ukaribu kati ya wawili hawa huwa hauna strong bonds.

Matokeo yake ni watoto kuwa na vinyongo na wazazi wao.. Huku wazazi wakiwa na maumivu ya ndani, wakitamani wajieleze na kuomba msamaha lakini hawajui waanzie wapi

Zile nyakati za shule wakati watoto wakifuatwa na wazazi wao. Zile nyakati za shule watoto wanaposimuliana furaha za nyumbani na wazazi wao. Kuna ambao hawana cha kusimulia na hubaki na maumivu na maswali mengi.. Huku nao wakitamani wangekuwa na wazazi wao.

Ni afadhali waambie wajue kwamba wazazi wamekufa kuliko waambiwe wapo Hai

Mifano ni mingi hata hapa JF..!
Mkuu umetupa jiwe gizani na limewapata wengi. Mada yako ni kama upanga ukatao kuwili. Kuna watenda na watendewa wote wameguswa. Asante kwa ujumbe unaogusa ndani ya moyo.
 
Mm ni kama ww ,ila Bora ww unaongea naye ,mm mzee wangu alinikataa full nkiwa mdogo nakumbuka nlienda kufuata ada ya shule na madaftar baada ya kuambiwa na kielekezwa kua ndiye babangu ,bas nkajkoki nkiwa mdogo shule ya msingi kwenda Kwa mzee Wang maana alikua mtumishi wa umma mwenye kuheshmika na ukizngatia nmerudishwa nyumban kisa ada na michango mingine ,sare Sina alaf nipo mguu peku ,nkafka kweny ofsi yake nlio elekezwa bwana wee alnkana na kunifukuza niondoke hapo haraka sana ,,nlitoka macho yamejaa machoz ,mpka na nyumban Kwa wajomba zangu, na nkakaa kmya na sijawai kumwambia mtu yeyote na sjawai kuangaika naye Tena, juz juz ndo nmeskia watu wanasema eti ana mtot mkubwa ambaye yupo sehem na ni kijana wake pendwa ambaye ndiye mm ,, nkabak nashangaa sana ,,, maana nna miaka Zaid ya 20 hatujaonana ,na kabla ya hapo tulikua hatuongeleshani kabsaa ,,nkimuona nlkua namkwepa maana ilkua inanijia Ile picha ya kilio nlichokua nalia sku ilee nliokwenda ofsin kwake ,,,
Vipi mmeyamaliza ?
 
Asante Mshana kwa mada yenye kufikirisha. Lakini, bila kuondoa ukweli na uhalisia wa kile ulichokieleza, nawiwa kueleza machache.

Kimsingi, maisha yamebadirika sana zama hizi ukilinganisha na zamani. Changamoto ambayo naiona kwa sasa tunapoangazia changamoto za familia au Jamii zetu, bado tumeendelea kuwaza na kuzungumza changamoto za miaka 47 iliyopita ambapo, Mwanaume ndiye alikuwa anahusika zaidi kama chanzo cha changamoto husika, kwa kiwango kikubwa. Bado hatuangalii uhalisia wa sasa.

Tukiacha mbali sababu ya Watoto kulelewa na Ndugu wengine ili Mzazi wa Kike aende kuolewa, naomba ifahamike kwamba, siku hizi Wanawake wengi wanaojiweza kifedha, wamekuwa chanzo cha kuwaweka mbali Wanaume na Watoto wao. Wanatumia kama fimbo ya kuwaadhibu Wanaume waliozaa nao baada ya mahusiano kushindwa kuendelea kwa sababu zozote zile. Na haya yanafanyika kwa msaada mkubwa wa Ndugu wa Mwanamke.

Rai yangu, wakati umefika sasa tuyaangalie mambo haya ya Familia na Jamii kwa ujumla, kwa uhalisia wake na kutenda Haki ipasavyo. Haki sawa, kwa namna inavyochukuliwa na kutekelezwa, inaharibu Ustawi wa Familia, Jamii na Kizazi cha Kiume. Mwanaume, kama Kiongozi wa Familia, hawezi kuwa sawa na Mwanamke anayemuongoza na mambo yakawa sawa.
 
Rai yangu, wakati umefika sasa tuyaangalie mambo haya ya Familia na Jamii kwa ujumla, kwa uhalisia wake na kutenda Haki ipasavyo. Haki sawa, kwa namna inavyochukuliwa na kutekelezwa, inaharibu Ustawi wa Familia, Jamii na Kizazi cha Kiume. Mwanaume, kama Kiongozi wa Familia, hawezi kuwa sawa na Mwanamke anayemuongoza na mambo yakawa sawa.💪🏿🙏🏿🙏🏿📌🔨
 
Nimetoka kusema hiki kitu kwenye moja ya threads zangu, hatuwezi kuwa na kizazi cha ufeminia bila kuiangaiza taasisi ya familia.

Hapa lazima tuchague tunataka kipi. 50/50 au ustawi wa familia.
 
Mkuu ni ubinafsi ndio uliutujaa, mwanaume anamuacha mwanamke na mtoto kwa changamoto za baba na mama mtoto anaingia kwenye huo moto wakati hausiki
Na hasa wanaume ndio wa kulaumiwa ktk kadhia yote hii, mimi naamini, mwanaume hapaswi kumuacha mwanae aliemleta duniani akateseka kwa sababu yoyote ile! lije jua ije mvua..
 
Na hasa wanaume ndio wa kulaumiwa ktk kadhia yote hii, mimi naamini, mwanaume hapaswi kumuacha mwanae aliemleta duniani akateseka kwa sababu yoyote ile! lije jua ije mvua..
Uko sahihi hata kama mwanamke alikutegeshea mimba ili umuoe
 
Mshana Jr mimi nashukuru Mungu kwetu tulilelewa na wazazi wawili, japo mwaka huu tumempoteza baba yetu akiwa ameshazeeka, tumebakia na mama tu. Lakini tunashuhudia watoto wanaolelewa na mzazi mmoja wanavyoteseka.
 
Mmebahatika sana
 
Back
Top Bottom