Kuna baadhi ya wazazi wanaishi kwa siri na maumivu makubwa. Wanatamani wawaombe watoto wao msamaha lakini hawajui waanzeje

Kuna baadhi ya wazazi wanaishi kwa siri na maumivu makubwa. Wanatamani wawaombe watoto wao msamaha lakini hawajui waanzeje

Dah nimeandika comment ndefuu ya kufarijiana lkn nimefuta nimeiona kama haifai, ila tunapaswa kujua tunaishi kwenye Dunia inayo chukua njia yake kutokana na asili we can't change our fate(Sijui niiwekeje hii ili nieleweke). Samehe maisha yaendelee, ngoja niishie hapa japo Nina mengi ya kusema.
 
Aisee Mkuu natamani kuonana na Wewe still na face some trials nashukuru kuna dogo alinipa namba yako naweza kukucheki next week kuna mambo fulani naweza nikapata connection ili kufanikisha
Karibu sana sana siku hizi sipo Kilingeni Msata tena nipo mjini karibu na lile jumba jeupe😀
 
Dah nimeandika comment ndefuu ya kufarijiana lkn nimefuta nimeiona kama haifai, ila tunapaswa kujua tunaishi kwenye Dunia inayo chukua njia yake kutokana na asili we can't change our fate(Sijui niiwekeje hii ili nieleweke). Samehe maisha yaendelee, ngoja niishie hapa japo Nina mengi ya kusema.
Andika kadiri uwezavyo.. Kuna tiba ya ajabu kwenye maandishi hasa kiroho
 
Ni mpaka uishi hayo maisha ndio unaweza kupata hisia halisi za hii mada
Hapa nazungumzia wale wazazi kwa sababu zozote zile waliwatelekeza watoto wao udogoni na kuja kuonana nao ukubwani
Hapa nazungumzia wale wazazi ambao walitengena kwa sababu zozote zile na watoto kulelewa na mzazi mmoja ama mzazi wa kufikia.. Mzazi wa kambo
Kuna unafuu kidogo kama huyo mtoto/watoto huko wanakolelewa wakapata mapenzi kama ya mzazi halisi.. Kuna wachache wana hiyo bahati.. Wengi wameambulia mateso, masimango na shida za kila aina
Kuna wazazi wa kike walipata ujauzito wakiwa shuleni..wakaacha masomo na kulea mimba na hatimaye kujifungua salama.. Baadhi walitaka kurudi na kuendelea na masomo hivyo kuwaachia ndugu zao walee mtoto ...maranyingi ni mama dada au shangazi
Makuzi ya mtoto katika umri wa awali ni muhimu sana kupata mapenzi ya wazazi wote wawili.. Mmoja ama wote wakiyumba mapenzi hayo huhamishiwa kwa walezi wanaowalea
Kuna wazazi ambao walitengena wakiwa kwenye ndoa na watoto na baada ya hapo wakapata wenza wapya! Hapo watoto wanaenda kuanza maisha mapya mageni kwa mama/baba wa kufikia

Kuna tofauti kubwa sana kati mzazi halisi na mzazi wa kufikia.. Daima kuna kitu kitapungua
Kuna baadhi ya wazazi ambao walipata watoto kabla ya ndoa na sasa wakapata watu wa ndoa, hapo wengi waliwaacha watoto kwa ndugu ili wao wakajenge ndoa zao
Kuna wazazi waliwatelekeza watoto kwa ndugu na wao kupotea kwenda kutafuta maisha
Scenario ni nyingi lakini mwisho wa siku watoto huwa wakubwa na kuja kukutana na wazazi wao halisi(kwa wale wenye bahati hiyo)
Hapo watoto huwa na maswali mengi sana ambayo wengi huwa hawayaulizi.. Na wazazi nao huwa na maelezo mengi sana lakini hawajui waanzie wapi
Ukaribu kati ya wawili hawa huwa hauna strong bonds.. Matokeo yake ni watoto kuwa na vinyongo na wazazi wao.. Huku wazazi wakiwa na maumivu ya ndani, wakitamani wajieleze na kuomba msamaha lakini hawajui waanzie wapi

Zile nyakati za shule wakati watoto wakifuatwa na wazazi wao
Zile nyakati za shule watoto wanaposimuliana furaha za nyumbani na wazazi wao.. Kuna ambao hawana cha kusimulia na hubaki na maumivu na maswali mengi.. Huku nao wakitamani wangekuwa na wazazi wao..
Ni afadhali waambie wajue kwamba wazazi wamekufa kuliko waambiwe wapo Hai

Mifano ni mingi hata hapa JF..!
Sahihi kabisa
 
Karibu sana sana siku hizi sipo Kilingeni Msata tena nipo mjini karibu na lile jumba jeupe😀
Sio mambo ya Kilingeni Mkuu, nadhani unaweza ukanisaidia mahala fulani ili kupata connection fulani namba ninayo yako nitakucheki tu
 
Habari mbaya ni kuwa kuna uwezekano wa kuendeleza cheni ya utelekezaji kama ulitelekezwa. Ni rahisi aliyetelekezwa kutelekeza kuliko ambaye hakutelekezwa, isipokuwa kwa wale waliotambua trauma zao na kuamua kupona na kurekebisha kwaajili ya wengine.

Kuna vitu tunasema ile koo ina laana, si kweli kuwa ni laana bali ni trauma response zinazotengeneza tabia za kufanana kati ya wahusika na tabia zao kupelekea matokeo yakufanana.

Most of broken people wanatokea kwenye broken families. Get healed before starts a family.

Many of us carries down our issues to our children rather than addressing them and rise our kids better than we were raised.
 
Habari mbaya ni kuwa kuna uwezekano wa kuendeleza cheni ya utelekezaji kama ulitelekezwa. Ni rahisi aliyetelekezwa kutelekeza kuliko ambaye hakutelekezwa, isipokuwa kwa wale waliotambua trauma zao na kuamua kupona na kurekebisha kwaajili ya wengine.

Kuna vitu tunasema ile koo ina laana, si kweli kuwa ni laana bali ni trauma response zinazotengeneza tabia za kufanana kati ya wahusika na tabia zao kupelekea matokeo yakufanana.

Most of broken people wanatokea kwenye broken families. Get healed before starts a family.
 
Bush Dokta
Mshana Jr
Pitieni hapo kwenye huu uzi mtaona na kama mna uwezo wa kuangalia mambo kwa jicho la tatu mtaona how hardly I survived to gain the momentum mpaka kufikia hapa nilipo leo

Thread 'Maisha sio kulalamika, ni kupambana tu...' https://www.jamiiforums.com/threads/maisha-sio-kulalamika-ni-kupambana-tu.2108610/

Post # 18 kwenye huu uzi ni ya jamaa niliyesoma naye Primary mpaka Sekondari tukaja kuachana baadaye lakini bado baadae tukakutane tena kwenye mizunguko na maisha yangu yalivyokuwa sio maigizo.
Manyanza hii link haifunguki mkuu
 
Aisee Mkuu natamani kuonana na Wewe still na face some trials nashukuru kuna dogo alinipa namba yako naweza kukucheki next week kuna mambo fulani naweza nikapata connection ili kufanikisha
Nimefanikiwa kuisoma ile mada jitahidi tuwasiliane
 
Ni miaka 40 sasa sijaonana na mzee,najua alipo na tunawasiliana,siku ntakayonana nae ana kwa ana sidhani kama itakuwa siku yenye furaha, maana kuna maswali mengi sana ntataka anijibu.
Nahisi tutaishia kugombana ingawa sina nachohitaji kutoka kwake, nina hasira nae sana,kulelewa na mzazi mmoja wakati mzazi mwingine yupo inaumiza sana.
I will be like... " eeeh mzee ...what happened?".
Ntamuwashia moto asiponipa majibu ya kueleweka. Nina dukuduku sana, sipendi kumuuliza kwa njia ya simu nataka anijibu tukiwa tunaangaliana usoni.
Mzee wako utakua unamuonea bure, unaweza kuta chanzo cha matatizo yote ni Mama yako, sasa bora.ukae chini na mama yako akupe ukweli wote!!
 
Hii imenigusa mno mno baba na mama walitengana nikiwa miaka 6 tukatengana na mama mim na mdogo wangu Sasa tuko na miaka 30 sijuag upendo wa mama miaka yote yupo ni kuongea Kwa sim mara chache miaka hata miwil au mitatu tusimuone Sina Ile bond na mama Sina Ile feeling kwamba Kuna mtu anaitwa mama sijui mapenz ya mama yakoje yaan sijui kma Kuna mtu ananielewa Kwa Sasa mama akikutafuta nikukuambia shida za hela na sio kwamba Hana lahasha hakuna story yoyote zaid ya hela yaan naweza kaa hata wiki nisimkumbuke yaan hayupo Kwa akili yangu kabisa
Piga chini Haina haja ya kuwa na mahusiano na mtu asiye kupenda yeye anapenda pesa tu
 
Wahi kamsalimie kabla hajanyamaza ukajilaumu!!

Usiishie kulaumu wazee kina mama wanazingua sana haha maisha!!
Wanawake ndiyo chanzo sema wengi wanaficha, mi nina kijana mkubwa tu kaletwa ukubwani eti anataka kujua kwa nini sikuwepo katika maisha yake ya ukuwaji!? Mi mbele ya Mama yake nikamwambia hilo swali jibu lake analo Mama yako, nikamwambia haya Mama mjibu mwanao, kweli Mama mtu akajibu kua yule Baba aliyemlea alijipendekeza na maokoto kwake ikabidi na mimba ampee yule baba mwenye maokoto, na kipindi hicho mi bado niko shule sina mipango,Mama mtu ndiyo akaamua kunitosa na kuambatana na jamaa mwenye maokoto! Sasa mimi kama Baba mzazi hapo nina makosa gani ikiwa umasikini wangu ndiyo ulifanya hadi nikafichwa mtoto wangu!!? Kijana alibaki kimya hana la kusema zaidi ya kusema lakini Mama wwe ndiyo mwenye makosa, Baba wala hana makosa! Ila nikamwambia kijana kua hata Mama yako hana makosa, maana alipambana ili wwe ukuwe kwenye maisha bora,kwa hiyo usimlaumu sana!!
 
Kuna unafuu kidogo kama huyo mtoto/watoto huko wanakolelewa wakapata mapenzi kama ya mzazi halisi
Nakazia!

Mama wadogo wanatusimanga mimi na mke wangu eti kwa vile alikuja kwangu akiwa na mtoto mdogo! Nimewaambia waishie huko huko na ujinga wao maana na wenyewe siyo wasafi kama wanavyotaka kutudangaanya!
 
Back
Top Bottom