Kuna haja ya Tundu Lissu kuandaliwa kuiondoa CCM 2025 madarakani?

Hivi hakuna mtu mwingine wa kuleta mabadiliko zaidi ya huyo mkimbizi?
Mbona wanaharakati wa mapinduzi wako wengi tu! Tena watatoka ndani ya CCM, trust me!

CCM haina wanaharakati wa mapinduzi bali kuna majizi ya kura na watu wa kujikomba. Watu wanaotegemea vyombo vya dola tu kufanya siasa wana jeuri gani?
 
Kumbuka CDM Haina utamaduni wa kurudia mgombea.

Pia KATIBA mpya na Tume huru vikipatikana kabla ya uchaguzi wowote, tutapunguza tatizo la kutegemea watu Badala ya kutegemea mifumo imara ya kiongozi.

Ameeeen
 
Kwamba CCM imeoza, bt Sa100 yupo fresh kabisa!!!!! Rudi shule.
 
Wewe jamaa mkoa wako hauna miundombinu na huduma mhimu hospital, barabara, vituo vya afya kuanzia kantaramba,iyula mpaka igamba wilaya yako ya mbozi mpaka chunya hakna hospitali,hata barabara ya lami hakuna, lakini huoni umuhimu wa Mabadiliko .maji hakuna, ukifika pale Tunduma toka Uhuru hakuna maji ni matope tu..Watu mnakua mumelogwa walahi!!
 
Hivi wewe unatuonaje lakini? Yani nchi nzima kabisa tukose watu wenye akili timamu wa kuwachagua mpaka tumpe lisu urais? Labda mtuloge kwanza!
 
Lissu urais hafai na hauwezi....

Lissu anafaa kuwa waziri mkuu ili kichwa kikipata moto sana kuwe na mtu juu yake wa kumdhibiti.
 
Nchi hii haina upungufu wa watu wenye uwezo wa kuongoza kwa ufanisi, ni wengi sana. Bali kinachokosekana ni Katiba bora tuu.
 
Inaonesha wewe huna shida na CCM, ila huwapendi baadhi ya viongozi wa CCM.
Ndio maana unamtaka TUNDU LISSU.
KIFUPI: Sioni mabadiliko ya kuitoa CCM Madarakani kwa sasa hivi( Labda itokee external force, kama ilivyotokea LIBYA).
 
Hivi hakuna mtu mwingine wa kuleta mabadiliko zaidi ya huyo mkimbizi?
Mbona wanaharakati wa mapinduzi wako wengi tu! Tena watatoka ndani ya CCM, trust me!
Utakuwa huna uzazi kabisa wewe dada.
Unathubutu kumuita Lissu mkimbizi?
Mtu aliyemwaga damu yake kwa kitetea wanyonge?.

Nchi hii tangu uhuru hajatokea mtetezi jasiri kama Lissu.
 
Hivi nyie sijui huwa mnawaza takataka gani Tundu Lissu agombee urais ashinde? Huyo chizi akisimama na Samia kihalali kabisa samia anachukua mapema tu.Upinzani mjifunze kusimamisha watu wenye haiba ya uongozi siyo hawa wanaharakati wa ovyo,walivyo na akili matope wanaweza msimamisha hata Fatma Karume au Mange Kimambi au yule mtoto wa Sarungi. Hawa achaneni nao kabisa bora hata Peter msigwa ila isiwe Mbowe wala Heche mtapoteza mapema tu
 
Magufuli hakuwa mwanaharakati au "kichaa"? Alikua na haiba au lugha ya kiuongozi? Mbona alikua Rais?. Ndio maana mtoa mada kasema aandaliwe, uchaguzi ukiwa huru hata CHADEMA ikimsimamisha Dereva BodaBoda Samia anaangushwa!! She's not that popular hasa bara so hizo ni kura za bure kwa CHADEMA come 2025!!
 
Watu wa Deep State wabadilike wawe kama wa Kenya ni wazalendo kwa Nchi yao.

Uchaguzi wa kenya uwe chachu system za ccm ziamke.

We need to step up. Dunia inakimbia sisi tunatembea bado na mabakuli ya kuomba misaada ya matundu ya choo.
 
CCM wote wamechafuka ni ngumu kuleta mabadiliko ya kweli, Lissu Hana makando kando ya ufisadi so ni rahisi kukemea madudu ya CCM.
Lissu ameeendelea kuwa mtu bora sana wakati woote.

Ni ngumu sana mtu mchafu kukemea machafu akakubalika.

Tunamhitaji Mr Clean, Mr Haki, Mr Maendeleo. Tundu Antiphas Lissu.
 
Tunamhitaji Mr Clean, Mr Haki, Mr Maendeleo. Tundu Antiphas Lissu.
 
Nondo za Maria Salungi inaonekana zinakutesa sana.

Bahati Mbaya huyo.Mange usiye mpenda ndiye alipewa Fursa ya Front Space kumpokea Rais Samia Marekani.

Kama unachukia jinyonge.

We jamaa usidhani Tanzania inajiendea endea tu kwa mihemko yako hiyo.
 
Inaonesha wewe huna shida na CCM, ila huwapendi baadhi ya viongozi wa CCM.
Ndio maana unamtaka TUNDU LISSU.
KIFUPI: Sioni mabadiliko ya kuitoa CCM Madarakani kwa sasa hivi( Labda itokee external force, kama ilivyotokea LIBYA).
Ccm is wholy rotten
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…