Kuna kazi wanaozifanya sijawahi kuelewa huwa wanaishi vipi

Wanasema biashara ni rahisi ukiwa unasimuliwa.

Ingia mzigoni mwenyewe ndio utajua uhalisia ulivyo.
 
Hao ni TISS
 
Maisha ni vile Ambavyo wewe utakavyo Yapa maana

Mwenzio anaweza kuishi kwenye chumba kimoja Na akala zake wali maharage and still akafurahia maisha , na ikawa Hana muda wakuwaza kabisa suala la kuwa na Mansion Wala gari hata la mtumba la ML 6, so maisha ni vile Ambavyo wewe utakavyo Yapa maana katika Psychology Yako ,

Ni sawa na namna ambavyo sisi tunavyoweza kuwashangaa wahadzabe na life style Yao wakati huo huo unaweza kukuta na wao wana tushangaa sisi na life style yetu huwenda wana Shangaa kwanini tuna Hangaika kufanya mambo mengi ya kuishi katika Dunia ya usasa wakati Maisha duniani tunapita tu
 
Mtu anayetembeza bidhaa au anayeuza bidhaa anaweza kupata kipato cha wastani cha watanzania wote. ,, tsh 300,000+ halafu ngoja ni kuulize mkuu hivi unajua kipato cha watanzania 90% ni chini ya laki tano kwa mwezi? Mbona wanaishi 🤣
Wastani wa pato la Mtanzania kwa mwezi ni laki mbili na nusu, huo ni wastani kwa hiyo kuna wengine wanapata zaidi na wengine wanapata kidogo. Nina uhakika Kuna watembeza bidhaa wengi kwa siku wanaambulia elfu tano tu.
 
Sio rahisi kama unavyosema wewe.
 
Makuli kushusha gunia la kiaz buku semi ina gunia 300 wanakuwa wanne kwa siku wanapiga had semitrael 2 jion kila mmoja anarud na ka 70 mtaji nguvu vp wewe wa mshahara laki 8 unaeza mfikia sema wanamatumiz makubwa hasa ya starehe
 
Ice cream za Bakhresa zinauzwa 250/300 wao wanauza 500 MTU akiuza dell zima box zake mbili ama 3 ana zaidi ya 20,000 faida, hela kubwa kushinda mwalimu.

Machinga wengi wanapata hela ndefu hasa hao wa mjini, sasa hivi wao ndio wanaongoza kwa retail maduka mengi yamebaki jumla.

Kuna wabeba mizigo wanafunga zaidi ya laki kwa siku, right area na connection ni biashara moja nzuri kushinda hata maofisa wa juu wa Wizara ama Taasisi kubwa hapa Mjini.

Kijana yoyote wa mjini anajua hizo KAZI watu wengi wanatoboa.
 
Tusidanganyane, hakuna binadamu anayeweza kuridhika katika hali hiyo ya maisha, hapo akiumwa serious hata siku moja tu ni maafa matupu.
 
Tusidanganyane, hakuna binadamu anayeweza kuridhika katika hali hiyo ya maisha, hapo akiumwa serious hata siku moja tu ni maafa matupu.
Wewe ndiye unayesema hivyo Sasa , Kuna watu hata kazi za maana hawafanyi wanaishi kwenye nyumba zao za urithi na wanatafuta Hela za kula tu unalijua Hilo kwanza !? Muda wa kuwaza mambo makubwa hawana
 
Ujenge mjengo mkali kwa kuuza vipande vya tikiti tu?

Maishaaaaaa!!!

Labda kama kuna biashara zingine wanaficha na hawataki kuzisema hadharani.
Yes, Hapa kkoo kuna watu wanapata hayo matunda, sahani buku wanawekwa kwenye vifungashio vya take away na vijiti vya meno.

1. Uchafu wao wanajaza mapipa matatu ama zaidi, siku wasipopita watu wa takataka mtaa haupitiki.

2. Matunda wanauza sahani kwa mamia kama sio maelfu, MTU kufunga faida laki kadhaa kwa siku Jambo la kawaida kabisa.

3. Nenda mwenyewe Kariakoo pita Mitaa kama Swahili na mchikichi ama Swahili na Agrey wamejaa kibao kaa kama nusu saa hesabu wameuza plate ngapi, then Rudi jukwaani ubishe tena.
 
Infro we hukubaliani na kila kitu kwenye ulimwengu huu😆
Unajua hizi hearsay za kusimuliwa tu, hazina uthibitisho.

Hakuna anayeleta experience yake mwenyewe ya hizi biashara.

Kila mtu analeta stori za kuambiwa na kusimuliwa tu.

Mara, Kuna jamaa anauza tikiti tu, katoboa, kuna jamaa anauza ice cream tu, kuna jamaa anatembeza nguo tu.

Sasa hizi ni stori za kusimuliwa tu, inabidi mtu ambaye ametajirika na mwenye experience ya biashara hizi ndio aeleze mchanganuo mzima ulivyoenda.

Maana mtu aki kuhadithia tu, anauza ice cream au tikiti, utahakikisha vipi kwamba ni kweli na hana biashara nyingine inayo msapoti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…