Kuna kazi wanaozifanya sijawahi kuelewa huwa wanaishi vipi

Kuna kazi wanaozifanya sijawahi kuelewa huwa wanaishi vipi

Ndio maana sijawataja wauza matunda, waosha magari na bodaboda. Kuna namna fulani muuza matunda katika Jiji kubwa anaweza kupiga hatua akakuza biashara na kipato, muosha magari tayari muda wote anakutana na watu wenye pesa na michongo, anaweza kuwa chawa, akajipatia sugar mamy, akaanzisha kijiwe chake kutokana na network aliyo nayo n.k. Bodaboda wanapata pesa nyingi sana, mtu unaweza kupata maendeleo kiasi kama hutakufa mapema au kuwa kilema kwa ajali.
Mkuu dunia kubwa sana hii, katika hao uliowataja hapo juu baadhi yao wanakuzidi kipato wwe ulipo hapo. Na kama naongea na mzee said salim bakhresa utanisamehe mzee fumba hakujambo?
 
Wamachinga watembezi bidhaa barabarani, bar n.k.
Wapiga debe,
Wauza ice cream,
Wabeba mizigo(makuli),
Wachuuzi stendi,

Sijawahi kuelewa mtu anayefanya hizi kazi anawezaje kukidhi mahitaji yake ya chakula, mavazi, makazi na kuhudumia familia bila kukata tamaa ya maisha.

Ni kazi za kusikitisha sana.
Hutembei uswahilini? Kuna sehemu nilikuta vyumba nikabaki nashangaa. 1. Vyumba vidogo kama vyoo, hata kitanda hakikai. Unakuta jamaa kagawa nyumba yake vyumba 20 na kila kimoja kina kijana analala pale. 2. Msosi kuna mama ntilie wa bei rahisi mno. Au wanachanga wananunua mafungu la utumbo wa kuku uliokaangwa, na unga kilo moja, wanakata na kachumbali za nyanya za rahisi siku inaenda.
 
Ninaowaona hasa hapo Mbezi stand ndogo wapo safi kabisa, tena baadhi yao ni wale makonda na madereva ambao hawana magari kwa kipindi hicho. Kila gari ni 1000.
Labda location, si unajua kila biashara ina location yake. Mimi kwangu salasala. Nikitoka na famikia wikiend kwenda beach za huku upande wa bagamoyo kuanzia mbuyuni mpaka tegeta huwa nawaona hata afya zao ni duni sana
 
Ninaowaona hasa hapo Mbezi stand ndogo wapo safi kabisa, tena baadhi yao ni wale makonda na madereva ambao hawana magari kwa kipindi hicho. Kila gari ni 1000.
Dereva au konda ambaye Hana gari wakati huo huwezi kusema ni mpiga debe, wapiga debe halisi ni wale ambao huwa unaona wanarushiwa mia mbili au jero wakati daladala inaondoka.
 
Kwa watembezi wa bidhaa, kuna pesa hapo tena ya maana kabisa, inategemea tu na bidhaa mfano kuna yale makampuni yanayotafuta ma ajenti wa kutembeza bidhaa maeneo mbalimbali unapewa na bei ya bidhaa husika hapo ukifika huko unaweza kuuza bidhaa ya 5k hata kwa 12k just inategemea na nguvu yako ya ushawishi na bidhaa husika. Ile unaweza kupata pesa fresh tu kabla ya mwisho wa mwezi
 
Maisha ni vile Ambavyo wewe utakavyo Yapa maana

Mwenzio anaweza kuishi kwenye chumba kimoja Na akala zake wali maharage and still akafurahia maisha , na ikawa Hana muda wakuwaza kabisa suala la kuwa na Mansion Wala gari hata la mtumba la ML 6, so maisha ni vile Ambavyo wewe utakavyo Yapa maana katika Psychology Yako ,

Ni sawa na namna ambavyo sisi tunavyoweza kuwashangaa wahadzabe na life style Yao wakati huo huo unaweza kukuta na wao wana tushangaa sisi na life style yetu huwenda wana Shangaa kwanini tuna Hangaika kufanya mambo mengi ya kuishi katika Dunia ya usasa wakati Maisha duniani tunapita tu
Good point, but neither excellent nor realistic view. Jamii zipo za aina tano, mtoa mana amezungumzia gepu katia yetu tunaoish maisha ya kisasa. Ni kweli leo hii mfugaji ukimuwekea ng'ombe 10 na ghorofa 1 ilala atachukua ng'ombe ainie nao porin

Watu wa tabala la chini,kazi wanazofanya na mahal wanapoishi kunafanana. Chumba kimoja inakaa famlia nzima yani baba mama na watoto humohumo. Kiuhalisia, nakubaliana na wewe partialy kuwa pengine maisha ya tia tia maji kwa standard ya maskini sio tatizo kabisa. Mlo miwili wa siku na dagaa la mia tatu, nyanya mia mbili na ndimu 100 wanakula familia nzima
 
Unajua hizi hearsay za kusimuliwa tu, hazina uthibitisho.

Hakuna anayeleta experience yake mwenyewe ya hizi biashara.

Kila mtu analeta stori za kuambiwa na kusimuliwa tu.

Mara, Kuna jamaa anauza tikiti tu, katoboa, kuna jamaa anauza ice cream tu, kuna jamaa anatembeza nguo tu.

Sasa hizi ni stori za kusimuliwa tu, inabidi mtu ambaye ametajirika na mwenye experience ya biashara hizi ndio aeleze mchanganuo mzima ulivyoenkuuda.

Maana mtu aki kuhadithia tu, anauza ice cream au tikiti, utahakikisha vipi kwamba ni kweli na hana biashara nyingine inayo msapoti?
Mkuu usibishe usichokijua kabisa, kuna goli nilikuwa nakunja 60k mpaka 70k per day, mchawi location tu na watu wasikucopy mitaa hiyo maana wabongo ni noma,
 
Back
Top Bottom