Kuna kazi wanaozifanya sijawahi kuelewa huwa wanaishi vipi

Kuna kazi wanaozifanya sijawahi kuelewa huwa wanaishi vipi

Sasa utaelewa vipi kazi ambayo sio kazi yako na hujawahi ifanya?
Hata wewe hapo kuna watu hawaielewi kazi yako mkuu, wanahisi unapoteza muda tuu! 😁
Ila hawakwambii, wanauchuna tuu.
Wala sihisi wanapoteza muda na kweli wanafanya kazi kweli kweli kuliko mimi na labda hata zaidi ya Punda vile, ambacho sielewi ni jinsi gani wanakidhi mahitaji yao na hizo kazi zao.
 
Mshangazi au sio ?? 🤸🥰🥰
Eenh nitafutie kakijana kadogodogo basi🤗
08902F62-2E5D-4BED-AD8B-28BEE952D941.jpeg
 
Hutembei uswahilini? Kuna sehemu nilikuta vyumba nikabaki nashangaa. 1. Vyumba vidogo kama vyoo, hata kitanda hakikai. Unakuta jamaa kagawa nyumba yake vyumba 20 na kila kimoja kina kijana analala pale. 2. Msosi kuna mama ntilie wa bei rahisi mno. Au wanachanga wananunua mafungu la utumbo wa kuku uliokaangwa, na unga kilo moja, wanakata na kachumbali za nyanya za rahisi siku inaenda.
Usonge ugali kilo wa nn? Ugali kwa mama ntilie 1200 tu maji 100 ya baridi. Yani 13000 unakula siku 10 mlo wa usiku tu
 
Semeni kooote ila hapa kwa waokota makopo hapo asilimia 99 ni wezi. Kilo moja ya makopo ni sh 400 kama haijapanda, niambie kwa siku anakusanya kilo ngapi auze sh ngapi

Nb; kuna baadhi ya hawa omba omba ni wachora ramani za ujambazi
 
mtoa Uzi umenifurahisha, mim ni machinga natembeza nguo za mtumba za wadada nimekosa sana Kwa siku faida 30k hadi 50k siku za weeknd na nakaa room ya 70k siyo Dsm nipo mkoa vyet vyangu nimeviweka uvunguni wa kitanda sijui kama havijaliwa na mende

lakin watu tukipita mtaani wananichukulia poa silipi Kodi TRA wala Kodi ya frame ofisi miguu yangu
 
Labda upate hela ya kula na kusogeza siku.

Ila hela ya kushusha mjengo mkali, labda ufanye hiyo biashara kwa kipindi kirefu sana, ukifanya savings za hatari kabisa.
Endelea kuishi kwenye denial, sio Tu mijengo kuna MTU namfahamu personal anauza spices sokoni na zimemfanya Ajenge Ghorofa.

Biashara haina fixed income na mjasiriamali hachagui biashara.
 
Makuli kushusha gunia la kiaz buku semi ina gunia 300 wanakuwa wanne kwa siku wanapiga had semitrael 2 jion kila mmoja anarud na ka 70 mtaji nguvu vp wewe wa mshahara laki 8 unaeza mfikia sema wanamatumiz makubwa hasa ya starehe
Acha stori za vijiwen mjomba, 40 feet unaijua vizur kushushwa na watu wawili!?
 
Endelea kuishi kwenye denial, sio Tu mijengo kuna MTU namfahamu personal anauza spices sokoni na zimemfanya Ajenge Ghorofa.

Biashara haina fixed income na mjasiriamali hachagui biashara.
Huyo mtu alikuthibitishia kwamba spices za sokoni ndio zilimuwezesha kujenga hilo ghorofa?

Alikupa mchanganuo wa mauzo wa hizo spices na mchanganuo wa ujenzi wa hilo ghorofa?

Ukahakikisha hiyo michanganuo miwili?
 
Endelea kuishi kwenye denial, sio Tu mijengo kuna MTU namfahamu personal anauza spices sokoni na zimemfanya Ajenge Ghorofa.

Biashara haina fixed income na mjasiriamali hachagui biashara.
Sasa muuza viungo sokoni si mtu anayeweza kulipia na kizimba kabisa, halafu spices ni bidhaa za thamani kubwa tu kama na ni rahisi kuuza za jumla hadi mikoani.
 
Wanaishi Kwa mahesabu makali Sana zaidi ya waliosoma uchumi halafu kingine Wana side hustle nyingine za kupata pesa (sio wote), wale wa Bar wengi ni Malaya halafu wanapata tips Sana, wapiga Debe wengine ni wezi, machinga hawa wako baadhi wanauza Sana mitaani na kukopesha juu, waokota makopo wengine ni wazee wa dili...

Kusema kweli wengi wanaofanya kazi za Kupiga Debe, wadada wa Bar, kuokota chupa wengi wao wamekata tamaa ya maisha na wachache Sana ndo Wana malengo, wamachinga hao wengi Wana akili timamu.

HIzo kazi Kwa nature Yake Hapa TZ ni kazi za SURVIVAL MODE, mtu akiwa kwenye Hali hii ni hatari Sana.
 
Kwa watembezi wa bidhaa, kuna pesa hapo tena ya maana kabisa, inategemea tu na bidhaa mfano kuna yale makampuni yanayotafuta ma ajenti wa kutembeza bidhaa maeneo mbalimbali unapewa na bei ya bidhaa husika hapo ukifika huko unaweza kuuza bidhaa ya 5k hata kwa 12k just inategemea na nguvu yako ya ushawishi na bidhaa husika. Ile unaweza kupata pesa fresh tu kabla ya mwisho wa mwezi
Moja kati ya kazi zenye kuzeesha na kudhoofisha mwili ni hizo kazi, wale wengi wao huwa ni wageni wa mji, wakishaujua mji huwa wanajiunga na wasajili line za simu
 
Wanaishi Kwa mahesabu makali Sana zaidi ya waliosoma uchumi halafu kingine Wana side hustle nyingine za kupata pesa (sio wote), wale wa Bar wengi ni Malaya halafu wanapata tips Sana, wapiga Debe wengine ni wezi, machinga hawa wako baadhi wanauza Sana mitaani na kukopesha juu, waokota makopo wengine ni wazee wa dili...

Kusema kweli wengi wanaofanya kazi za Kupiga Debe, wadada wa Bar, kuokota chupa wengi wao wamekata tamaa ya maisha na wachache Sana ndo Wana malengo, wamachinga hao wengi Wana akili timamu.

HIzo kazi Kwa nature Yake Hapa TZ ni kazi za SURVIVAL MODE, mtu akiwa kwenye Hali hii ni hatari Sana.
Hii ndio tafsiri nzuri zaidi kazi za 'survival", kwa hakika hizi kazi ni kwa ajili ku survive tu.
 
Sasa muuza viungo sokoni si mtu anayeweza kulipia na kizimba kabisa, halafu spices ni bidhaa za thamani kubwa tu kama na ni rahisi kuuza za jumla hadi mikoani.
Hata hao wa matunda ni same, unafkiri hawana meza? We pitia Mitaa niliotaja hapo juu then njoo lete feedback uuzaji wao
 
mtoa Uzi umenifurahisha, mim ni machinga natembeza nguo za mtumba za wadada nimekosa sana Kwa siku 30k hadi 50k siku za weeknd na nakaa room ya 70k siyo Dsm nipo mkoa vyet vyangu nimeviweka uvunguni wa kitanda sijui kama havijaliwa na mende

lakin watu tukipita mtaani wananichukulia poa silipi Kodi TRA wala Kodi ya frame ofisi miguu yangu
Hiyo 30k hadi 50k kwa siku ni mauzo au faida?
 
Huyo mtu alikuthibitishia kwamba spices za sokoni ndio zilimuwezesha kujenga hilo ghorofa?

Alikupa mchanganuo wa mauzo wa hizo spices na mchanganuo wa ujenzi wa hilo ghorofa?

Ukahakikisha hiyo michanganuo miwili?
Yap nina uhakika 99% ni MTU wa karibu na watoto wake ni best friends wangu. Hata hapa kkoo ukitaka naweza kukupoint wapi ukaangalie spices utokaje wake. Kuna sehemu kkoo watu wanapanga foleni sokoni almost all the time
 
Wala sihisi wanapoteza muda na kweli wanafanya kazi kweli kweli kuliko mimi na labda hata zaidi ya Punda vile, ambacho sielewi ni jinsi gani wanakidhi mahitaji yao na hizo kazi zao.

Huwezi kuelewa sababu hujafanya kazi hizo.
Makuli/wabeba mizigo watu sita wanaweza pakia/kushusha gunia 320 tani 32 kwenye lori/kichanja/flat bed.

Kila gunia wanapakiza na kupanga kwa shilingi 1000/= kutoka ghala mpaka kwenye gari, hivyo wanalipwa 300k kwa lori moja, kupakia na kupanga gunia kwenye gari. Wanakuwa wanapokezana kwa mzunguko.

Kuna sehemu ukienda kupakia mpunga, mahindi, ukezi au karanga kuna kazi tatu za makuli.
Kwanza mzigo lazima upimwe kwa debe au kwa kilo kulingana na tajiri anavyotaka ili hesabu ipatikane. Maana mkulima/dalali yeye anakuwa anaweka tuu mzigo ghalani hapimi, wakati wa biashara lazima mzigo upimwe na uwekwe kwenye gunia la tajiri. Hakuna mkulima au dalali atakuuzia mzigo na mfuko. 😁

1. Kupima kwa madebe au kwa kilo na kushona ni 300/= kwenye mfuko mpya.
2. Kupakiza kwenye gari inategemea na umbali, umbali ukiwa mkubwa ni 1000/=. Vijana sita wanafanya kazi hiyo. Wawili wanainua, mmoja anatia mgongoni kupeleka kwenye gari. Kule kwenye gari wawili wanampokea na kupanga steka kwenye gari.

Kwa hiyo kama mzigo unahitaji kupimwa na kupakizwa watakula 1,300/= kwa kila kilo mia au debe sita walizopima. Gari moja linakula tani 32, yaani gunia 320 zilizopangwa vizuri.

Sasa vijana hao kwa siku wanaweza wakapakia gari mbili. Unawezaje kusema wanaishi vipi bwashee.
 
Kuna wale vibarua wanapiga 'daywork' kwenye viwanda vya bia, soda, au kwa wahindi kubeba viroba vya unga, mabox, viwanda vya nondo naskia wanalipwa 3000-5000 kwa siku; hawa nao tunawaweka kundi gani?
 
Back
Top Bottom