Mkuu ukikaa nao chini unaweza ukajikuta pesa wanayopata ni zaidi ya mfunga tai anayekula kiyoyozi na anayetebelea crown.
Kuna jamaa yangu mmoja shughuli zake ni kuuza vipande vya tikitiki vya jero na buku ,jamaa ana mjengo mkali sana ,na kazi yake ni hiyo hiyo ,kuna mwingine anauza chipsi aisee ni hatari ana mijengo mitatu ,miwili mkoa anakusanya kodi na mmoja DIZIM ndipo anapokaa.
Kuna mwingine anaosha magari aisee wana maisha hao jamaa sema wasomi huwa wanawachukulia poa.
Kuna wengine wanaingiza pesa ni bodaboda nina maanisha boda ambaye anajielewa siyo hawa tatu mzuka au vishandu ,hao bodaboda au bajaji wanaingiza hadi laki sometime per day.