Kuna kazi wanaozifanya sijawahi kuelewa huwa wanaishi vipi

Kuna kazi wanaozifanya sijawahi kuelewa huwa wanaishi vipi

Mimi pia kama mtu niliyezaliwa na kukulia kijijini, napata shida sana kuelewa baadhi ya mambo na jinsi yanavyoendeshwa, mfano hayo aliyoyataja mleta mada.

Kuna muda nikiwaangalia naanza kuoverthink na kuwa emotional 🥹
Sasa unakuta umetulia zako Bar unapata Safari zako huku unasubiria kitimoto nusu na ndizi mbili halafu mtu anapita na mbegu za maboga au soksi, kwa kweli huwa ni huzuni sana hadi mtu unaji feel guilty kama vile wewe ndio ulisababisha awe katika hali hiyo.
 
Mkuu ukikaa nao chini unaweza ukajikuta pesa wanayopata ni zaidi ya mfunga tai anayekula kiyoyozi na anayetebelea crown.

Kuna jamaa yangu mmoja shughuli zake ni kuuza vipande vya tikitiki vya jero na buku ,jamaa ana mjengo mkali sana ,na kazi yake ni hiyo hiyo ,kuna mwingine anauza chipsi aisee ni hatari ana mijengo mitatu ,miwili mkoa anakusanya kodi na mmoja DIZIM ndipo anapokaa.

Kuna mwingine anaosha magari aisee wana maisha hao jamaa sema wasomi huwa wanawachukulia poa.

Kuna wengine wanaingiza pesa ni bodaboda nina maanisha boda ambaye anajielewa siyo hawa tatu mzuka au vishandu ,hao bodaboda au bajaji wanaingiza hadi laki sometime per day.

Story ikianza "kuna jamaa " huwa zina uongo mwingi sana,

Kwanini isiwe "mimi?" Kuna jamaa kuna jamaa, 🚮🚮🚮
 
Kuna watu wanafanya kazi zinazoonekana hazina hela, unaweza kujiuliza wanapataje hela za kukidhi mahitaji yao? Siri za mafanikio yao wanazo wenyewe, hiyo ni code yao wengine hatuwezi kujua wanapataje hela kupitia kazi zao hizo wanazozifanya
 
Ice cream za Bakhresa zinauzwa 250/300 wao wanauza 500 MTU akiuza dell zima box zake mbili ama 3 ana zaidi ya 20,000 faida, hela kubwa kushinda mwalimu.

Machinga wengi wanapata hela ndefu hasa hao wa mjini, sasa hivi wao ndio wanaongoza kwa retail maduka mengi yamebaki jumla.

Kuna wabeba mizigo wanafunga zaidi ya laki kwa siku, right area na connection ni biashara moja nzuri kushinda hata maofisa wa juu wa Wizara ama Taasisi kubwa hapa Mjini.

Kijana yoyote wa mjini anajua hizo KAZI watu wengi wanatoboa.
True
 
Hii nimekataa...lazima anamiliki bonge la koboko ndani...pilipili manga na karafuu hizi hizi nazozijua?🤔
Yes hizo hizo, kama unajua unapata wapi ama Lima mwenyewe.

Zaatari kilo moja inafika Hadi 80,000 kwa MTU ambaye ana vertical integration ni super profit.

Kila biashara ina Eneo lake kutega na technical know how pamoja na ujasiriamali wako, usidharau biashara yoyote, wengi humu wanaoropokwa ni watu ambao hawana skills za ujasiriamali.
 
nilikuwa kuli asa unabishana na mimi
Mimi pia katika career yangu nimewahi shika kitengo cha Export ICD za Bandarini, nilikua nasimamia makuli kama 6-8 hivi, hao wanashusha Hadi lori 6 kwa siku kupakiza kwenye container, kila Lori at that time tulikua tunalipa 80,000-120,000 miaka kama 10 iliopita. Kuli wawili kushusha 40 feet ni kawaida kabisa, inategemea Tu na bidhaa yenyewe.

Kkoo ama sehemu nyengine za biashara container moja linashushwa na makuli wengi sababu distance toka kwenye gari Hadi store ni parefu inabidi wagawane roles anayeshusha, anaetembea, anayepanga store etc, Ila hizo za Magunia ama mbao unatoa kwenye Lori na kubwaga Tu chini MTU mbili wanapiga KAZI bila tatizo.
 
Yes hizo hizo, kama unajua unapata wapi ama Lima mwenyewe.

Zaatari kilo moja inafika Hadi 80,000 kwa MTU ambaye ana vertical integration ni super profit.

Kila biashara ina Eneo lake kutega na technical know how pamoja na ujasiriamali wako, usidharau biashara yoyote, wengi humu wanaoropokwa ni watu ambao hawana skills za ujasiriamali.
Humu wengi wanaongea kitu wasichokijua. Miaka kadhaa nyuma nilifanya biashara ya iriki aisee balaa. Yaani mzigo unanunuliwa kabla haujafika.
Kiujumla biashara ya viungo ni pesa inayopatikana bila jasho.
 
Story ikianza "kuna jamaa " huwa zina uongo mwingi sana,

Kwanini isiwe "mimi?" Kuna jamaa kuna jamaa, 🚮🚮🚮
Unataka nimtaje? Hao naosema kuna jamaa mimi ndiyo nawajua na ninawaona ,nimeweka jamaa kuficha identity zao...ila nikimwambia nenda sehemu flani utamkuta huyo nayesema jamaa.
 
Back
Top Bottom