Kuna kazi wanaozifanya sijawahi kuelewa huwa wanaishi vipi

Mkuu dunia kubwa sana hii, katika hao uliowataja hapo juu baadhi yao wanakuzidi kipato wwe ulipo hapo. Na kama naongea na mzee said salim bakhresa utanisamehe mzee fumba hakujambo?
 
Hutembei uswahilini? Kuna sehemu nilikuta vyumba nikabaki nashangaa. 1. Vyumba vidogo kama vyoo, hata kitanda hakikai. Unakuta jamaa kagawa nyumba yake vyumba 20 na kila kimoja kina kijana analala pale. 2. Msosi kuna mama ntilie wa bei rahisi mno. Au wanachanga wananunua mafungu la utumbo wa kuku uliokaangwa, na unga kilo moja, wanakata na kachumbali za nyanya za rahisi siku inaenda.
 
Ninaowaona hasa hapo Mbezi stand ndogo wapo safi kabisa, tena baadhi yao ni wale makonda na madereva ambao hawana magari kwa kipindi hicho. Kila gari ni 1000.
Labda location, si unajua kila biashara ina location yake. Mimi kwangu salasala. Nikitoka na famikia wikiend kwenda beach za huku upande wa bagamoyo kuanzia mbuyuni mpaka tegeta huwa nawaona hata afya zao ni duni sana
 
Wastani wa pato la Mtanzania kwa mwezi ni laki mbili na nusu, huo ni wastani kwa hiyo kuna wengine wanapata zaidi na wengine wanapata kidogo. Nina uhakika Kuna watembeza bidhaa wengi kwa siku wanaambulia elfu tano tu.
Sasa mbona hashangi mtu anaishije kwa laki mbili na nusu?
 
Ninaowaona hasa hapo Mbezi stand ndogo wapo safi kabisa, tena baadhi yao ni wale makonda na madereva ambao hawana magari kwa kipindi hicho. Kila gari ni 1000.
Dereva au konda ambaye Hana gari wakati huo huwezi kusema ni mpiga debe, wapiga debe halisi ni wale ambao huwa unaona wanarushiwa mia mbili au jero wakati daladala inaondoka.
 
Kwa watembezi wa bidhaa, kuna pesa hapo tena ya maana kabisa, inategemea tu na bidhaa mfano kuna yale makampuni yanayotafuta ma ajenti wa kutembeza bidhaa maeneo mbalimbali unapewa na bei ya bidhaa husika hapo ukifika huko unaweza kuuza bidhaa ya 5k hata kwa 12k just inategemea na nguvu yako ya ushawishi na bidhaa husika. Ile unaweza kupata pesa fresh tu kabla ya mwisho wa mwezi
 
Good point, but neither excellent nor realistic view. Jamii zipo za aina tano, mtoa mana amezungumzia gepu katia yetu tunaoish maisha ya kisasa. Ni kweli leo hii mfugaji ukimuwekea ng'ombe 10 na ghorofa 1 ilala atachukua ng'ombe ainie nao porin

Watu wa tabala la chini,kazi wanazofanya na mahal wanapoishi kunafanana. Chumba kimoja inakaa famlia nzima yani baba mama na watoto humohumo. Kiuhalisia, nakubaliana na wewe partialy kuwa pengine maisha ya tia tia maji kwa standard ya maskini sio tatizo kabisa. Mlo miwili wa siku na dagaa la mia tatu, nyanya mia mbili na ndimu 100 wanakula familia nzima
 
Mkuu usibishe usichokijua kabisa, kuna goli nilikuwa nakunja 60k mpaka 70k per day, mchawi location tu na watu wasikucopy mitaa hiyo maana wabongo ni noma,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…