Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Mnaelekea walipo kkkt [emoji776]
 
Unaendaje kanisani na buku 5 mkuu? Wakati baa mnaingia na laki beba kuanzia hamsini ukiona unahoji mambo ya sadaka jua umekufa kiroho toa ulichonacho huna tulia Mungu anakuona matumiz ya sadaka hayatuhusu imarisha uhusiano wako na Mungu kwa kutoa
 
Kweli michango imezid na inakera. Unatoa sadaka kabla hata kanisani hujafika na kabla hujashiriki mtiririko mwingine wa ibada.
Japo siwez hama kwa hizo sababu lakin inabid warekebishe mahali wanatukwaza waumini.
 
Lakini ni hiyari yako tu hapo usisingizie Dini.
Wanaoangamia leo ni kwa kukosa maarifa siyo kitu kingine...mwisho wa kunukuu.
 
Kwa bahati mbaya aliowaachia kanisa wakendeleze wanashikana mashati kugombea makanisa
 
Kwa uzoefu wangu mdogo wa eneo nililokulia, zamani kulikuwa na mapadre wazungu, ambao mashirika yao na waumini wa huko ulaya, walikuwa hawaishi kuleta pesa,magari, mitumba, chocolate na biskuti, ambacho, viliwezesha kujenga makanisa, shule, na nyumba za mapadre na masista. Nafikiri siku hizi mambo yamebadilika, kama wapo wazungu ni wachache, na wazawa ndio wanashikilia uongozi na hakuna misaada kama ya mwanzo. Sasa hii michango lukuki kama inakwenda kimahesabu au ni ulaji, hilo sijui.
 
M nakushauri tu jaribu kuusoma na Uislamu
 
[emoji23][emoji23][emoji23], baada ya kifo ni HUKUMU, mengine ni maigizo tuu
 
Wanasema mrija wa wahisani umekatika. Lakini zamani ulivyokuwepo pia kanisa lilikua linajishughulisha na shughuli nyingine za kujiingizia kipato. Sijui kimetokea nini mpaka wanatulalia waumini.

Mimi hua nawachallenge viongoz wangu wa jumuiya na wanabaki kucheka cheka bila majibu
 
Roma kama Roma, ni muda wa kujitafakari sana madhumuni ya kuja hizi dini hapa bongo
 
Siku ukipata au ukihitaji huduma ya kikanisa, ndio utajua mashtaka unapata au hupati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…