Mwalimu wa tuisheni
JF-Expert Member
- Oct 19, 2019
- 6,602
- 10,801
Vatican kwa popeHizo fedha wanapelekaga wapi ukizingatia jamaa wanasema hawaruhusuwi kuoa na wenzao hawaruhusiwi kuolewa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vatican kwa popeHizo fedha wanapelekaga wapi ukizingatia jamaa wanasema hawaruhusuwi kuoa na wenzao hawaruhusiwi kuolewa?
Mnaelekea walipo kkkt [emoji776]Nilijuwa watetezi hamuwezi kukosekana, hebu nieleze tu miradi ya kanisa katoliki ina faida gani kwa kanisa? Na ile benki yetu ya Mkombozi inalifaidisha vipi kanisa?
Kwani huko nyuma tuliweza vipi kujenga makanisa na mashule kwa sadaka za kawaida bila huu uharamia mpya ulioingia? Ni nini kilichobadirika?
Sisi parokia yetu ilikuwa na vigango vitatu na vyote vimekuwa parokia sasa zenye makanisa makubwa tu, tuliwezaje hayo kwa mwendo wa kawaida bila watu kunung'unika na leo kimebadirika nini?
Huamini au?[emoji2][emoji2][emoji2] yani waliotuletea dini mioyo yao imepoa?,
Pope anapeleka wapi pesa?Vatican kwa pope
Unaendaje kanisani na buku 5 mkuu? Wakati baa mnaingia na laki beba kuanzia hamsini ukiona unahoji mambo ya sadaka jua umekufa kiroho toa ulichonacho huna tulia Mungu anakuona matumiz ya sadaka hayatuhusu imarisha uhusiano wako na Mungu kwa kutoaInakuwa kama mchango wa kuendesha NGO bwana! tena bora ya hiyo mnatoa ada na kiingilio kama 50,000 kwa mwaka lakini unanufaika maana siku nyingine mnaenda kula kuku pale SERENA hotel kwenye semina.
Mimi kuna siku nimeenda kusali anglicana na buku 5, michango iliyotajwa hapo ikaonekana ile hela ni takataka. Kilichoniokoa ni kwa siku hiyo alikuja askofu kwa hiyo ratiba ilibadilika kidogo wakasogeza mbele michango.
Watu taratibu wameanza kuuelewa ukweliNdio maana nchi zilizoendelea makanisa yamegeuzwa museums watu walishashtuka siku nyingi kwamba huu wa sasa ni upigaji. Huku kwetu ndio bado watu wameng'ang'ania ila taratibu tutakuja kuelewana tuu.
Kwa bahati mbaya aliowaachia kanisa wakendeleze wanashikana mashati kugombea makanisaNi vigumu kwa vijana wa kizungu kuwaswaga kama tunavyofanyiwa waumini wa Tanzania.
Uzuri wa wazungu wana reasoning, ndio maana hata walipoleta hii dini walikuwa wanajenga wao makanisa na hospitali target yao ilipotia wakavuta end break.
Sasa ajitokeze mkatoliki hapa leo anieleze miradi mikubwa ya kanisa chuo kikuu cha SAUT mashule, mahospitali mahostel yana faida gani kwetu kama waumini tunaendelea kukamuliwa hivi?
Maana hata Martin Luther alipojitenga na Vaticano na yeye kuna mambo ya kipuuzi yalimkwaza.
Kwa uzoefu wangu mdogo wa eneo nililokulia, zamani kulikuwa na mapadre wazungu, ambao mashirika yao na waumini wa huko ulaya, walikuwa hawaishi kuleta pesa,magari, mitumba, chocolate na biskuti, ambacho, viliwezesha kujenga makanisa, shule, na nyumba za mapadre na masista. Nafikiri siku hizi mambo yamebadilika, kama wapo wazungu ni wachache, na wazawa ndio wanashikilia uongozi na hakuna misaada kama ya mwanzo. Sasa hii michango lukuki kama inakwenda kimahesabu au ni ulaji, hilo sijui.Nilijuwa watetezi hamuwezi kukosekana, hebu nieleze tu miradi ya kanisa katoliki ina faida gani kwa kanisa? Na ile benki yetu ya Mkombozi inalifaidisha vipi kanisa?
Kwani huko nyuma tuliweza vipi kujenga makanisa na mashule kwa sadaka za kawaida bila huu uharamia mpya ulioingia? Ni nini kilichobadirika?
Sisi parokia yetu ilikuwa na vigango vitatu na vyote vimekuwa parokia sasa zenye makanisa makubwa tu, tuliwezaje hayo kwa mwendo wa kawaida bila watu kunung'unika na leo kimebadirika nini?
M nakushauri tu jaribu kuusoma na UislamuMimi ninavyojuwa dini ni swala binafsi la mtu mahusiano yake na Mungu, hizi dini za Abraham sioni kama zinatofautiana, zote zinaongelea kitu kilekile ila tu tafsiri na mapokeo ni tofauti, vitabu ambavyo vipo kwenye biblia baadhi yake vipo kwenye Quran.
Huwezi kuamini nikikwambia huwa naita masheikh kufanya duwa nyumbani kwangu.
Tatizo la upande wa Ukristo sasa hivi viongozi wameamuwa kuwa wanyang'anyi na kuwafanyia uharamia waumini wake pasipo kuwaonea huruma.
[emoji23][emoji23][emoji23], baada ya kifo ni HUKUMU, mengine ni maigizo tuuKuna ile ya kuwataka waumini waliofiwa na wapendwa wao eti watoe sadaka kubwa kubwa kadri wawezavyo kama kikokotoo cha kuwawezesha hao wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki kupata ahueni ya maisha huko kaburini. Yaani mimi hii haijawahi kuniingia akilini kabisa.
Wanasema mrija wa wahisani umekatika. Lakini zamani ulivyokuwepo pia kanisa lilikua linajishughulisha na shughuli nyingine za kujiingizia kipato. Sijui kimetokea nini mpaka wanatulalia waumini.Sisi parokia yetu imezaa parokia tatu, unaweza kuelewa machozi na damu tuliyopitia.
Tuna nyumba ya masista, tuna nyumba ya mapadri ya zamani, ikajengwa ghorofa likaja hilo ghorofa likaonekana dogo utadhani mapadre wetu ni matembo tukajenga ghorofa nyingine mpya kubwa.
Tumemnunulia paroko Prado, tuna dispensary tuna maternity tuna Ambulance tuna nursery school, kama hiyo haitoshi kuna nyumba nne jirani tumezinunuwa tumevunja ndio umeanza upuuzi eti tujenge nyumba ya mama bikira Maria.
Yani the way nilichojifunza hakuna kipindi mtaachwa mpumuwe ni kutwishana mizigo mwaka mzima.
Roma kama Roma, ni muda wa kujitafakari sana madhumuni ya kuja hizi dini hapa bongoMkuu, hata ukitoa unaweza usipewe huduma vilevile!
Mimi mama yangu mzazi alikua kiongozi wa jumuia huko kijijini na alikua mtoa sadaka asie na kifani, shughuli zote za ujenzi wa kanisa alishiriki kikamilifu kwa maisha yake yote mpaka amezeeka.
Bahati mbaya akaja kupata tatizo la kiafya ambalo limemuweka kitandani zaidi ya miaka 10 sasa. Cha ajabu eti kila mwaka analetewa bahasha ya zaka na kanisa linatishia kwamba akifa halitamzika kama sisi watoto hatutakua tunatoa hela za kwetu na zake!
Sasa mimi najiuliza, mtu ambae amelala kitandani hilo fungu la 10 analitoa wapi? Tangu amelala kitandani, kanisa limemsaidia vipi? Michango yote aliyochanga tangu akiwa binti mdogo mpaka sasa ni mzee, haijatosha tu? Ni mpaka tone la mwisho??
Siku ukipata au ukihitaji huduma ya kikanisa, ndio utajua mashtaka unapata au hupati.Wajinga ndio waliwao
Yesu Kristo hakukusanya fedha hivyo, kama tunaishi kwa mfano wa Yesu Kristo basi tukatae mambo yote ya Caeisar, hivyo wakristo lazima tuwe macho sana kwa sasa, makanisa yamekuwa ni business as usual. Bahati nzuri sana, usipotoa, hakuna mashtaka.
Hakuna ubora hapo ni vile hujapa yanayowasibu wanaoenda hukoBora Anglicana