Kuna madhara gani mwanaume anapochelewa kuoa?

Ujue maisha yana formula ingawa wengine hulipinga hili.

Kijana anayeoa mapema ana fursa nzuri sana ya kuenjoy maisha yake na mkewe uzeeni mwake.

Kama ni kustaafu, atastaafu akiwa kamaliza majukumu yote ya kulea na kusomesha watoto zake.

Let say, kaoa akiwa na umri wa miaka 25-30.
Miaka 30 mbele yake ni ya kumaliza kabisa majukumu ya lazima ya malezi.

Haya mambo ya kusema kujijenga kwanza, huwa ni dhana ya kufikirika zaidi ya uhalisia ambayo mimi imeniathiri pakubwa.

Mawazo ya kimfumo dume hutuchelewesha sana wanaume kujenga familia zetu mapema.

Ni nani aliyesema ukioa mapema mwanamke mwenye mapenzi ya dhati pamwe uchungu wa maisha huwa anachelewesha maendeleo?

Mchango wa mawazo pamoja na nguvu ya mwanamke kwenye maisha ya ndoa ni muhimu sana kwa maendeleo ya familia.
Ninayasema haya kwa uzoefu.

Nilijipoteza makusudi kwa kujichelewesha kuoa nikijidanganya kwa kufikiria hayo wanayoyafikiria vijana wa sasa, ninaona jinsi wanajipoteza.

Nina watoto wa mwisho wanaoniita 'babu' kwa sababu wanalingana makamo na wajukuu wa wadogo zangu.

Furaha niliyonayo ni kwamba hatutaishi peke yetu na mke wangu hapa nyumbani kwa kuwa nitakuwa nina watoto wangu chipukizi watakaonifariji kwa maisha yangu yote.
 
mkuu umefanya nicheke kweli ati nini, wewe
 

Tafuta pesa kaka. Jay Z anamzidi Beyonce kama miaka 20 hivi. Donald Trump kamzidi mke wake miaka 30. It’s all about Benjamins
 
Kumbe wanaume na nyie mna deadline? Nikajua ni sisi wadada tu🤔
Aaah unakosea banaa,mwanaume hana deadline hata kidogo sema tu ni ile heshima ya yeye kuna mume/na ndoa.....sio kama mwanamke huwa wanachacha wakivuka certain age🤣🤣🤣....sijui ushanfahamu atiii.
 
Umri sahihi wa mwanaume kuoa ni 27-38.Hii imethibitishwa kitaalamu kabisa.Umri huu anakuwa amekomaa akili ipasavyo na kuuacha ujana wote.Ni tofauti na akiwahi lazima ndoa itikisike,japo unaweza wahi na ndoa ikadumu.
umri wangu huu,dah kumbe bado nipo ndani ya muda...hadi mwakaniiiii
 
Dah mimi nakaribia 30 ila sina hata mtoto wa kusingiziwa! Unanishauri vipi[emoji848] niachane na uzazi nishachelewa ama?
The funniest part is.. baba yangu ananambia hv mamii kuna wanaume siku hizi[emoji23] naomba uangalie maisha yako kwanza. Kijana anakuja na suruali matakoni halaf useme ndo mume? Akanambia kwanza kuolewa mateso tu... hebu tufocus na hela[emoji23][emoji23] suala hili kwa kweli kwetu hakun kusakamana. Aliyeolewa kaolewa. Ambaye bado basi bado. Mbali na kwamba having ur own family is a blessing lakini nyumbani nako patamuu... maybe kma kwenu kuwe na tatizo or else unaozea hapo
 
njoo kwangu tuunganishe KOO
 
Kumbe wanaume na nyie mna deadline? Nikajua ni sisi wadada tu[emoji848]
Deadline ni ukosefu wa pesa kwa wanaume wa mijini na wale wa kijijini deadline ni ukosefu wa nguvu za kiume na kuwa na watoto wa kiume ambao wakioa wanawachukua mama zao na kuishi nao mjini na kuwaacha baba zao kijijini wanapigika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…