Wote mna changamoto.
Tukianza na wewe, hupaswi kumuadhibu mtoto kwa kujikojolea. Ukweli ni kuwa kukojoa kutakoma baada ya muda. Ungetafuta namna ya kumsaidia, ama aamshwe usiku akakojoe au kuweka vizuia unyevu kupenya kwenye godoro.
Lakini pia, kama unaona ungekuwa na ualakini katika malezi basi usingemruhusu kutoka awali aje na mwanae. Kama alikataa kumpeleka kwa mama yake basi nawe ungekataa kukaa naye.
Tukirudi kwake, hapaswi kukulazimisha umpende mwanae. Upendo huja automatically, haulazimishwi.
Lakini pia, ana akili za kimalaya. Kwamba, unapawa kumhudumia kwa sababu unamtumia. Sijui namna gani unamtumia, ila nadhani ni kulala naye. Kama unamfanyisha kazi basi anastahili mshahara.
Ngono si one side sided. Kila mmoja anawajibika kwa mwingine. Ninyi wote mnafurahia.
Lakini pia, amezidisha mapenzi kwa mwanaye. Mpaka analazimisha mambo ya hovyo. Kutotaka mtoto wa miaka 7 alale mwenyewe ni upuuzi. Mtoto hawezi kulala mwenyewe wala si traumatization. Ni malezi bora kabisa akajilalie mwenyewe.
Kulala na mtoto wa miaka saba ukiwa na mpenzi wako kitanda kimoja ni unyanyasaji. Mtoto wa 7 years ni mkubwa sana. Anaelewa vitu vingi. Kusikia mama yake analia huku anapelekewa pipe, ni unyanyasaji.
Cha msingi hamtawezana. Kila mtu afuate muelekeo wake.