Dr Restart mi natofautiana na wewe.
1. Mtoto wa miaka 7 kujikojolea sio sahihi, unless ana tatizo la kiafya. Mimi nilimchapa wakwangu akiwa na 5 ama 6 kama siokosei....na aliacha immediately maana katabia kenyewe kaliibuka out of nowhere. Watoto wana tendency yakujaribu watu kwakufanya makosa kwa makusudi pale wanapoamini they'll get away with it. Kuna mtoto wa dada yangu (12 yrs old), huwa anakojoa kitandani, tena sometimes asubuhi kushakucha. Nimeshasafiri nae mara mbili, biti analopigwa kuhusu kujikojolea ugenini huwa lina matokeo chanya, which proves nyumbani huwa anafanya makusudi maana anaeishia kugombezwa ni dada wa kazi na sio yeye.
2. Kama nimeelewa sahihi
Tuta Absoluta Kantangaze alikua na malengo na mpenzi wake, so jambo la kuruhusu/taka mtoto awe sehemu ya muda wao pamoja halina ubaya wowote. Ilikua vizuri ili watengeneze bond, lakini pia imemsaidia kujua huyo dada ni
mama wa aina gani. Angekuja kugundua miaka miwili/mitatu baadae wameshaongeza wakwao ingekua mbaya zaidi.
3. Jamaa haonyeshi kutokumpenda mtoto, nnachoona ni kwamba analazimishwa kumkubali na tabia zake hata ambazo sio nzuri pamoja na aina ya malezi anayopewa. Kitu ambacho sio sahihi. If we are being honest, huyo mwanamke anaweza kuona kama anamsaidia mwanae kwakumuendekeza (sio kumpenda) ila anamuharibu.
All in all, the guy is right. Kupitia maongezi yao inaonekana kabisa he's done his best, ila
single mother hana shukrani wala hataki hata ku-acknowledge juhudi za jamaa. Amuache akachoshane na mtu mwingine mbele ya safari.