Kuna mambo hutokea katika Uhusiano ujue mwenzi wako ni mtu wa namna gani. Huyu wangu nimegundua hana akili

Kuna mambo hutokea katika Uhusiano ujue mwenzi wako ni mtu wa namna gani. Huyu wangu nimegundua hana akili

Wanawake was hivi tunakutanaga nao Sana tu sema tunajiaminishaga watabadilika
Mfano mama J wako.
allooooooh!
Mimi ni mwanamke , ila siwezi hata urafiki, ujirani wala chochote na yule mwanamke wako!
Ningekuwa namkata vibao kila siku!
Haki siwezi!
Huwa nakushangaa , ila ndo hivo wenyewe mnapendana!
 
Nimecheka kama mazuri
ama kweli mwenye bahati habahatiki.. Dada angu kashindwa kuwa na shukrani hajui hujamzaa/wala sio baba wa mtoto unafanya kwa hisani tu! Mana kama kutumika unaweza ukalalwa mwaka na usipewe kitu!

Yani hapo mama mtu ndo ana trauma/inferiority hoja ni kufiwa kuhalalisha ujinga! Kwa style hio tutaendelea kukuza kizazi cha hovyo mno! Et bibiake mkali
ila mkome na nyie si mnataka beauty with brain yatawakuta mengi mno
 
Hahah eti kama ni hivyo nipangie nyumba ya vyumba viwili na jiko ya laki 3 niajiri dada wa kazi ili nikiwa nakuja kwako niwe namuacha na dada...nimegundua huyo analea mtoto kama yai na bibi yake mtoto hapendi ujinga ndo maaana hataki akae nae..yani analea bomu..

Huyu mwanamke ni pasua kichwa..yani kama utamrudia kisa sijui mzuri...walai utakufa kabla ya siku zako..
Hi kulea mtoto kwa social media ndio madhara yake. Kuna familia nilienda eti mtoto amelia tu kidogo nikasikia maza ake anasema dogo apewe simu aangalie katuni funny na video za kuchekesha huko youtb ili anyamaze .Nikasema DAAH! Mungu atusaidie sana. 50 to 100 yrs to come sijui kutakuwa jamii gani.
 
Wote mna changamoto.

Tukianza na wewe, hupaswi kumuadhibu mtoto kwa kujikojolea. Ukweli ni kuwa kukojoa kutakoma baada ya muda. Ungetafuta namna ya kumsaidia, ama aamshwe usiku akakojoe au kuweka vizuia unyevu kupenya kwenye godoro.

Lakini pia, kama unaona ungekuwa na ualakini katika malezi basi usingemruhusu kutoka awali aje na mwanae. Kama alikataa kumpeleka kwa mama yake basi nawe ungekataa kukaa naye.

Tukirudi kwake, hapaswi kukulazimisha umpende mwanae. Upendo huja automatically, haulazimishwi.

Lakini pia, ana akili za kimalaya. Kwamba, unapawa kumhudumia kwa sababu unamtumia. Sijui namna gani unamtumia, ila nadhani ni kulala naye. Kama unamfanyisha kazi basi anastahili mshahara.

Ngono si one side sided. Kila mmoja anawajibika kwa mwingine. Ninyi wote mnafurahia.

Lakini pia, amezidisha mapenzi kwa mwanaye. Mpaka analazimisha mambo ya hovyo. Kutotaka mtoto wa miaka 7 alale mwenyewe ni upuuzi. Mtoto hawezi kulala mwenyewe wala si traumatization. Ni malezi bora kabisa akajilalie mwenyewe.

Kulala na mtoto wa miaka saba ukiwa na mpenzi wako kitanda kimoja ni unyanyasaji. Mtoto wa 7 years ni mkubwa sana. Anaelewa vitu vingi. Kusikia mama yake analia huku anapelekewa pipe, ni unyanyasaji.

Cha msingi hamtawezana. Kila mtu afuate muelekeo wake.
Mmmh kupelekewa pipe...??
 
Ngoja kwanza , twende taratibu na ujibu hili swali Kabla ya kuamua kuishi nae huyo single maza ulijua sababu ya kifo cha mume wake?

Maana tunawaambia kila siku vijana siyo tuu muonyeshwe kaburi na cheti cha kifo mkaridhika ,hata kujua sababu ya kifo cha mume wake ni point ya msingi sana kuiweka maanani.
Wee jamaa mchawi 😅😅😅😅😂😂😂😂😅😅😅😅😅😅😅
 
Mwishowe mitoto inakuja kuwa mishoga kwa kuendekeza upumbavu wa kuwalealea kizungu... Sijui kwanini nimejikuta natamani huyo mtoto aje aishi kwetu nadhani angenyooka wote na mama yake😬😬🤦
Sasa wewe ungemfanyaje mama yake? Dude lililokubuhu, likashindikana na mwanaume, wewe ungewezaje kumnyoosha?
 
Hi kulea mtoto kwa social media ndio madhara yake. Kuna familia nilienda eti mtoto amelia tu kidogo nikasikia maza ake anasema dogo apewe simu aangalie katuni funny na video za kuchekesha huko youtb ili anyamaze .Nikasema DAAH! Mungu atusaidie sana. 50 to 100 yrs to come sijui kutakuwa jamii gani.
Miaka 50 mbalii..miaka 20 tuu ijayo..ni aibu
 
Ni jambo baya ila naweka pia na wengine wajifunze. Wakati mwingine usitake sana kumridhisha au kumfurahisha mwenzio. Usitake kuvumilia sana tabia ambazo unajua si sawa kwa kigezo cha mapenzi.

Huyu dada nilimkuta na mtoto nikamwambia haina shida nitamlea mtoto. Mumewe alifariki. Lakini kama ambavyo nliandika uzi jana. Sisemi single mothers wote wapo hivi ila huyu wangu ni kilaza. Nlimuamini sababu ana degree alimaliza CBE na ni dada mzuri wa sura , umbo na rangi. Nlidhani pia kwa kufiwa na kuwa na mtoto angekuwa matured. Bado ana upumbavu mwingi kichwani.

View attachment 2866044View attachment 2866046View attachment 2866048View attachment 2866049

mkuu tunashukuru kwa huu uzi!!

We unamoyo mi siwez hata moja yaan uyo mwanamke ningeachana nae siku ya pili! tu mtoto wa miaka 7 anajikojolea??? hapana siwezi huu ujinga
 
Sasa wewe ungemfanyaje mama yake? Dude lililokubuhu, likashindikana na mwanaume, wewe ungewezaje kumnyoosha?
Sio Mimi, Namaanisha wazazi wangu wangewanyoosha kweli nakwambia😂😂.. Mzee wangu Mimi Hana lelemama,.. Nadhani angeanza na huyo dogo within a week kujikojolea ingekua historia, hata bila kuambiwa mda wakulala ukifika anaongoza mwenyewe chumbani kwake kulala pekeyake.. Halafu angefata mama yake Kuna lifestyle tu moja hivi ya kijeshi angepitishwa kiburi chote na kujitoa ufahamu angeacha..
 
Wote mna changamoto.

Tukianza na wewe, hupaswi kumuadhibu mtoto kwa kujikojolea. Ukweli ni kuwa kukojoa kutakoma baada ya muda. Ungetafuta namna ya kumsaidia, ama aamshwe usiku akakojoe au kuweka vizuia unyevu kupenya kwenye godoro.

Lakini pia, kama unaona ungekuwa na ualakini katika malezi basi usingemruhusu kutoka awali aje na mwanae. Kama alikataa kumpeleka kwa mama yake basi nawe ungekataa kukaa naye.

Tukirudi kwake, hapaswi kukulazimisha umpende mwanae. Upendo huja automatically, haulazimishwi.

Lakini pia, ana akili za kimalaya. Kwamba, unapawa kumhudumia kwa sababu unamtumia. Sijui namna gani unamtumia, ila nadhani ni kulala naye. Kama unamfanyisha kazi basi anastahili mshahara.

Ngono si one side sided. Kila mmoja anawajibika kwa mwingine. Ninyi wote mnafurahia.

Lakini pia, amezidisha mapenzi kwa mwanaye. Mpaka analazimisha mambo ya hovyo. Kutotaka mtoto wa miaka 7 alale mwenyewe ni upuuzi. Mtoto hawezi kulala mwenyewe wala si traumatization. Ni malezi bora kabisa akajilalie mwenyewe.

Kulala na mtoto wa miaka saba ukiwa na mpenzi wako kitanda kimoja ni unyanyasaji. Mtoto wa 7 years ni mkubwa sana. Anaelewa vitu vingi. Kusikia mama yake analia huku anapelekewa pipe, ni unyanyasaji.

Cha msingi hamtawezana. Kila mtu afuate muelekeo wake.

Nakubali kote ila hapo kwene mtoto wa miaka saba kukojoa et ni sawa !! Bi no

labda n ukoo wenu

sisi miaka 4 nakumbuka nimeacha chekechea
 
Sio Mimi, Namaanisha wazazi wangu wangewanyoosha kweli nakwambia😂😂.. Mzee wangu Mimi Hana lelemama,.. Nadhani angeanza na huyo dogo within a week kujikojolea ingekua historia, hata bila kuambiwa mda wakulala ukifika anaongoza mwenyewe chumbani kwake kulala pekeyake.. Halafu angefata mama yake Kuna lifestyle tu moja hivi ya kijeshi angepitishwa kiburi chote na kujitoa ufahamu angeacha..
Kuna watoto wanapigwa na bado wanajikojolea.

Mimi nimesoma shule za boarding tangu nikiwa mtoto. Kuna wakubwa kabisa wanakojoa mno. Na kila siku asubuhi viranja (walikuwa wakubwa mno, wanapiga zaidi ya Walimu) walikiwa wanapita kitanda baada ya kitanda kutembeza bakora. Wanawadunda balaa, lakini kesho yake tena kaliachia.

Lazima tufahamu kuwa, tunatofautiana. Kuna watoto (wakiwepo wangu) hata miaka miwili haiishi, hakojoi tena kitandani.

Kuna wengine wana vibofu vidogo kujikojolea usiku kutakuwepo tu.

Anaweza kupigwa na kupigwa asiache.
 
Nakubali kote ila hapo kwene mtoto wa miaka saba kukojoa et ni sawa !! Bi no

labda n ukoo wenu

sisi miaka 4 nakumbuka nimeacha chekechea
Wapo watoto wagonjwa, hivyo tunapaswa nao kuwaadhibu kwa sababu wanajikojolea?

Ukoo wetu hakuna, ila haimaanishi iwe universal kuwa hata kwa wengine wasiwepo. Hapana.
 
Back
Top Bottom