Vyama Huru vya wafanyakazi Makuli Bandarini waanzishe maandamano, au wafanyakazi wa TPA hawafundishiki kama yalivyokuwa matumaini ya awali ktk makubaliano ya IGA hapa chini yalivyokuwa yanasema neno kwa neno kutoa mafunzo stahiki .....
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI
MAELEZO YA AWALI KUHUSU MAPENDEKEZO YA KURIDHIA
MKATABA BAINA YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA NA SERIKALI YA DUBAI KUHUSU USHIRIKIANO WA
KIUCHUMI NA KIJAMII KWA AJILI YA UENDELEZAJI NA UBORESHAJI WA UTENDAJI KAZI WA BANDARI TANZANIA (INTER-GOVERNMENTAL AGREEMENT - IGA BETWEEN THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND THE EMIRATE OF DUBAI
CONCERNING ECONOMIC AND SOCIAL PARTNERSHIP FOR THE
DEVELOPMENT AND IMPROVING PERFORMANCE OF PORTS IN
TANZANIA)JUNI 2023
Page 1
MAELEZO YA AWALI KUHUSU MAPENDEKEZO YA KURIDHIA
MKATABA BAINA YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA NA SERIKALI YA DUBAI KUHUSU USHIRIKIANO WA
KIUCHUMI NA KIJAMII KWA AJILI YA UENDELEZAJI NA UBORESHAJI WA UTENDAJI KAZI WA BANDARI TANZANIA
A: UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ilianzishwa kupitia Sheria Na. 17 ya mwaka 2004. Mamlaka hii ilirithi na kuchukua majukumu ya iliyokuwa Mamlaka ya Bandari
Tanzania (Tanzania Harbors Authority-THA) iliyoanzishwa kupitia Sheria ya Mamlaka ya Bandari Na. 12 ya mwaka 1977 baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kupewa
majukumu zaidi ya kumiliki, kuendesha na kuendeleza bandari zilizopo pwani ya Bahari ya Hindi na Maziwa Makuu.
2. Mheshimiwa Spika, Sheria hiyo ya Bandari Na. 17 ya Mwaka 2004
inaipa TPA majukumu ya kumiliki, kusimamia, kuendesha na
kuendeleza maeneo yote ya bandari Tanzania Bara. Madhumuni makuu ya kuanzishwa kwa TPA yameainishwa katika Kifungu cha (5) cha Sheria hiyo ambayo ni kuhakikisha Tanzania inaendelea kunufaika na faida ya kijiografia ikiwemo: kuchagiza usimamizi bora na
ufungamanishaji wa tija wa bandari zilizopo pwani ya Bahari ya Hindi na Maziwa Makuu; kuhakikisha kunakuwa na tija katika huduma zinazotolewa za upakiaji na ushushaji wa mizigo pamoja na abiria; kuendeleza, kuboresha na kusimamia miundombinu ya kibandari;
kusimamia usalama wa bandari; na kuingia mikataba au makubaliano na mtu au taasisi yoyote kwa ajili ya utoaji wa huduma za bandari.
Page 2
zitakazo ongeza idadi ya Watalii nchini na kuongeza pato la
Taifa;
xi. Kusimika Mifumo ya TEHAMA kwa ajili ya shughuli za bandari
na kuwaunganisha wadau wake;
xii. Mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa TPA katika Bandari zote (knowledge and skills transfer);
xiii. Uanzishwaji wa Maeneo Maalum ya Kiuchumi/Viwanda; na
xiv. Kuchochea ukuaji wa sekta zingine za kiuchumi zikiwemo
Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi; kuchagiza shughuli za Viwanda na Biashara; kuchagiza ukuaji wa sekta ndogo za
usafirishaji kwa njia ya reli (SGR, TAZARA na MGR) na...
Page 12