Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Msingi Mkuu wa CCM kukataa KATIBA MPYA unatokana na KATIBA ILIYOPO KUWAPA NGUVU Wanasiasa kuliko Watendaji hivyo Wanasiasa kutapanya pesa za wananchi kwa namna wanavyojisikia wao bila hofu ya kufanywa chochote kile. Na fedha hizo wanasiasa wanazitumia kwa maslahi yao binafsi na CCM.
Kusema ukweli TANZANIA sio masikini. Nchi hii ni tajiri sana ila ukweli ni kwamba fedha za walipakodi zimekuwa zikitapanywa na kutumiwa vibaya na Wanasiasa tena hovyo hovyo.
Ujinga wa Watanzania unawafanya pia kushangilia matumizi mabaya ya fedha zao. Na hili ndo linawafanya CCM leo hii kuendelea kung'ang'ania Katiba hii kwa kuwarubuni Watanzania eti Katiba haitawaletea ugali mezani.
Tanzania ndo nchi pekee ambayo Rais anajiamulia tu kununua magoli ya Timu (Club za michezo) bila fedha hizo kuidhinishwa kwenye bajeti yeyote ile alafu watu hawaulizi wala kuhoji chochote kile.
Tanzania ndo nchi ambayo Rais anaweza toa mamilioni ya fedha kununua gari la Askofu au kuchangia ujenzi wa kanisa au msikiti alafu mitanzania ikashangilia au kukaa kimya wakati walipaswa kumuhoji Rais anatumia fedha hizo kutoka kwenye fungu gani lililoidhinishwa kupitia bajeti ipi ya Serikali?
Hawajui kuwa Rais sio mmiliki wa fedha za wananchi. Fedha za wananchi zinapaswa kutumiwa kwa utaratibu ulioidhinishwa na Bunge tu kupitia bajeti iliyopitishwa Bungeni.
Ni ujinga tu wa Watanzania ila kiukweli fedha hizi ndo fedha zinazopaswa kwenda kununulia madawa ya hospitali, kulipa walimu wanaofundisha watoto wetu vizuri ili kuwapa motisha na kurekebisha miundombinu ya barabara ambazo ni mbovu karibia kwenye majiji na vijiji vyote.
Shughuli nyingi za Chama cha Mapinduzi zinazofanyika kwenye Mikoa na Wilaya zinatumia fedha za Serikali kutoka kwenye Ofisi za Halmashauri husika.
Wakurugenzi wa Halmashauri wanatoa mamilioni ya fedha kufadhili shighuli hizo za CCM kwa maelekezo ya Wanasiasa ili kulinda nafasi zao. Fedha hizi zinapaswa kutumiwa kwa shughuli za maendeleo ya wananch kama kuwanunulia madawa hospitali, kuwatengenezea barabara nzuri za lami na zege kwenye mitaa na vijiji vyao na kuwawekea miundombinu mizuri ya maji mpaka majumbani mwao.
Mfano mwingine tumeona jana kwenye sherehe ya miaka 48 ya chama cha Mapinduzi. Idara ya Itifaki ndiyo iliyokuwepo kwenye maadhimisho yale. Kwa maana nyingine fedha za kugharamia maazimisho yale zimetoka Serikalini tena kodi za wananchi.
Kutokana na ujinga wa Watanzania kamwe huwezi kukuta wakiuliza shughuli hizo za CCM zinaghalamiwa kwa fedha zipi zilizotoka wapi ila kila siku wanaona hawana huduma nzuri na kupata mahitaji mazuri ambayo ni haki zao za msingi.
Ila Watanzania hao wakiona Trump kasitisha misaada na ndugu zao wanakosa dawa za ukimwi na kuanza kufubaa huku wengine waliojiriwa kwenye mashirika ya marekani wakikaa nyumbani kwa kukosa kazi bado hawapati akili ya kuanza kudai KATIBA MPYA ili kuwabana vizuri hawa CCM wasitumie fedha zao vibaya na kuwafanya waishi maisha ya kubahatisha.
Hitimisho.
Kama kuna kitu Watanzania wote wanapaswa kukipambanania kwa nguvu zote na namna zote ni KATIBA MPYA.
Lord Denning
Dubai