min -me
JF-Expert Member
- Jul 20, 2022
- 23,322
- 64,738
Kwa hiyo kama mke wangu anatafunwa na jirani ni halali na wako atafunwe mkuu?Ukiondoa south africa nchi zote za africa zinafanana!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo kama mke wangu anatafunwa na jirani ni halali na wako atafunwe mkuu?Ukiondoa south africa nchi zote za africa zinafanana!
Una hoja nzuri sema machawa waliopo hapa watakupinga kwa maslahi yao kwa ufupi sana watanzania tulio wengi bado hatujitambui hko mikoani ndo kabisa hasa mkoa wa dodomaMsingi Mkuu wa CCM kukataa KATIBA MPYA unatokana na KATIBA ILIYOPO KUWAPA NGUVU Wanasiasa kuliko Watendaji hivyo Wanasiasa kutapanya pesa za wananchi kwa namna wanavyojisikia wao bila hofu ya kufanywa chochote kile. Na fedha hizo wanasiasa wanazitumia kwa maslahi yao binafsi na CCM.
Kusema ukweli TANZANIA sio masikini. Nchi hii ni tajiri sana ila ukweli ni kwamba fedha za walipakodi zimekuwa zikitapanywa na kutumiwa vibaya na Wanasiasa tena hovyo hovyo.
Ujinga wa Watanzania unawafanya pia kushangilia matumizi mabaya ya fedha zao. Na hili ndo linawafanya CCM leo hii kuendelea kung'ang'ania Katiba hii kwa kuwarubuni Watanzania eti Katiba haitawaletea ugali mezani.
Tanzania ndo nchi pekee ambayo Rais anajiamulia tu kununua magoli ya Timu (Club za michezo) bila fedha hizo kuidhinishwa kwenye bajeti yeyote ile alafu watu hawaulizi wala kuhoji chochote kile.
Tanzania ndo nchi ambayo Rais anaweza toa mamilioni ya fedha kununua gari la Askofu au kuchangia ujenzi wa kanisa au msikiti alafu mitanzania ikashangilia au kukaa kimya wakati walipaswa kumuhoji Rais anatumia fedha hizo kutoka kwenye fungu gani lililoidhinishwa kupitia bajeti ipi ya Serikali?
Hawajui kuwa Rais sio mmiliki wa fedha za wananchi. Fedha za wananchi zinapaswa kutumiwa kwa utaratibu ulioidhinishwa na Bunge tu kupitia bajeti iliyopitishwa Bungeni.
Ni ujinga tu wa Watanzania ila kiukweli fedha hizi ndo fedha zinazopaswa kwenda kununulia madawa ya hospitali, kulipa walimu wanaofundisha watoto wetu vizuri ili kuwapa motisha na kurekebisha miundombinu ya barabara ambazo ni mbovu karibia kwenye majiji na vijiji vyote.
Shughuli nyingi za Chama cha Mapinduzi zinazofanyika kwenye Mikoa na Wilaya zinatumia fedha za Serikali kutoka kwenye Ofisi za Halmashauri husika.
Wakurugenzi wa Halmashauri wanatoa mamilioni ya fedha kufadhili shighuli hizo za CCM kwa maelekezo ya Wanasiasa ili kulinda nafasi zao. Fedha hizi zinapaswa kutumiwa kwa shughuli za maendeleo ya wananch kama kuwanunulia madawa hospitali, kuwatengenezea barabara nzuri za lami na zege kwenye mitaa na vijiji vyao na kuwawekea miundombinu mizuri ya maji mpaka majumbani mwao.
Mfano mwingine tumeona jana kwenye sherehe ya miaka 48 ya chama cha Mapinduzi. Idara ya Itifaki ndiyo iliyokuwepo kwenye maadhimisho yale. Kwa maana nyingine fedha za kugharamia maazimisho yale zimetoka Serikalini tena kodi za wananchi.
Kutokana na ujinga wa Watanzania kamwe huwezi kukuta wakiuliza shughuli hizo za CCM zinaghalamiwa kwa fedha zipi zilizotoka wapi ila kila siku wanaona hawana huduma nzuri na kupata mahitaji mazuri ambayo ni haki zao za msingi.
Ila Watanzania hao wakiona Trump kasitisha misaada na ndugu zao wanakosa dawa za ukimwi na kuanza kufubaa huku wengine waliojiriwa kwenye mashirika ya marekani wakikaa nyumbani kwa kukosa kazi bado hawapati akili ya kuanza kudai KATIBA MPYA ili kuwabana vizuri hawa CCM wasitumie fedha zao vibaya na kuwafanya waishi maisha ya kubahatisha.
Hitimisho.
Kama kuna kitu Watanzania wote wanapaswa kukipambanania kwa nguvu zote na namna zote ni KATIBA MPYA.
Lord Denning
Dubai
Mkoa wa Dodoma ndo unaongoza kwa mazezeta Tanzania.Una hoja nzuri sema machawa waliopo hapa watakupinga kwa maslahi yao kwa ufupi sana watanzania tulio wengi bado hatujitambui hko mikoani ndo kabisa hasa mkoa wa dodoma
Nenda mahakamani unajifanya unajua kumbe waoga tu ukiambiwa utoke maandamano unatia mashuka mavi!Unaandika ujinga tu, hizo hela wanazotapanya CCM ni kodi zetu. Hoja hapa ni kuwa bajeti inayotengwa kwa ajili ya matumizi ya anasa yz serikali ya CCM ni kubwa mno kulinganisha na bajeti ya huduma na maendeleo ya jamii.
WEwe upoo,haupo?Kuna nchi rais anawapa wachezaji nyumba na magari sembuse magoli mbona ni kidogo sana pili CCM ina majihela na miradi mbali mbali....lissu anasema tuandamane kuitoa ccm je upo tayari!
Mkuu mfano ni tofauti sana!Kwa hiyo kama mke wangu anatafunwa na jirani ni halali na wako atafunwe mkuu?
Zinafanana kitu gani?Ukiondoa south africa nchi zote za africa zinafanana!
Hujafika Marekani ww. Ss hv Republicans wanajigaia posho tyu.Ujinga wa Watanzania ni mtaji mkubwa sana kwa Chama cha Mapinduzi.
😜Matumizi mabaya ya Kodi za umma yamesababishwa na watanzania kukosa elimu.Mtanzania akiona rais katoa zawadi ya milioni kumi Kwa ajili ya goli wanaoamini kabisa ni Hela za rais zimetoka mfukoni mwake.Siku watanzania wakipata elimu kama ilivyo wenzao wakenya ndiyo watapata uchungu wa kuzisimamia Kwa nguvu Kodi zao kuliwa hovyo kama ilivyo Sasa.
Wala rushwa na wezi!Zinafanana kitu gani?
Hapana wenye mapenzi na hii nchi lazima tuisafishe.Ukishindwa kupigana nao jiunge nao.
Vijana mkipata nafasi msiichezee.
CCM wameinajisi nchi, haiwezi kusafishika
hao ndio wajinga wenyewe hao. hata majina ya kijinga wanayo mbaya zaidi Vichwa vyao vimetawaliwa na fikra za wazungu unategemea nn hapo?Tatizo ni hao watanzania wasiokuwa wajinga hatuoni juhudi zao ambazo zitawatofautisha wao na hao wajinga, hao watanzania wasiokuwa wajinga ndio walipaswa kuonyesha juhudi ambayo ingekuwa mfano mzuri kuwaamsha hao wajinga. Hakuna hata asiyemjinga mmoja mwenye kuhoji serikali hadharani, yani ukiacha kulalamika humu mitandaoni hakuna chengine wanachofanya kutoa ujumbe kwa serikali kuonyesha hisia zao.
Tutaendelea tu kuitana wajinga na waoga tumeshaamini hayo maneno tumekubali kujitambua kwa uoga na ujinga.
Hayo yote unayosema hayatafanikiwa maana Katiba ya Marekani imejenga mifumo imara sana.hao ndio wajinga wenyewe hao. hata majina ya kijinga wanayo mbaya zaidi Vichwa vyao vimetawaliwa na fikra za wazungu unategemea nn hapo?
ss Watanzania tuwaaikilize hawa mamluki na vibaraka wa kibeberu?
Rais wa Marekani Donald Trump amekanyaga Katiba ya huko Marekani na karibia kila Executive oreder ametoa., huwasikii hawa wakikemea maovu yake, amempa Netanyahu Billioni za madola, anataka kuvunja wizara ya elimu, kawafukuza kazi wote ambao wanakinzana na sera zake. Huwasikii hawa wakikemea?? Jiulize kwanini
Kuna mambo yanafanywa katika nchi hii mpaka unajiuliza viongozi wetu wana akili timamu kweli.Hapana wenye mapenzi na hii nchi lazima tuisafishe.
Ni kweli CCM wameshainajisi hii nchi na wakati wowote kuanzia sasa tarajieni hii nchi kuwa chini ya Hima Empire.
Hao Walikuwa Wanazurura Na Helicopter Anga La Dodoma, Tu Wakijiona Wapo MawinguniUjinga ni .... hapana upumbavu ni kuwalipa Wasanii ,machawa na viherere wengine kama Kitenge na Zembwela mabilioni ya fedha huku mkuu wa mkoa anasema kama hospital hakuna gloves za kuwa saidia kina mama kujifungua uende na mkasi kwa mumeo ukajifungue.
Upumbavu uliikithiri ni kutumia fedha kwa anasa za hovyo huku unategemea Trump akupe US $514 million za msaada Kila mwaka.
Hizi Yutong Mbona Wanasema Zimechukuliwa Wizara Ya MijegejeEneo linalotumia Kodi zetu
Saivi JWTZ limekuwa Jeshi la Wapiga Picha na kupenda sifa.Hizi Yutong Mbona Wanasema Zimechukuliwa Wizara Ya Mijegeje